Sababu Kwa Nini Kutibu Viini Kwa Watoto Huenda Kukakutatiza

Sababu Kwa Nini Kutibu Viini Kwa Watoto Huenda Kukakutatiza

Iwapo ungependa kujua jinsi ya kuwatibu watoto wako wanapo ugua kutokana na viini, makala haya yatakusaidia kupata maarifa zaidi.

Bi Owokoniran alikuwa na fikira nyingi akilini. Mtoto wake wa kiume Dapo alipata viini tena. Alikuwa amemtibu threadworms mwezi uliopita, na miezi mitatu kabla ya hapo. Alikuwa amenyunyiza dawa kwa nyumba na kuosha sakafu kwa kutumia sabuni na kuosha vitu vyote. Vidoli vyake pia havikuachwa nyuma. Alikuwa amesafisha kila kitu kwa nyumba hiyo. Kwa nini mtoto wangu ana pata viini kila mwezi? Alijiuliza, hadi akafanya uamuzi wa kumwuliza rafiki yake bi Aliyu jinsi ya kutibu viini kwa watoto.

Jinsi ya kutibu viini kwa watoto: Kwa nini mtoto wako anaugua viini wakati wote

kutibu viini kwa watoto

Wanawake hawa wawili walikaa chumbani wakijadili jambo hili. Na wakafanya uamuzi wa kupatana kila Alhamisi ili kujuzana yanayo wakumba kwa maisha yao kama mama na bibi. Walikuwa wamepatana mwaka mmoja uliopita kwenye mikutano ya shule. Watoto wao wote walikuwa wanasomea shule na darasa moja.

"Je, Aminu ashawahi kuugua viini?"

"Naam, kwa bahati nzuri, siku hizo zimepita. Kwa wakati huo, ilionekana kana kwamba haingewahi isha."

"Oh! Viliishi kumpata mara kwa mara pia?" Bi Owokoniran alikuwa na furaha sasa. "Jambo sawa linamfanyikia Dapo. Hii ni mara ya tatu anaugua viini kwa kipindi cha miezi mitano," alimwambia rafiki yake. "Kumtibu sio tatizo. Sielewi kwa nini haviishi."

"Una uhakika uli vitibu mara ya kwanza?" Bi Aliyu alimwuliza rafiki yake. Alijua jinsi jambo hili lina weza mkwaza mzazi. "Wacha nikujulishe kitu ambacho daktari dadangu alicho niambia."

"Viini ama threadworms hutaga mayai karibu na upande wa nyuma wa mtu aliye ambukizwa, hasa usiku. Pamoja na mayai, viini hivi hutoa kamasi inayo sababisha kujikuna.

Sababu Kwa Nini Kutibu Viini Kwa Watoto Huenda Kukakutatiza

Iwapo mayai haya hubaki kwenye kucha za mtu anapo jikuna, yana weza pelekwa hadi kwa mdomo, vitu vingine ama hata nguo. Iwapo watu walio karibu wameshika vitu hivyo, wanaweza pia kuyapeleka mayai hayo kwenye midomo yao. Mtu anapo ambukizwa, nyumba yote inapaswa kupata matibabu.

Mayai haya yana uwezo wa kuishi kadi wiki mbili kabla ya kutaga. Iwapo mayai haya yana taga karibu na sehemu ya nyuma, viini hivi vipya huingia tumboni. Mayai yaliyo mezwa yana weza taga mwilini. Baada ya wiki 2, viini hivi hukomaa na kuanza kutaga tena.

Kwa hivyo iwapo una uhakika nyumba ni safi, na je shuleni? Kwa sababu ana ambukizwa kutoka mahali pengine. Kwa hivyo kama sio nyumbani, basi ni shuleni."

"Hmmm", alisema Bi. Owokoniran. "Huenda basi ikawa hiyo ndiyo sababu kwa nini ni vigumu sana kupambana na tatizo hili. Nafahamu tatizo ni lipi sasa. Hata kama tuna safisha nyumba vizuri, tuna tibu Dapo peke yake. Wakati ninapo mfanya anawe mikono na kuzingatia usafi, siko makini na dadake. Na wanacheza pamoja. Hakuna njia ya kujua iwapo mikono yake kwa bahati mbaya imepata viini hivi."

