Dessert Ya Zobo Popsicles Ambayo Watoto Wako Watapenda

Dessert Ya Zobo Popsicles Ambayo Watoto Wako Watapenda

Hapo awali desserts nyingi zilikuwa na matayarisho ya keki, tarts, puddings na krimu. Ila, shukrani kwa wapishi wataalum kutoka nchi ya Nigeria, hadithi hii imebadilika. Hiari za desserts zime ongezeka na zina desserts nyingi za mapishi kutoka matunda na vyakula nchini. Matokeo ni mapishi yaliyo na vyakula asili, mawazo geni na ubunifu, kama dessert ya zobo popsicles. Iwapo wewe ama watoto wako wanapenda vitu vitamu, hiki ni kitu mtakacho penda na kufurahia.

Je, ungependa kujua jinsi ya kutengeneza dessert hii ya Nigeria? Tunakusaidia kwa kukuelimisha jinsi ya kutengeneza dessert ya zobo popsicle hapa chini.

Lakini kwanza, tuangalie historia kuhusu zobo.

Nigerian dessert zobo popsicle

Zobo kwa lugha ya Hausa ina maana ya Caribbean Sorrel, sehemu zinazo lika za mmea wa Hibiscus zinazo julikana kama Roselle. Mmea wa Hibiscus una dhamana ya virutubisho na kiwango kikubwa cha vitamini C inayo saidia kuponya homa, kukohoa, joto jingi na maambukizi. Cha zaidi ni kuwa ina anti oxidants na asilimia 15-30 za asidi asili zinazo saidia kuepusha saratani kwa sababu zina upa mfumo wa kinga nguvu zaidi. Hii ndiyo inayo fanya kinywaji cha hibiscus kiwe maarufu zaidi, na sio sehemu za Nigeria Kaskazini mbali Afrika nzima. Hata akama desserts za Nigeria sio maarufu sana, wapishi wengi wana kuwa wabunifu zaidi kuhusu vyakula asili. Familia yako itafurahia dessert ya zobo popsicles baada ya kuwa nyumbani wakati mrefu ama mnapo enda mahali kutulia.

Pia, inaaminika kuwa kinywaji hiki cha zobo ni bora wakati wa hedhi ili kufanya kipindi chako kisiwe kichungu sana kwa mwanamke.

Zobo Popsicles ni tamu sana na ni dessert bora

Matayarisho

Wakati wa matayarisho dakika 20

Wakati wa kupika masaa 13

Wakati jumla unao tumika masaa 13 dakika 20

Viungo

 • 1½ kikombe cha matawi ya Zobo
 • 3 vikombe vya maji
 • 2 vikombe vya sukari
 • 1kijiko cha vanilla
 • 1 kijiko cha sharubati ya ndimu (sio lazima)
 • Maji ya machungwa
 • Kiwi ama nanasi iliyo katwa
 • Rum(sio lazima)

 Maagizo

 1. Weka maji kwa sufuria hadi yachemke, kisha uoshe na uongeze matawi ya Zobo kwenye maji hayo na uyawache kwa dakika 30 hadi lisaa limoja.
 2. Mwaga sharubati ya Zobo kwa kichungi na uweke sharubati hiyo kwenye chungu tena na urudishe kwa moto. Ongeza sukari na moto wa wastani; huku ukikoroga mara kwa mara, na uwache yachemke hadi viputo/ bubbles zianze kuonekane. Toa maji hayo kwenye moto na uwache yapoe; kisha uongeze vanilla na sharubati ya ndimu iwapo unaitumia na utenge kando kwa matumizi mengine.
 3. Mwaga matunda kwenye vikombe/ moulds; kisha umwage sharubati kwenye popsicle moulds. Na ufinike na uweke kwenye barafu usiku wote.
 4. Kutoa popsicles kutoka kwa molds hizo, vuta kwa urahisi na uzimwagilie maji ya vuvgu vugu; kisha uvute kidogo.

 

Chanzo: Nigerian Lazy Chef

Soma pia: Creating the perfect food time table for Nigerian homes

 

Written by

Risper Nyakio