Jinsi Ya Kutengeneza Pornstar Martini

Jinsi Ya Kutengeneza Pornstar Martini

Mwongozo huu unakusaidia kujua jinsi ya kutengeneza kinywaji kitamu cha pornstar martini. Bila shaka utakifurahia!

Kinywaji hiki cha pornstar martini ni kitamu na ni kizuri cha mikutano ya jioni ama usiku na mpenzi ama marafiki zako. Matunda matamu ya vanilla na passion huchanganywa na kutengeneza kitu kitamu. Tuna kufunza jinsi ya kutengeneza pornstar martini ya kupendeza. Kwanza, tuna angazia historia ya martini. Je, ulifahamu kuwa hiki ni kinywaji anacho kipenda zaidi James Bond? Tuangazie zaidi.

Historia Kuhusu Kinywaji Cha Martini

pornstar martini

Historia ya martini inaweza anzishwa katika karne ya 19. Hiyo ndiyo mara ya kwanza ilipo orodheshwa kwenye vinywaji vinavyo uzwa kwenye vilabu. Na kujulikana katika mwaka wa 1887 kufuatia vinywaji vya Jerry Thomas. Alikuwa maarufu katika kutengeneza vinywaji kwa vilabu na alifanya kazi katika hoteli ya Occidental huko San Francisco. Ila, baadhi ya watu hawakubaliani na hili.

Mji wa Martinez umekana jambo hili sana. Mji huo una amini kuwa kinywaji hiki kili julikana kwa mara ya kwanza kwenye kilabu maarufu Martinez, ambako kilijulikana kama 'Martinez Special." Huko mchimbaji maarufu alipatiwa kinywaji hiki akielekea Sana Francisco. Baada ya kufurahia kinywaji hiki sana, mchimbaji huwa wa dhahabu alipatiana matayarisho huko San Francisco ambapo alimfunza mtu wa kutengeneza vinywaji kwenye klabu. Swali hili limepelekwa kortini kati ya miji hii miwili na bado tuna subiri maamuzi. Tuendelee kuangazia jinsi ya kutayarisha kinywaji hiki.

Jinsi Ya Kutengeneza Pornstar Martini

Jinsi Ya Kutengeneza Pornstar Martini

Kinywaji hiki cha Pornstar Martini ni mojawapo ya vinywaji maarufu zaidi huko Umarekani. Mtengenezaji vinywaji Douglas Ankrah alitengeneza kinywaji hiki katika kilabu cha Knightsbridge. Yeye pia ndiye mwanzilishaji wa LAB (London Academy of Bartending).

Mara ya kwanza aliita kinywaji hiki Maverick Martini, kama njia ya shukrani ya klabu kidogo huko Cape Town. Ila baadaye alibadilisha jina na kukiita Porn Star Martini. Alisema aliipa jina hili kwa sababu aliiona kama ni kinywaji ambacho porn star ange kunywa. Alisema ni kinywaji cha raha, starehe na kujifurahisha.

Ila haya ni maagizo ya kuibua, asili yana tumia 50mL Vanilla Vodka, 20mL Passion Fruit Liqueur, 50mL Passion Fruit Puree na vijiko viwili vya sukari ya vanilla ya kutengenezewa nyumbani.

Utaratibu wa Kutengeneza Pornstar Martini

Viungo

  • 60mL Vodka
  • 30mL matunda ya Passion
  • 30mL Vanilla Syrup
  • 15mL sharubati ya limau iliyo freshi
  • Prosecco ama Champagne

Maagizo

  1. Changanya vitu hivi vyote mbali na divai ya sparkling kwenye chombo chako cha kuchanganya
  2. Changanya ama tingisha na barafu
  3. Chuja na uweke kwenye glasi
  4. Rembesha kwa kutumia matunda ya passion (mwagilia sukari ya vanilla, ila sio lazima)
  5. Weka kwa glasi ndogo ya Champagne
Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio