Ikiwa umekuwa ukijaribu kupata mimba kwa muda mrefu, huenda unapo anza kushuku kuwa una mimba hautakuwa na uvumilivu wa kungoja hadi utakapo anza kushuhudia ishara. Ili kudhitibitisha kuwa una mimba. Furaha ya kutaka kujua kama una tarajia mtoto itakufanya ufanye kipimo ili ujue matokeo mapema. Habari njema ni kuwa siku hizi, tofauti na hapo awali, unaweza jua ikiwa una mimba ingali changa ya wiki mbili. Kuna mbinu nyingi za kinyumbani zitakazo kusaidia kujua ukweli. Tuna jadili zaidi kuhusu jinsi ya kupima mimba nyumbani.
Jinsi ya kupima mimba nyumbani
Mbinu hizi tunazo angazia za kupima mimba ukiwa nyumbani zitakusaidia kufanya kipimo cha mimba ukiwa kwa starehe zako nyumbani. Uzuri wa kutumia mbinu hizi ni kuwa, hautatumia gharama yoyote kwani unatumia bidhaa ulizo nazo nyumbani mwako.
1.Poda ya kuoka

Watu wengi wana poda ya kuoka manyumbani mwao. Hasa kama u-miongoni mwa watu wanao penda kuoka mikate na keki zao nyumbani. Kipimo cha mimba kutumia baking soda ni maarufu sana na pia ni rahisi kufanya. Kwa kontena safi na inayo kuruhusu kuona ndani, ongeza kijiko kimoja cha poda ya kuoka. Kisha uongeze mkojo wako wa asubuhi. Unashauriwa kufanya kipimo hiki baada tu ya kuamka kabla ya kula ama kunywa chochote. Ikiwa rangi itabadilika na kuwa nyeupe ama kutoa sauti, hongera! Kwani una mimba!
2. Kutumia kitunguu
Kata kipande cha kitunguu kisha uingize ndani ya uke wako. Ukiamka asubuhi na harufu ya mdomo wako ni ya kitunguu, hauna mimba. Ikiwa hauna harufu ya kitunguu, una mimba.
3. Maziwa freshi
Ongeza maziwa kwenye kontena kisha uweke mkojo wako wa asubuhi. Ziki changanya kisha kuwe na rangi nyeupe, hongera mama! Una tarajia kuwa mama.

4. Sabuni ya nywele
Shampoo ya nywele ni bidhaa ambayo wana dada wengi huwa nayo bafuni mwao. Hii si bidhaa ya kuosha nywele tu, ila ni bidhaa muhimu sana unapo taka kupima mimba. Kwenye bakuli safi na wazi, ongeza kiwango kidogo cha mkojo wa asubuhi kisha uongeze shampoo. Mchanganyiko huu ukibadili rangi, nafasi kubwa ni kuwa una mimba.
5. Siki (Vinegar)
Ndani ya kontena safi, weka sika kisha uongeze mkojo wako na utazame kitakacho tendeka. Rangi ikibadilika, hiyo ni ishara kuwa baada ya miezi tisa utakuwa mama.
6. Sabuni
Kata vipande vidogo vya sabuni kisha uongeze mkojo wako wa asubuhi. Ikiwa una mimba, povu zitaonekana. Ila kama hakuna povu zitakazo tokea hauna mimba.
Soma Pia:Jinsi Ya Kutatua Uchungu Wa Nyonga Katika Mimba