Wanao penda mikate wana ipande kiasi kuwa wanaweza kula mkate kama kiamsha kinywa, chamcha na chajio iwapo wataruhusiwa. Mkate wa Nigeria ni mojawapo ya vitu vya kupendeza zaidi ambazo unaweza fanya na mkate ukiwa jikoni na uishie kuwa na kitu chenye ladha, kitamu na kilicho rahisi kutengeneza. Kwa kutumia sandwich maker, grill pan ama kaangio, mkate wako wa toast utakuwa tayari kwa muda chini ya dakika 10. Fahamu jinsi ya kutengeneza mkate wa toast wa Nigeria.
Jinsi Ya Kutengeneza Mkate Wa Toast Wa Nigeria

Viungo vingine huchanganyika vyema na mkate na ndiyo sababu kwa nini ni vigumu kukataa mkate wa toast. viungo hivyo vingine huleta virutubisho zaidi kwa mchanganyiko ambao huenda mkate huo unakosa. Kutengeneza usawa ulio na ladha na afya nzuri zaidi. Mkate wa toast hufanya kazi vizuri zaidi ukitumika kama kiamsha kinywa na pia ili kukupa hamu ya kula.
Mkate wa toast wa Nigeria na toaster
Picha: Unsplash
Viungo
- 4 vipande vya mkate
- 1 yai
- 2 Sardines
- Lettuce
- Siagi
Maandalizi kwa kutumia toaster
- Pasha joto toaster yako hadi mwangaza uzime.
- Paka vipande vya mkate siagi kwenye pande moja.
- Piga mayai kwenye bakula kisha utumbukize vipande vya mkate kwenye mayai haya.
- Weka upande wa chini wa mkate kwenye griddle na ukate sardines, lettuce na viungo vingine vya maharagwe, cheese ama mayai yaliyo chemshwa. Kisha ufunikie na kipande cha pili cha mkate. Una shauriwa kupanga unapo weka kwenye toaster.
- Funika kifuniko cha toaster na uwache ipikike vyema. Inafanyika wakati ambapo mkate unageuka na kuwa hudhurungi. Kisha mkate wako wa toast utakuwa tayari.
Mkate wa toast wa Nigeria kwa kutumia kikaangio

Viungo
- 6 vipande vya mkate
- 2 mayai
- 100ml maziwa
- 2 vijiko vya sukari
- 1 kijiko cha siagi ya kukaanga
- Sukari, asali, jam ya kupakua
Maagizo
- Piga mayai kwenye bakuli hadi iwe laini kabisa. Piga na uchanganye tena huku ukiongeza maziwa na suari ili kuyakubalisha yachanganyike.
- Ongeza siagi kwenye pan ama kikaangio na ungoje yayeyuke. Kisha tumbukiza vipande hivi vya mkate kwenye siagi ya mayai moja baada ya nyingine kwa angalau sekunde 10 hadi 20 kwa kila pande.
- Kaanga vipande hivi kila upande hadi vigeuke viwe rangi ya hudhurungi. Ongeza siagi zaidi kwenye kaangio ya kukaanga iwapo ita kauka.
- Rembesha na sukari, asali ama kitu kingine utakacho amua.
Patia toast hii hata ladha zaidi, unaweza ongeza vanilla extract na nutmeg iliyo siagwa kwenye siagi ya mayai.
Soma pia: The Fluffiest Pancake Recipe You Ever Saw
Vyanzo: Nigerian Diet
Makala haya yali andikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.