Kondomu hutumika wakati wa ngono kutengeneza kizuizi kinachozuia manii kuingia kwenye uke.
Kondomu zinasaidia kulinda dhidi ya kupata maambukizi ya magonjwa ya kingono na ujauzito. Ni njia nzuri ya kupanga uzazi kwani kondomu ni rahisi kupata, za bei nafuu na zinapatikana mahali popote.
Ufanisi wa utumizi wa kondomu ya kiume
Ufanisi wa kondomu hulingana na iwapo ilitumika kwa njia inayofaa.
Kondomu za kiume zinapotumika kwa njia inayofaa, kondomu huwa na asilimia 98 ya kulinda dhidi ya magonjwa ya kingono na ujauzito. Kondomu za kike huwa na ufanisi wa asilimia 95.
Aina za kondomu

- Latex. Watu wengi hutumia aina hii ya kondomu. Ila, kuna watu wanaokuwa na mzio wa latex. Watu hawa wanashauriwa kutumia kondomu za plastiki.
- Zilizo lubricated. Lube na lubrication kwenye kodomu husaidia kulinda dhidi ya kuhisi uchungu ama kutokuwa na starehe wakati wa ngono.
- Zenye spermicide. Kemikali inayofahamika kama nonoxynol-9 inayoua manii. Hata ingawa kemikali hii inaua manii na kupunguza nafasi za kushika mimba, genitalia za mwanamke hukosa starehe. Huenda akahisi kujikuna kwenye uke baadaye.
Jinsi ya kutumia kondomu za kiume
1.Hakikisha kuwa kondomu iko katika hali nzuri na haijapita wakati wa kutumika kwake
2. Fungua kutoka kwa kijikaratasi chake kwa umakini
3. Wekelea kwenye ncha ya uume uliosimama, kisha uingize kwenye uume
4. Wacha nafasi ya inchi nusu kwenye ncha ya uume ambapo manii yatamwagika. Inasaidia kondomu isivunjike
5. Baada ya ngono itoe kwa umakini kabla ya uume kuwa laini. Kwa kuhakikisha kuwa haumwagii mchumba wako manii.
6. Funga kondomu hiyo na tishu kisha uitupe kwenye pipa la taka.
Vidokezo vya utumizi wa kondomu

- Tumia kondomu ambayo haijapita muda wake wa matumizi
- Tumia kondomu mpya katika kila kitendo cha ngono
- Hakikisha kuwa haurarui kondomu unapoitoa kwenye kijikaratasi chake
- Valia kondomu kabla ya kumwingia mchumba wako
- Usitoe kondomu kabla ya kitendo cha ngono kutamatika
- Ifunge vizuri na uitupe kwenye pipa baada ya kitendo cha ngono
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kuboresha Ubora Na Idadi Ya Manii Ili Kudumisha Uzalishaji Katika Wanaume!