Jinsi Ya Kutengeneza Poda Ya Soya Beans: Hatua Kwa Hatua

Jinsi Ya Kutengeneza Poda Ya Soya Beans: Hatua Kwa Hatua

Maziwa ya soy yana faida nyingi za kiafya! Iwapo unapendelea maziwa ya soy yaliyo tengenezewa nyumbani, makala haya yana vidokezo vya jinsi ya kutengeneza poda ya soya beans.

jinsi ya kutengeneza poda ya soya beans

soy milk ina ladha na virutubisho vingi!

Jinsi ya kutengeneza poda ya soya beans

Viungo
 • 2 vikombe vya soya beans
 • 10 vikombe maji
 • 1 ndizi mbichi
 • ½ njugu zilizo kaangwa
 • Asali, sukari
 • 3 vijiko vya  ground crayfish (kwa hiari yako)
Mbinu – jinsi ya kutayarisha poda ya soya beans

soya beans powder

Hatua 1 – Kuosha na kutayarisha soya beans

  Chagua soya beans kwenye bakuli na utupe uchafu, mchanga ama zilizo haribika

Utachagua soya beans zako njia sawa unavyo chagua maharagwe ya kawaida. Hii inahakikisha kuwa hazina uchafu na kufanya mchakato wa kusiaga kuwa rahisi zaidi. Kujifunza jinsi ya kutengeneza poda ya soya beans itaanza kutoka hatua ya kwanza ya usafi wa maharagwe yako.

Osha soya beans kisha uziwache zikauke usiku

Maharagwe yana paswa kuwa yamekauka kabla ya kusiaga. Yakikosa itakuwa vigumu kupata poda laini. Huenda poda yako ikatoka ikiwa na chembechembe iwapo bado kuna maji kwenye maharagwe yako. Katika hatua hii, angalia iwapo kuna uchafu ama mawe.

Kwenye sufuria, kaanga soya beans hadi zi kauke kidogo na ziwe na rangi ya hudhurungi na maganda yana toka kwa urahisi

Unapo kaanga soya beans, unapaswa kuzichanganya mara kwa mara huku ukitumia moto wa chini ili zisichomeke. Unakaanga kama vile njugu.

Siaga soya beans zingali moto

Utapata poda laini ukizisiaga punde tu baada ya kuzitoa kwenye moto. Baada ya kupoa, huenda zika shikana na kufanya poda yako iwe imeshikana badala ya kuwa laini. Unashauriwa kukaanga maharagwe baada ya kutayarisha viungo vingine vinavyo hitajika.

Jinsi Ya Kutengeneza Poda Ya Soya Beans: Hatua Kwa Hatua

Maendelezo ya jinsi ya kutengeneza poda ya soya beans.

Hatua 2 – kutayarisha mandizi mbichi
 • Osha kisha utoe maganda ya ndizi ile mbichi
 • Kata ndizi yako iwe vipande vidogo na uiwache kwenye jua ikauke
 • Kama sio hivyo, iwapo hakuna jua tosha ya kukausha, unaweza kausha ndizi yako kwenye oven
 • Ama pia unaweza ruka hatua yote ya kukausha iwapo utanunua vibanzi vya ndizi vilivyo tayari kutoka sokoni na uvikaushe
Hatua 3 – Kutayarisha njugu
 • Kaanga njugu zako kwenye sufuria hadi ziwe na rangi ya hudhurungi kisha uziweke zipoe.
 • Toa maganda ya njugu ili kuzitenganisha na maganda
Hatua 4 – kusiaga viungo vyote
 • Weka viungo vyote kwenye kifaa cha kusiaga kisha usiage vyema
 • Hifadhi poda hiyo kwenye kontena ambayo haipitishi hewa

Maziwa ya soy yana ladha na virutubisho. Iwapo una hisi kujaribu vitu vipya baada ya kujifunza jinsi ya kutengeneza poda ya soya beans, unaweza ongeza ladha ya vanilla, mint ama ya kahawa. Iwapo unawalisha watoto wako maziwa ya soya, unaweza ongeza crayfish kuongeza idadi ya virutubisho.

Umuhimu wa maziwa ya soy

Iwapo ungependa kujua jinsi ya kutayarisha poda ya soya, unajaribu kusoma jinsi ya kutengeneza maziwa ya soya ukiwa nyumbani. Maziwa ya soy yana ladha na afya, hizi ndizo sababu kwa nini unapaswa kuyaongeza kwenye lishe yako.

1. Maziwa ya soy ina vitamini na madini ambayo ni nzuri kwa mwili wako

2. Kunywa maziwa ya soya beans kunaweza saidia kupunguza cholesterol mbaya na kuimarisha afya yako ya moyo

3. Watu wanao tatizika kutokana na Type 2 diabetes wana faidika kutokana na kunywa maziwa ya soy kwa sababu ina rekebisha shinikizo la damu

4. Inasaidia kupunguza athari za kufikisha umri wa kuto zaa kwenye wanawake.

5. Kulingana na American Cancer Society, kunywa maziwa ya soya beans kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya saratani ya matiti kwenye wanawake.

Kumbukumbu: Organic Facts

US National Library of Medicine 

Soma pia: Nigerian chicken pepper soup recipe

Written by

Risper Nyakio