Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Njia Ya Kienyeji

Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Njia Ya Kienyeji

Jinsi ya kupima mimba kwa njia asili.

Kuna njia nyingi ambazo wanawake wanaweza tumia kupima iwapo wana mimba ama la. Njia zinazo julikana zaidi ni kuwatembelea wataalum ama kununua vifaa vya kupima mimba ukiwa nyumbani. Huenda ukataka kujua hali yako ya ujauzito ukiwa nyumbani. Ni vyema kujua jinsi ya kupima mimba kienyeji ili uweze kupima bila ya kuhangaika kutafuta vifaa vinavyo tumika kwa mara nyingi. Vifaa hivi vinapatikana kwa maabara, zahanati ama kwa hospitali na vituo vingine vya afya. Pima mimba kwa mazingara uliyo yazoea na kwa kutumia kiungo ambacho kinapatikana nyumbani mwako.

Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Njia Ya Kienyeji

Jinsi Ya Kupima Mimba Kienyeji

Njia inayo julikana zaidi ya kupima mimba ya kienyeji ni kwa kutumia chumvi. Chumvi ni kiungo cha jikoni ambacho huwezi kikosa kwenye kila nyumba. Pia ni rahisi kupata na kununua iwapo ungependa kununua chumvi hasa ya kufanya kitendo hiki. Ikilinganishwa na vifaa vingine vya kupima mimba, chumvi ina bei nafuu na pia hauhitajiki kufanya kwenda kwa zahanati kuinunua.

Kutumia chumvi kupima mimba

Kipimo hiki kimekuwa kikitumikwa kwa miaka mingi kupima mimba unapokuwa nyumbani. Hauhitaji vitu vingi na pia ni cha bei nafuu kwani hakuna kitu kipya unacho hitajika kununua. Mahitaji unayopaswa kuwa nayo ni chumvi(vijiko viwili), kontena safi na mkojo wa asubuhi.

jinsi ya kupima mimba kienyeji

Hakuna mbinu hasa unayopaswa kufuata kufanya kipimo hiki. Unapaswa kutumia mkojo wa kwanza punde tu unapo amka kwani una kiwango cha juu cha HCG. Weka mkojo huo kwenye kontena yako safi kisha uongeze chumvi ulio itenga na ungoje kwa masaa machache, kwa kawaida mawili. Iwapo mkojo huo unapata rangi nyeupe, kulingana na kipimo hiki una mimba. Iwapo mchanganyiko ule utabaki rangi asili, hauna mimba.

Hakuna sayansi nyuma ya imani kuhusu kipimo hiki, iwapo kina udhabiti ama la. Utafiti zaidi unaendelea kufanyika ili kudhihirisha iwapo imani hizi ni za kweli. Tuna shauri watu kufanya vipimo vya hospitali ama kutembelea zahanati iliyo karibu zaidi na wao kubainisha iwapo wana mimba ama la baada ya kufanya kipimo cha mimba kwa kutumia chumvi.

Written by

Risper Nyakio