Kipimo Asili Cha Mimba Kilicho Maarufu Zaidi

Kipimo Asili Cha Mimba Kilicho Maarufu Zaidi

Kipimo cha mimba kutumia chumvi ni kipimo kinacho kuruhusu kupata matokeo kwa kasi, ukiwa nyumbani mwako, bila gharama yoyote na kwa usiri wako.

Kwa sekunde moja, fikiria kuwa wewe ni mwanamke anaye ishi katika miaka ya 1920. Na yote ambayo wanawake walipitia katika enzi hizo. Njia yao ya maisha na mitindo ya mavazi na nywele. Una shuku kuwa huenda ukawa na mimba, ila, hauna uhakika. Je, utafanya nini? Unadhani wanawake katika enzi hizo walitumia mbinu zipi kutabiri iwapo wana mimba? Jinsi ya kupima mimba kwa chumvi ama kungoja hadi wakose kipindi chao cha hedhi?

Leo hii, vipimo vya mimba vinapatikana kwa urahisi kwenye duka za dawa, maabara na zahanati. Lakini vipimo hivi havikuwa vimepitishwa hadi mwaka wa 1976.

Kupima mimba kiasili

Kwa hivyo katika enzi za kale, wanawake walitumia vipimo asili vya kupima mimba ama kungoja ishara za mimba kama vile kukosa kipindi cha hedhi, ugonjwa wa asubuhi, uchovu na tumbo kunenepa. Vipimo vya jinsi ya kupima mimba kiasili ama kienyeji vilitumika kuonyesha kuwepo kwa mimba. Mojawapo ya vipimo maarufu ni jinsi ya kupima mimba kwa chumvi. Ambapo chumvi, kontena ndogo na mkojo vilitumika kudhihirisha iwapo mwanamke ana mimba ama la.

Jinsi ya kupima mimba kwa chumvi

kupima mimba kutumia chumvi

Jinsi kipimo hiki kinavyo fanyika.

Kulingana na vyanzo vyetu vinavyo dhihirisha kuwa vipimo hivi haviegemezwi kisayansi. Utahitaji vitu hivi:

  • Kontena safi na wazi inayo kuwezesha kuona kinacho fanyika ndani
  • Kiwango kidogo cha mkojo wako wa asubuhi kabla ya kunywa kiamsha kinywa
  • Kijiko kimoja ama viwili vya chumvi

Kuna aina tofauti za chumvi zinazo patikana kwenye maduka lakini kipimo hiki hakija onyesha aina hasa unayo paswa kutumia, kwa hivyo ni sawa kutumia chumvi ya aina yoyote ile.

Jinsi ya kufanya kipimo hiki

1.Weka chumvi kwenye kontena safi

2. Chukua kiwango kidogo cha mkojo wako wa asubuhi

3. Weka mkojo kwenye kontena safi

4. Kisha ungoje

Jinsi ya kusoma matokeo

kupima mimba kutumia kitunguu maji

Matokeo hasi

Ikiwa hakuna kitu kitafanyika, ina maana kuwa matokeo hayo ni hasi.

Matokeo chanya

Vitu vilivyo kwenye kontena vikibadilika viwe na rangi nyeupe sawa na ya maziwa, una tarajia mtoto.

Kipimo cha mimba kutumia chumvi ni kipimo kinacho kuruhusu kupata matokeo kwa kasi, ukiwa nyumbani mwako, bila gharama yoyote na kwa usiri wako. Hakuna atakaye fahamu kuwa ulijaribu kufanya kipimo hiki. Ila, ni vyema kukumbuka kuwa kipimo hiki hakija dhihirishwa kuwa na matokeo sahihi kisayansi. Kwa hivyo baada ya kufanya kipimo hiki nyumbani, hakikisha kuwa una tembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe ili kupata majibu sahihi.

Chanzo: Healthline

Soma Pia:Mbinu Ya Kupima Mimba Kutumia Baking Soda Ni Ya Kuaminika Ama La?

Written by

Risper Nyakio