Wahenga walisema kuwa kila nzuri lina mbaya lake, sukari na shubiri. Na hivyo ndivyo maisha yalivyo, sawa na mapenzi. Mapenzi haiji bila misuko suko yake, haijalishi jinsi mnavyo pendana ama wakati mlio kuwa pamoja. Hata kwa wanao anzia uhusiano wao kama marafiki wa dhati, kisha kwenda hatua nyingine ya kuwa wapenzi. Ni vigumu kukosana mara kwa mara kufuatia mambo tofauti. Ila katika kesi zilizo zidi, wachumba hujipata wakitengana na kila mtu kuenda njia tofauti. Kutengana na mchumba wako kamwe haijawahi kuwa jambo rahisi, haijalishi kama mmekuwa pamoja kwa miaka miwili ama wiki mbili.
Kutengana huleta hisia za huzuni, majonzi na chuki, hasa kama wewe ndiye unaye wachwa. Huenda ukakosa kuiamini jinsia tofauti tena na kuapa kuto penda tena. Sio rahisi pia kwa aliye fanya uamuzi wa kutoka katika uhusiano huo. Katika wakati huu, una mawazo mengi ukijiuliza ikiwa unafanya kitu sawa ama la.
Kocha wa uhusiano aliwajuza watu vidokezo 5 bora vya jinsi ya kutengana na mchumba wako kwa njia iliyo komaa.

- Kuwa wazi
Mara nyingi, watu hufanya uamuzi wa kutengana, wakati ambapo mchumba waliye naye kamwe hana mahitaji, maoni ama hatazami vitu kwa njia sawa. Kwa hivyo, kabla ya kutengana, hakikisha kuwa umeorodhesha mambo yasiyo kupendeza tena, unavyo hisi na ulicho soma kwenye uhusiano huo ili uwe wazi kwa mchumba wako mnapo tengana.
2. Hakikisha kuwa akili yako haihisi mapenzi tena

Ikiwa unajaribu kutengana na mtu lakini kila mara unajipata ukikumbuka mambo yaliyo kuvutia kwake, ama mambo ya kufurahisha mliyo fanya pamoja. Hii ni kawaida, lakini ili mtengane, lazima hisia zako zianze kwenye akili yako na sio kwenye mtima wako. Angazia mambo yaliyo kufanya ufanye uamuzi wa kumtenga. Kisha ubaki ukirudia hayo.
3. Kuwa mwenye heshima, ila zingatia mipaka
Kutengana bila shaka kuna umiza na kuwacha hisia za chuki, kwa wachumba wote wawili. Kuwa na heshima hata unapo anza kujitenga na mpenzi wako, ila zingatia mipaka unayo tengeneza kwa sababu usipokuwa wazi, huenda ukajipata umerudi kwa uhusiano unaojaribu kutoka
4. Tahini thamini yao
Ikiwa umemthamini mpenzi wako kwa muda mrefu, unaweza tenga wakati spesheli wa kuwa na mazungumzo haya naye. Ikiwa hauwa thamini sana, unaweza watumia ujumbe mfupi wa kutengana nao. Huu utakuwa uamuzi wako.
Hitimisho
Kwa kufanya haya, utahakikisha kuwa, hakuna aliye baki na hisia za chuki kwa mwingine, kutumia maneno makali ama matusi. Na huenda hata mkazidi kuwa marafiki baada ya hapo. Fikiria kuhusu mambo ambayo ungependa kufanya baada ya kutengana, kisha uanzie maisha yako mapya.
Soma Pia: Jinsi Ya Kujua Iwapo Atakua Mwanamme Bora Katika Ndoa: Sifa Za Mwanamme Mwema