Mitandao ya kijamii- jinsi ya kuitumia. Siku hizi, tumezoea mitandao ya kijamii sana kama vyombo vya mawasiliano vinavyo tusaidia kuwajulisha watu kinachofanyika maishani mwetu, kujua jinsi wengine wanavyo endelea na kuungana tena na marafiki wetu wa hapo awali. Je, utumizi wa mitandao ya kijamii inaweza kuathiri ndoa zetu kivipi? Inalingana na jinsi ambavyo mitandao hii inavyo tumika. Tazama vidokezo muhimu vya jinsi ya kutumia mitandao kwa wanandoa.
Jinsi ya kutumia mitandao kwa wanandoa

- Kuwa na mipaka
Sote tunafahamu jinsi ambavyo wakati hupita kwa kasi tunapo anza kutumia mitandao kama Facebook ama Instagram. Tukichambua kurasa baada ya nyingine kuangalia kinacho tendeka na habari za hivi punde. Wengine wetu huenda wakawa na hatia ya kutumia muda zaidi kwenye mitandao ikilinganishwa na tunavyo zungumza na wachumba wetu. Huenda tukachukua muda zaidi kutuma jumbe kuhusu chakula chetu kwenye mitandao badala ya kuzungumza na wachumba wetu. Tusipokuwa makini, kuwasiliana na dunia huenda ikachukua kipau mbele ikilinganishwa na kuzungumza na wachumba wetu.
Fikiria kuhusu kuweka mipaka kwenye wakati unaotumia katika mitandao ya kijamii. Kwa mfano, nusu saa kila siku ama unapo zuru peke yako. Wanandoa wanapaswa kujadiliana kuhusu matarajio yao kuhusu mitandao ya kijamii. Mawasiliano yanayo fanyika kwenye mitandao ya kijamii hasa na jinsia tofauti. Pia mambo msiyopaswa kuweka kwenye mitandao ya kijamii.
2. Kuwa wazi
Kuwa na uwazi ni muhimu katika ndoa zote, ambapo wanandoa hawafichi kitu chochote. Hata inapofika kwa mitandao ya kijamii. Mkubalishe mchumba wako aweze kuona mitandao yako ya kijamii na unachokifanya. Hata kumpa neno lako la siri.

3. Kuwa na heshima
Ikiwa umemkasirikia mchumba wako, mitandao ya kijamii sio mahali pa kumtolea mchumba wako hasira zako. Sharti moja ni kuwa, haupaswi kuweka ujumbe wowote kwenye mitandao ya kijamii ambayo hauwezi pendelea ukiwekwa kwenye kurasa ya kwanza ya gazetti. Badala yake, kuwa na jumbe chanya kwenye mitandao. Unapokuwa na tatizo lolote na mchumba wako, litatue mbali na mitandao. Epuka kuweka picha ambazo mchumba wako hapendelei kwenye mitandao.
Mitandao ya kijamii ni vyombo ambavyo vinaweza kutumika kuboresha mahusiano yetu na wachumba wetu na watu wengine, tunapofuata vidokezo tulivyo angazia.
Iwapo una mawazo zaidi kuhusu njia bora za kutumia mitandao ya kijamii, tujulishe kwa kuwacha ujumbe mdogo hapa!
Chanzo: family.org
Soma Pia: Kumchukia Bwana Baada Ya Kujifungua: Vyanzo Na Suluhu La Jambo Hili