Mbinu Zinazo Aminika Kudhibitisha Jinsia Ya Mtoto Anaye Tarajiwa

Mbinu Zinazo Aminika Kudhibitisha Jinsia Ya Mtoto Anaye Tarajiwa

Kuna vipimo vingi tofauti ambavyo mama anaweza tumia kujua iwapo ama mimba ama la, kama vile kwa kupima mimba kiasili. Baada ya kugundua kuwa ana mimba, atakuwa na maswali mengi kichwani. Kila mzazi angependa kujua jinsia ya mtoto anaye tarajia. Kwa kufahamu jinsia ya mtoto wake, ataweza kuanza kujipanga na mavazi atakayo mnunulia na kununua yanayo faa. Kupima mimba kiasili kunakusaidia kugundua iwapo una mimba lakini ili kufahamu jinsia ya mtoto wako, unapaswa kufanyiwa vipimo zaidi.

Ili kupata kipimo sawa cha mtoto ambaye hajazaliwa, ni vyema kuwasiliana na daktari wa afya ya kike. Ata tumia mbinu zinazo egemezwa na sayansi na zinazo aminika zaidi kudhibitisha jinsia ya mtoto wako.

Vipimo Vya Kudhibitisha Jinsia Ya Mtoto

Kipimo cha ultrasound

kupima mimba

Kipimo hiki cha 2-D ultrasounda kina fanyika katika wiki 20 za ujauzito na ni njia shwari ya kujua jinsia ya mtoto wako na asilimia 98.2 ya kuwa sahihi. Inafanywa na daktari wako ama mtaalum wa ultrasound na itakusaidia kuona picha ya mtoto wako alivyo tumboni hata genetalia yake inayo kua. Na picha hizi zinakusaidia kuhakikisha jinsia ya mtoto aliye tumboni mwako.

Kipimo cha DNA

Vipimo tofauti vya DNA vinafanyika na kupitia usaidizi wa sampuli za damu, vinaweza dhibitisha jinsia ya mtoto. Vipimo kama vile Maternit21, Verifi, Harmony na Panorama ni vipimo vya damu vinavyo angalia kuwepo kwa chromosome Y. Kwa sababu jinsia ya kike haina chromosome hiyo, kuwepo ama kutokuwepo kwa chromosome hiyo kuta dhibitisha jinsia ya mtoto. Sampuli iliyo na chromosome Y ina maanisha kuwa mtoto ni wa kiume, na kukosekana kwake kuna dhihirisha kuwa mtoto anaye tarajiwa ni wa kike.

Mbinu Zinazo Aminika Kudhibitisha Jinsia Ya Mtoto Anaye Tarajiwa

Kipimo cha amniocentesis

Kipimo hiki kina fanywa na daktari aliye na maarifa ya kipimo hiki. Kiwango kidogo cha ugiligili wa amniotic kutoka kwa mwanamke aliye na mimba kinachukuliwa kwa kutumia sindano. Ugiligili huu huwa na seli zinazo mwagika kutoka kwa fetusi, kisha zina pimwa kudhihirisha ikiwa fetusi ina changamoto zozote. Pia seli hizi zinaweza onyesha jinsia ya mtoto.

Vipimo tulivyo angazia vina saidia kudhibitisha jinsia na afya ya fetusi inayo kua, tofauti na kupima mimba kiasili, mama anaweza kufahamu ikiwa mtoto anaye tarajia ana changamoto zozote za kimaumbile. Una shauriwa kutegemea mbinu hizi ili kuwa una uhakika kuhusu jinsia ya mtoto wako.

Vyanzo: Healthline, Medical News Today

Soma Pia:Jinsia Ya Kujua Iwapo Una Mimba Kabla Ya Kufanya Kipimo

Written by

Risper Nyakio