Usipo kuwa na uhakika kuhusu hali yako ya mimba, huenda ukafanya uamuzi wa kujaribu kipimo cha mimba cha nyumbani. Kuna anuwai nyingi za vipimo vya mimba vya nyumbani ambavyo unaweza kujaribu. Tuna kuelimisha jinsi ya kupima mimba kutumia siki ukiwa nyumbani mwako. Kutumia kiungo kinacho patikana kwa urahisi jikoni mwako, na bila gharama zozote.
Hata ingawa ujumbe wa vipimo hivi vya kinyumbani viko kwenye tovuti nyingi. Sio waandishi wengi wanao chukua muda kutafiti zaidi iwapo mbinu hizi zina egemezwa kisayansi.
Jinsi ya kupima mimba kutumia siki

Maagizo
- Tumia chupa safi na inayo kuwezesha kuona kinacho tendeka ndani.
- Tumia mkojo wa kwanza baada ya kuamka kabla ya kutia chakula chochote mdomoni. Mkojo huu una viwango vya juu vya kichocheo cha hCG.
- Weka nusu kikombe cha mkojo kwenye chupa hiyo.
- Ongeza kikombe kimoja cha siki ama vinegar
- Ngoja dakika tano kuona kitakacho fanyika
- Unapo ona mabadiliko kwenye chupa hiyo, hiyo ni ishara kuwa una mimba.
- Siki hiyo inapo baki kama ilivyo kuwa hapo awali, ni ishara kuwa hauna mimba.
Ikiwa una shaka kuhusu mapato ya kipimo hiki, tazama dalili za mapema ambazo zitakusaidia kujua ikiwa kwa kweli una mimba ama la.
Dalili za mapema za ujauzito
- Kukosa kipindi cha hedhi
- Kuhisi uchovu wakati wote
- Haja ya kuenda haja ndogo mara kwa mara
- Chuchu zilizo fura
- Kichefu chefu na kutapika
- Ugonjwa asubuhi
- Kuumwa na mgongo
Usahihi wa kipimo cha nyumbani cha mimba

Kufuatia kukosa utafiti wa kisayansi wa kuegemeza vipimo vya kinyumbani vya mimba, usahihi wake sio bayana. Kufuatia sababu hii wanawake wengi hununua kipima mimba baada ya kufanya kipimo cha mimba. Ili kuwa na uhakika kuhusu matokeo waliyo yapata.
Vifaa vya kupima mimba vinapatikana kwenye zahanati, hospitali ama duka kubwa za dawa. Pia, unaweza tembea kwenye kituo cha afya kufanyiwa vipimo. Kipimo cha damu kudhibitisha hali ya mimba huwa sahihi zaidi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ambavyo Mwanamke Anaweza Kuongeza Nafasi Zake Za Kutunga Mimba