Jinsi Ya Kurefuka Zaidi: Nini Wazazi Wanaweza Fanya Kuwasaidia Watoto Kufika Urefu Unaofaa

Jinsi Ya Kurefuka Zaidi: Nini Wazazi Wanaweza Fanya Kuwasaidia Watoto Kufika Urefu Unaofaa

Huenda urefu wa mtoto ukadhibitiwa na jeni zake, ila kuna mbinu za kumsaidia kufika urefu unao mfaa. Soma vidokezo vitatu vya jinsi ya kumsaidia mtoto wako kurefuka.

Watoto wanapo anza kuzeeka, wana anza kuwa makini na fizikia yao inavyo onekana. Swali moja hasa ambalo watoto huenda wakaanza kuuliza mapema ni jinsi ya kurefuka. Hii ni kwa sababu urefu ni kitu ambacho kinapimwa na kufuatiliwa kama mojawapo ya ukuaji wa mtoto kutoka wakati wanapo kuwa wadogo hadi wanapo fikisha urefu wa mwili wako, na kwa hivyo wana juzwa kulihusu wangali wachanga. Watoto huanza kujishughulisha na jinsi ya kurefuka zaidi wanapo anza kujihusisha na michezo ambapo urefu ni muhimu. Kwa mfano, katika mbuga, ama michezo ambapo kuna urefu unao takikana. Watoto wanapo fahamu kuwa hawawezi jiunga kwa sababu wao sio warefu vya kutosha, wana anza kutamani wakati ambapo watafikisha urefu unao hitajika.

Watoto wanao funzwa kuogelea pia kuanza kujua urefu wa bwawa la maji ikilinganishwa na urefu wao. Wanapo zidi kukua warefu muda unapo zidi kupita, wanaanza kugundua kuwa wanaweza tembea chini zaidi kwenye urefu wa bwawa hilo bila vichwa vyao kuenda chini ya maji. Kwa sababu ya mambo kama haya, watoto huwa na hamu ya kuwa warfu, na kuanza kufikiria jinsi ya kukua warefu zaidi.

Kama wazazi, huenda pia ukawa unashangaa kile ambacho unaweza fanya kukusaidia kuboresha ukuaji wa mtoto wako. Urefu wa mtu unadhibitishwa na jeni zake. Watoto ambao wana wazazi warefu wana nafasi zaidi za kuwa warefu ikilinganishwa na wale ambao wazazi wao wana urefu wa wastani ama chini. Bado, kuna vitu vichache ambavyo unaweza himiza mtoto wako kufanya ili kusaidia kukumbana na tatizo la jinsi ya kurefuka.

Jinsi ya Kurefuka zaidi na usaidizi wa kulala

how to grow taller sleeping

Usingizi ni muhimu sana kwa ukuaji wa akili na fizikia ya mtoto. Iwapo unashangaa jinsi ya kurefuka na msaada wa usingizi, ni kwa sababu homoni za ukuaji zinakua wakati wa kitendo hiki. Kwa hivyo, bila usingizi wa kutosha, watoto huenda wakawa hawapatii miili yao wakati tosha wa kukua na kupata nishati mpya.

Watoto wenye umri wa miaka 3-5 wana hitaji masaa 11-13 ya usingizi kila usiku. Watoto kutoka umri wa miaka 5 hadi 10 wana hitaji kulala kwa angalau masaa 10 hadi 11. Watu wachanga na wenye umri wa kutoka miaka 10 hadi 17 wanahitaji masaa manane na nusu hadi tisa na nusu ya usingizi kila siku.

Kurefuka na usaidizi wa lishe yenye virutubisho
how to grow taller

Hakikisha kuwa mtoto wako anakula ipasavyo

Lishe bora haiwasaidii watoto kuwa na nguvu na afya. Pia inasaidia miili yao kufikisha kiwango cha juu cha uwezo wao wa kukua. Ukihusihsa protini kiwango tosha kwenye lishe ya mtoto wako, zinazo julikana kama vyakula vya ukuaji vinaweza fanya tofauti. Katika wakati huo, unapaswa kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata vitamini na madini kila siku kupitia kwa matunda na mboga.

Kurefuka na usaidizi wa mazoezi

Jinsi Ya Kurefuka Zaidi: Nini Wazazi Wanaweza Fanya Kuwasaidia Watoto Kufika Urefu Unaofaa

Mazoezi yana saidia mwili kuwa na nguvu, kupigana na uzito mwingi wa mwili na kuhimiza misuli kukua. Katika wakati huo huo, mazoezi ya fizikia yana imarisha maendeleo ya homoni za ukuaji na huenda kuka sababisha mifupa yenye nguvu na mirefu. Kunyoosha pia husaidia kurefusha uti wa mgongo, kukaa vizuri na kufanya watoto wasimame wima na wawe warefu.

Wazazi huwa na jukumu kubwa katika ukuaji wa watoto. Jinsi ya kurefuka zaidi huenda kukawa ni jambo ambalo hukusumbua. Kwa kuwasaidia watoto wao wakomae na kufikisha kiwango cha juu kulingana na miili yao kwa kutumia vidokezo rahisi tulivyo angazia. Unapaswa kuwaona wakisimama wima, wakiwa warefu na wenye afya.

Soma pia: Top 8 foods to feed your child so that they grow taller and stronger

Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye theAsianparent Philippines kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio

Written by

Risper Nyakio