Kipimo cha mimba cha kinyumbani kinatumika kudhibitisha iwapo mwanamke ana ujauzito ama la. Wanandoa wanaolenga kuwa wazazi huenda wakawa na hamu ya kupima mimba kufahamu hali yao. Tunazingatia jinsi ya kutumia kipimo cha mimba kwa njia sahihi ili kupata matokeo bora.
Vipimo vya mimba vya kinyumbani ni rahisi kutumia na kusoma matokeo. Ili kupata matokeo sahihi, wanandoa wanapaswa kuzingatia matumizi kama ilivyoonyeshwa kwenye kijisanduku chake.
Jinsi ya kutumia kipimo cha mimba

Kipimo cha mimba hufanya kazi kwa kugundua uwepo wa homoni ya mimba (hCG). Homoni hii inatolewa mwilini yai linapojipandikiza kwenye fuko la uzazi. ili kupata matokeo sahihi ya kipimo cha mimba, angazia mambo haya:
1. Nunua kipimo. Wataalum wanashauri kununua kipimo cha mimba kutoka duka kubwa linalokuwa na wateja wengi kwa siku. Kwa njia hii, una uhakika unanua kipimo kipya ambacho hakijakaa kwenye duka kwa muda mrefu.
2. Angalia tarehe ya kuharibika kwake. Kila kifaa huwa na tarehe ya utumizi, baada ya tarehe hii, kifaa hiki huwa kimeharibika na hakuna uhakika kuwa utapata matokeo sahihi baada ya tarehe hii. Hakikisha kuwa kipima mimba unachokinunua hakijapitisha wakati wa matumizi.
3. Soma na ufuate maagizo ifaavyo. Ndani ya kijisanduku cha kipimo cha mimba, kuna kijikaratasi chenye maagizo ya kutumia kipima mimba kile.
4. Kusanya vifaa hitajika. Mbali na kipima mimba, utahitaji kontena safi na saa.
Kufanya kipimo cha mimba

Wakati bora wa kufanya kipimo cha mimba ni asubuhi. Muda tu baada ya kuamka kabla ya kutia chochote kinywani. Katika wakati huu, mkojo huwa umekolea na ni rahisi kugundua iwapo una homoni ya mimba.
1.Nawa mikono kwa kutumia sabuni na maji vuguvugu.
2. Toa kipima mimba kutoka kwa karatasi iliyokifunganisha
3. Enda msalani kisha uweke kiasi cha mkojo kwenye kontena ile
4. Kisha, weka kipima mimba kwenye kontena ile, kuangalia kwa umakini upande unaopaswa kuweka.
5. Ngoja dakika zilizoshauriwa kwenye maagizo ya matumizi.
Baada ya muda unaofaa kuisha, angalia matokeo ya kipima mimba.
Kusoma matokeo
Kulingana na aina ya kipima mimba chako, huenda kikaonyesha mistari miwili, mstari wa pinki, alama ya + ama neno 'pregnant' ikiwa una mimba. Ikiwa huna mimba, itakuwa mstari mmoja ama neno 'not pregnant'.
Soma Pia: Matokeo 7 Mwanamke Anayoshuhudia Baada Ya Kutoa Mimba