Bi. Aliyu alitabasamu huku akikubaliana naye. "Pia, unapaswa kuongea na mwalimu wake kuhusu jambo hilo. Iwapo mwanafunzi ana sambaza maambukizi, wanapaswa kujulishwa kuhusu jambo hilo."

Kutibu viini vya threadworms

Sababu Kwa Nini Kutibu Viini Kwa Watoto Huenda Kukakutatiza

Ili kufanikiwa kutibu viini, wanafamilia wote wanapaswa kutibiwa, hata kama hawana ishara za viini hivi. Hii ni kwa sababu ya hatari ya kusambaa kwa virusi hivi iko juu sana.

Jukumu la tiba hii ni kutibu viini na kuepuka kusambaa kwake. Hii mara nyingi inahusisha matibabu tofauti kuua viini na kuzingatia usafi wakati wote kuepuka kusambaa kwa mayai.

Matibabu makuu yanayo tumika kutibu viini hivi yana patikana kutoka kwa zahanati karibu nawe hata bila ya ushauri wa daktari. Walakini, ni muhimu kufuata maagizo yaliyoko kwenye kijisanduku cha dawa kwani sio nzuri kwa kila mtu.

Unahitaji kumwona daktari wako iwapo:

 • Una viini vya threadworms na una mimba na una nyonyesha
 • Mtoto wako ana viini hivi na ana umri chini ya miaka miwili

Hii ni kwa sababu matibabu yanayo shauriwa kwa visa hivi wakati mwingi sio sawa na yanayo shauriwa kwa watu wengi.

Hatua za usafi

Sababu Kwa Nini Kutibu Viini Kwa Watoto Huenda Kukakutatiza

Maisha ya viini hivi huwa muda wa wiki sita, kwa hivyo ni muhimu kuchukua hatua za usafi kwa muda huu wote. Kila mtu kwenye nyumba hiyo anapaswa kufuata ushauri tunao angazia hapa chini.

 • Fua nguo zote za usiku, za kitanda, taulo, vitambaa na vidoli laini unapo gunduliwa kuwa na viini hivi. Fanya hivi kwa joto ya kawaida, ila hakikisha kuwa una suuza vyema baada ya kufua
 • Repeat this regularly. Osha nyumba yote na kila kitu kwenye nyumba hasa vyumba vya kulala
 • Kwa utaratibu, safisha bafu na jikoni, na vyombo vyote vilivyoko kwenye vyumba hivyo na kuosha vitambaa vya jikoni kwa maji moto mara kwa mara
 • Epuka kugusa gusa vitu vilivyo chafuka kama vile vitambaa vya kitanda na nguo. Hautaki kushika viini ambavyo huenda vikawa kwenye nguo hizo
 • Usikulie chakula chumbani cha kulala, huenda ukameza mayai ya viini hivyo yaliyo toka kwenye nguo hizo
 • Hakikisha kuwa kucha zako ni fupi wakati wote - wahimize wanfamilia wengine kufuata nyayo zako
 • Wakanye kula kucha za vidole ama kunyonya vidole- hasa, hakikisha kuwa watoto hawa nyonyi vidole vyao vya gumba
 • Osha mikono yako mara kwa mara na usugue chini ya kucha zako. Ni muhimu kufanya hivi kabla ya kula na baada ya kutoka msalani na kabla ya kumbadili mtoto nepi
 • Oga mara kwa mara

Watoto wanaweza okota viini vya threadworms kwa urahisi kutoka kwa marafiki zao ama hata shuleni, kwa hivyo zingatia usafi ili kutibu viini kwa watoto na kuepuka kupata maambukizi haya tena.

Chanzo: NHS

Soma pia: Ratiba Ya Chanjo Kenya : Mwongozo Kwa Wazazi

Written by

Risper Nyakio