Jinsi Ya Kushika Nywele Kwa Mtindo Wa Bantu Knots

Jinsi Ya Kushika Nywele Kwa Mtindo Wa Bantu Knots

Bantu knots pia maarufu kama Zulu knots zimekuwa zikutumika kwa muda mrefu. Hasa hapo awali na mama zetu. Tumeona models wa bara la Afrika wakishika nywele zao na staili hii wanapo wakilisha bara letu. Ni njia rahisi sana ya kuhakikisha kuwa hauna “siku mbaya za nywele”. Kwa kuhakikisha kuwa nywele yako inakaa poa na kuupa uso wako muundo tofauti.

Umuhimu wa kushika nywele yako kwa mtindo wa bantu knots ni upi?

bantu knots

 

  • Zinasaidia katika ukuaji wa nywele bila kutumia joto.
  • Ni njia ya gharama ya chini ya kubadili unavyo kaa.
  • Zinaweza tumika kwa nywele za urefu wowote.
  • Unapo zifumua, zina fanya nywele yako kuwa na curls za kupendeza.
  • Tuna angazia njia za kusonga ama kutengeneza Bantu knots

Siku hizi ikilinganishwa na hapo awali, wanawake wanataka mitindo ya nywele ambapo wanatumia nywele zao asili ila si kuweka nywele za kutengenezwa. Kwa sababu hii, bantu knots zimekuwa kwa ongezeko kuu wasichana wakitaka kusongwa hivi. Tuna angazia jinsi ya kutengeneza staili hii inayosifika kw asana.

Safisha nywele zako

Unapo songwa mtindo huu, kuna sehemu ya kichwa chako ambayo hubaki ikionekana, ni vyema kuhakikisha kuwa kichwa chako ni kisafi. Tumia vifaa vyako vya kuosha nywele kisha uhakikishe uzi suuze kwa kutumia maji safi.

 

Kausha nywele yako

Baada ya kuosha na kusuuza nywele zako, chukua kitambaa kisafi na ukaushe nywele yako. Kuhakikisha kuwa hauna maji yanayo mwagika kwenye mgongo na nguo zako unapo tengeneza nywele zako. Chagua iwapo unataka kutumia nywele zilizo kauka zaidi ama kiasi kidogo.

Jinsi Ya Kushika Nywele Kwa Mtindo Wa Bantu Knots

Picha:Shutterstock

Zigawanye nywele zako

Hii ni sehemu muhimu sana katika safari yako ya kutengeneza mtindo huu. Tafuta vitu vya kushika kila kitita cha nywele unacho gawa. Vigawe vitita hivi kulingana na saizi ya bantu knots unazotaka, kutoka kwa konde hadi kwa nene zaidi.

Tengeneza kana kwamba kamba

Baada ya kugawa nywele yako kwa vitita tofauti, zi twisti kana kwamba unatengeneza kamba. Paka mafuta ya nywele unayotumia. Kuna mafuta hasa ya kutengeneza knots hizi. Kwa njia hii unahakikisha kuwa nywele yako inapata virutubisho vinavyo faa na pia ina maji tosha ambayo ni muhimu katika ukuaji wake. Hakikisha unapo itwisti nywele yako hauikazi sana ila unafanya kadri inavyo takikana.

Ifunge nywele

Chukua kila kitita ulicho tengeneza kamba kisha uiviringe kwenye sehemu ya chini ya kitita hicho. Tumia vipini kuhakikisha kuwa umeshika kila kitita vyema kisije kikatokana. Jiangalie kwa kioo, unapendezwa na matokeo unayo yaona? Uzuri wa staili hii ni kuwa inaweza baki kichwani mwako hadi kwa wiki 1 ama 2.

Uzuri wa kuifunga nywele yako hivi ni kuwa una uhuru wa kucheza na kujaribu njia tofauti za kuiweka nywele hivi.

Mitindo tofauti unayo weza kutumia

Kwa mfano, unaweza ipaka nywele yako rangi kisha uweke staili hii. Kulingana na ujasiri wako, unaweza tumia rangi tofauti kama vile nyekundu, kinjano ama hata pinki ama buluu. Kisha uzishike nywele zako kwa kutumia mwongozo tulio angazia.

Una weza jaribu unene tofauti.

Walio na nywele ndefu watapendeza zaidi wakifuga nywele hizi zikiwa nyembamba huku walio na nywele fupi wakijaribu bantu knots nene. Ila, haya ni maoni yangu tu na u-huru kujaribu chochote kinacho kufurahisha kuona itakavyo kukalia kichwani mwako.

bantu knots

Kuweka mapambo kichwani

Hauja thibitiwa kuwacha nywele bila kuweka mapambo. Tafuta mapambo tofauti kisha uyaweke kwenye knots hizi ulizo tengeneza.

Kusonga nywele

Kama unavyo songa nywele staili tofauti, unaweza songa laini kisha zifuate muundo wa bantu knots.

Kwa dada zetu walio na dreadlocks, pia hawajabaki nyuma. Mbali na kushika nywele kama ilivyo kaawaida, shika nywele zako kama bantu knots. Ili kubadili staili ulizo zoea.

Kinacho pendeza zaidi ni kuwa unaweza shika knots zako zikiwa mrefu ama fupi, kulingana na unavyo jihisi. Baadhi ya watu maarufu wameonekana kwa umma na staili hii. Usibaki nyuma! Jaribu uone utakavyo pendeza!

Vyanzo: wikihow, Darlingafrica

Written by

Risper Nyakio