Jinsi Ya Kutengeneza Kitamu Tamu Maarufu Zaidi Nigeria, Dodo Ikire

Jinsi Ya Kutengeneza Kitamu Tamu Maarufu Zaidi Nigeria, Dodo Ikire

Dodo Ikire ni kitamu tamu maarufu zaidi ambacho kimekuwa kikitengenezwa katika sehemu tofauti Nigeria.

Je, unafanya nini na ndizi zilizo iva kupindukia? Unazitupa kwa taka taka ama una tengeneza kitu kilicho na ladha kutoka kwa ndizi hizi? Kitu kama dodo ikire? Kitamu tamu hiki ni kizuri cha kukula nyumbani unapo tizama sinema. Iwapo unapenda kula mara kwa mara kama wanawake walio na mimba wanavyo penda, lazima uwe na Dodo Ikire. Katika makala haya, tuna angazia jinsi ya kutengeneza dodo ikire. Unapenda kitamu tamu hiki? Haditho yako ni ipi?

Chanzo Cha Dodo Ikire

Dodo Ikire ni chakula cha  kitamaduni kutoka kwa Ikire, mtaa mmoja ulioko katika sehemu ya Kaskazini Magharibi mwa Nigeria. Hapo awali ilitengenezwa kutoka kwa ndizi zilizo baki ila sasa hivi hutengenezwa kutoka kwa viungo freshi. Kulingana na hadithi, kitamu tamu hiki kilitengenezwa na mwanamke mmoja mzee maskini kutoka kwa mtaa wa Ikire. Ikire ni mtaa katika sehemu ya Kusini Magharibi mwa Nigeria kati ya miji ya Ibadan na Ile-Ife katika Osun state.

Mwanamke huyu mzee hakuwa na chakula mbali na mabaki ya ndizi zilizo iva zaidi ambazo angetupa kwa takataka. Ila alifanya uamuzi wa kuzi bonda pamoja na chumvi na pilipili na kuzikaanga kwa kutumia mafuta ya nazi. Alikula na kufurahia na kuamua kuwa gawia majirani wake.

Matokeo sasa yanajulikana kama Dodo Ikire, iliyo itwa baada ya mahali ilipo tengenezwa mara ya kwanza. Ina uzwa kwa sana sehemu za Kusini Magharibi mwa Nigeria.

Jinsi ya kutengeneneza Dodo Ikire

 

dodo ikire

Shukrani kwa: Dooney

Kutengeneza Dodo Ikire ni wazo bora ya chakula cha kutengeneza unapokuwa na ndizi zilizo iva zaidi na pia una wakati tosha mikononi mwako. Ni rahisi sana kutengeneza, ina ladha na pia ina kukumbusha mengi ya siku zako za udogoni.

Maagizo haya ya kutayarisha chakula hiki yana tosha watu 9 (ama kama ungependa kula kama kitamu tamu.

Viungo

 • 3 ndizi zilizo na ngozi nyeusi
 • 3 vijiko vya poda ya pilipili
 • Chumvi iwe na ladha
 • Mafuta (1/3 mafuta ya nazi na 2/3 mafuta ya kupika) ya kukaanga

Maagizo

 1. Kata ndizi na uchanganye na pilipili na chumvi na uzitengeneze ziwe mipira midogo.
 2. Pasha mafuta joto hadi iwe moto lakini isianze kutoa moshi.
 3. Lainisha mipira ile kidoggo na uiweke kwenye mafuta yale yaliyo moto.
 4. Punguza moto na ukaange mipira ile ya ndizi hadi iwe na rangi ya hudhurungi.
 5. Tumia kijiko kilicho na mashimo kutoa ndizi zile motoni kisha utumie tishu za jikoni kukausha mafuta yake.
 6. Ili kuwa na ladha yake asili ama unyevu wake wa kawaida, funga mipira ile ya ndizi vizuri kwenye begi ya plastiki na uwache ipoe. AMA
 7. Hiki ni kitamu tamu kizuri unapokuwa na wageni na ungependa kuwa mwenyeji bora zaidi, hii ni chaguo bora zaidi. Jaribu na uone kuwa wageni wako wata furahia na kukupenda zaidi.

Haijalishi iwapo una jino linalo penda vitu vitamu na unatafuta kitamu tamu chenye ladha ama unashangaa jinsi ya kuhifadhi ndizi zako zilizo iva zaidi, chakula hiki kitakufaa.

Kumbukumbu:

Wikipedia

Guardian Life

Soma pia: A simple ikokore recipe

Written by

Risper Nyakio