Vidokezo Muhimu Kwa Mama Mwenye Mimba

Vidokezo Muhimu Kwa Mama Mwenye Mimba

Kuna njia nyingi ambazo mama anaweza tumia kujua kama ana mimba ama la. Soma zaidi ufahamu njia zinazo aminika zaidi.

Kuna ujumbe mwingi kwenye mitandao, vitabu, marafiki, familia na jamii kuhusu ujauzito. Wote wana hamu ya kumwambia mama mwenye mimba anacho paswa kufanya na asicho kubalika kufanya. Ushauri ambao mama mjamzito anapatiwa ni kama vile, jinsi ya kupima mimba kienyeji, matunda anayo paswa kula, vyakula anavyo paswa kuepuka na kadhalika.

Kufuatia wingi wa ujumbe ambao mama mjamzito atapatiwa, ni vyema kuwasiliana na daktari wake ama kwenda kwenye kituo cha afya ili apate ushauri wa kimatibabu. Pia huenda ukapata kuwa wavyele wako wana kushauri kufanya mambo ya jadi yaliyo pitwa na wakati. Hakikisha kuwa ushauri unao amua kufuata umedhibitika kimatibabu.

Makala haya yana elimisha wanandoa walio na mimba vidokezo muhimu wanavyo paswa kukumbuka wakati wote.

Vidokezo muhimu kwa mama mwenye mimba

jinsi ya kupima mimba kienyeji

  • Wasiliana na mtaalum wa afya

Mara tu baada ya kupima mimba kienyeji ama kwa kutumia kifaa cha kupima ujauzito, enda kwenye hospitali kudhihirisha matukio uliyo yapata. Kwa njia hii, utakuwa na uhakika na pia utapata mtaalum wa afya atakaye kushauri hatua unazo paswa kufuata. Pia atafanya vipimo kuhakikisha kuwa hauna matatizo yoyote ya kiafya. Anza utunzi wa kabla ya kujifungua mapema iwezekanavyo. Vitamini hizo ni muhimu sana katika ukuaji wa uti wa mgongo na ubongo wa mtoto wako.

  • Kufanya mazoezi mepesi

Wanawake wengi wanapo pata mimba, wao hupuuza afya yao na kukoma kufanya mazoezi. Na kuhatarisha maisha yao na ya mtoto. Kufanya hivi kuna sababisha mtoto kuwa mnene na mama pia anapata uzito mwingi kupindukia. Uko katika hatari ya kujifungua kupitia upasuaji ikiwa mtoto atakuwa na uzito mwingi. Kufanya mazoezi kunamsaidia mama kuwa na uzito sawa wa mwili, mtoto kukua ipasavyo na kufanya utaratibu wa kujifungua uwe rahisi.

Wasiliana na mtaalum wa mazoezi na uhakikishe kuwa unafanya mazoezi mepesi ambayo hayata hatarisha mtoto anaye kua tumboni mwako.

how to prevent miscarriages

  • Kula lishe yenye afya

Huenda ikawa vigumu kuzingatia lishe yenye afya ukiwa na mimba kufuatia hamu za kula vyakula tofauti zinazo sababishwa na mimba. Kumbuka kuwa mtoto anaye kua tumboni mwako anategemea chakula unacho kula. Hakikisha kuwa unapata virutubisho vyote kutoka kwa chakula unacho kila ili mtoto akue na afya. Protini, vitamini na kalisi ni muhimu sana katika kipindi hiki.

vyakula vya mama mwenye mimba

  • Koma kutumia vileo, sigara na kahawa nyingi

Baada ya kufanya kipimo cha mimba hospitalini ama kwa njia mbadala kama vile jinsi ya kupima mimba kienyeji, na kupata matokeo chanya, kuwa mwangalifu wa afya yako. Afya njema ina husisha vitu unavyo viweka mwilini wako. Chochote unacho kila ama kunywa kinaenda kwa mtoto wako. Sigara na pombe mweka mtoto wako katika hatari ya kuzaliwa na kasoro ama ulemavu. Kunywa kahawa nyingi katika siku za kwanza za mimba huenda kuka sababisha kuharibika kwa mimba. Ni vyema kuwa makini na vitu unavyo kunywa na kula.

  • Punguza fikira nyingi

Kukwazwa kifikira kuta athiri afya yako na ya mtoto wako. Hakikisha una kaa mbali na mambo yanayo kufanya kuwa na fikira nyingi. Fanya kazi nyepesi zisizo shinikiza mgongo wako. Wasiliana na daktari wako kuhusu wakati unaopaswa kuenda mapumziko ya mama mjamzito.

Mama mjamzito ana shauriwa kuwa mwangalifu wa afya yake na kuona mabadiliko kwenye mwili wake. Ni rahisi kuhisi uchungu kwenye tumbo na kudhani kuwa ni kawaida, ila huenda uchungu huo ukawa ishara ya ugonjwa. Unapo gundua jambo lolote lisilo la kawaida, wasiliana na daktari wako.

Soma pia:Lishe Ya Ujauzito: Ratiba Ya Chakula Cha Ujauzito Cha Nigeria

Written by

Risper Nyakio