Maagizo Ya Jinsi Ya Kutayarisha Poda Ya Maharagwe Ya Soya

Maagizo Ya Jinsi Ya Kutayarisha Poda Ya Maharagwe Ya Soya

Maziwa ya soy yana manufaa mengi ya kiafya! Iwapo ungependa maziwa ya soy yaliyo tengenezewa nyumbani, soma zaidi upate vidokezo vya jinsi ya kutayarisha poda ya maharagwe ya soya.

how to prepare soya beans powder

Maziwa ya soy ni tamu na yenye ladha!

Jinsi ya kutayarisha poda ya maziwa ya maharagwe ya soy

Viungo
 • 2 vikombe vya  maharagwe ya soy
 • 10 vikombe vya maji
 • 1 ndizi ambayo haija iva
 • ½ kikombe cha njugu zilizo kaangwa
 • Asali, sukari (kwa hiari yako)
 • 3 vijiko vya poda ya crayfish (kwa hiari yako)
Maagizo – jinsi ya kutayarisha poda ya maharagwe ya soya

soya beans powder

Hatua ya 1 – Kuosha na kutayarisha maharagwe ya soya

Chagua maharagwe yako ya soya kwenye tray na utupe zilizo haribika

Lazima uchague maharagwe yako ya soya kwa njia sawa kama ungefanya kwa aina zingine za maharagwe. Huku kutasaidia kuziweka mbali na uchafu na kufanya mchakato wa kusiaga uwe rahisi zaidi. Kujua jinsi ya kutengeneza maharagwe ya poda ya soya itaanza kulingana na usafi wa maharagwe yako.

Osha maharagwe ya soya na uziwache usiku zikauke

Maharagwe lazima yawe yamekauka kabla ya kukaanga. Vinginevyo, ni vigumu kupata poda iliyo laini. Maharagwe yako ya poda ya soya huenda yakatoka na sehemu ngumu iwapo maharagwe yalikuwa na maji. Katika hatua hii, angalia iwapo yana mawe ama uchafu.

Kwenye kaangio, choma maharagwe yako ya soya hadi ziwe na rangi ya hudhurungi na utoe maganda kwa urahisi

Unapo choma maharagwe yako ya soya, unapaswa kuchanganya mara kwa mara kwenye moto wa kiwango cha chini ili yasiungue. Utachoma kama vile ungechoma njugu.

Siaga maharagwe yako ya soya yangali moto

Utapata poda laini uki siaga maharagwe punde tu baada ya kuyatoa kwenye moto. Inapo poa, kuna nafasi kuwa huenda yakashikana. Una shauriwa kuichoma baada ya kutayarisha viungo vingine.

jinsi ya kutayarisha poda ya maharagwe ya soya

Jinsi ya kutayarisha poda za maharagwe za soya kuendeleza.

Hatua ya 2 – kutayarisha ndizi mbichi
 • Osha na utoe maganda ya ndizi mbichi
 • Kata kata ndizi yako kwenye vipande vichache na uziwache kwenye jua zikauke
 • Mbadala, iwapo hauna jua tosha ya kukausha, unaweza kausha ndizi zako kwenye oven
 • Ama pia, unaweza ruka mchakato huu wa kukausha iwapo utanunua vibanzi vya ndizi zilizo tengenezwa kutoka sokoni na uvikaushe
Hatua ya 3 – kutayarisha njugu
 • Kaanga njugu zako kwenye kikaangio hadi ziwe na rangi ya hudhurungi, kisha uziweke kando zipoe
 • Toa maganda ya njugu uzitenganishe njugu na maganda
Hatua ya 4 – kusiaga viungo vyote
 • Weka viungo vyote kwenye kifaa cha kusiaga kisha usiage
 • Hifadhi poda kwenye kontena isiyo kubalisha hewa kuingia

Maziwa ya soy yana ladha na ni tamu. Iwapo unahisi ungependa kuwa mbunifu baada ya kusoma jinsi ya kutayarisha maharagwe ya poda ya soya, unaweza ongeza ladha ya vanilla, mint na kahawa. Iwapo unawalisha watoto wako maziwa ya soy, unaweza ongeza crayfish ili kuongeza ladha.

Faida za kiafya za maziwa ya soy

Iwapo unataka kujua jinsi ya kutengeneza poda ya maharagwe ya soy, bila shaka unataka kusoma kujua jinsi ya kutengeneza maziwa ya soy ukiwa nyumbani. Maziwa ya soy yana ladha na afya na hii ndiyo sababu unapaswa kuiongeza kwenye lishe yako.

1. Maziwa ya soy yana vitamini na madini ambazo ni nzuri kwa mwili wako.

2.  Kunywa maziwa ya maharagwe ya soy kuna saidia kupunguza mafuta zaidi mwilini na kuimarisha afya ya moyo wako.

3. Watu wanao ugua kutokana na kisukari cha aina ya pili wana nufaika kutokana na kunywa maziwa ya soy kwa sababu yana saidia kusawasisha shinikizo la damu.

4. Inasaidia kupunguza athari za kufika kilele cha uzazi kwa wanawake.

5. Kulingana na the American Cancer Society, kunywa maziwa ya maharagwe ya soy kunaweza saidia kupunguza hatari ya saratani ya matiti kwa wanawake.

Vyanzo: Organic Facts

US National Library of Medicine 

Soma pia: Nigerian chicken pepper soup recipe

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye na kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio