Je, Kipima Mimba Kina Fanya Kazi Vipi? Jinsi Ya Kutumia Pregnancy Strip

Je, Kipima Mimba Kina Fanya Kazi Vipi? Jinsi Ya Kutumia Pregnancy Strip

Matokeo chanya ya mimba ni ashirio kuwa mkojo wako una kiwango tosha cha kichocheo cha human chorionic gonadotropin (hCG).

Je, unafahamu jinsi ya kutumia pregnancy strip?

Maagizo ya jinsi ya kutumia pregnancy strip

jinsi ya kutumia pregnancy strip

  1. Kwa kutumia pregnancy strip, unaweza fanya kipimo cha mimba wakati wowote. Ila, kutumia mkojo wa kwanza wa siku una shauriwa. Kwani una viwango vilivyo kolea vya homoni ya mimba (hCG)
  2. Weka kiasi cha mkojo kwenye kichupa kisafi na kinacho kuruhusu kuona ndani
  3. Toa kipima mimba kutoka kwa kijikaratasi kilicho tumika kukifunganisha. Shika sehemu yenye rangi ya strip hiyo. Usiguse upande ulio na mishale ama sehemu ya katikati
  4. Kisha ukitumbukize kwenye mkojo ulio kwenye kichupa kile. Usipitishe sehemu iliyo andikwa 'MAX LINE'.
  5. Kisha utoe strip hiyo, sampuli inapo anza kufika kwenye sehemu ya jaribio. Angalau sekunde 10. Kisha uilaze strip hiyo chini, mahali pasafi na pasipo na unyevu nyevu.

Jinsi ya kubaini matokeo

kipima mimba

Laini 1= hauna mimba

Ikiwa baada ya dakika kumi strip ya mimba inaonyeshana laini moja, matokeo ya kipimo hicho ni hasi. Hauna mimba.

Laini 2= una mimba

Kipima mimba kikidhihirisha laini mbili baada ya kupima. Kipimo ni chanya na ni dhihirisho kuwa una mimba. Hata ikiwa laini ya pili ni nyepesi sana na haionekani. Una mimba, ila huenda ikawa viwango vya hCG mwilini sio vingi.

Matokeo yasiyo kubalika

Kuna wakati ambapo huenda kipima mimba kikawa na matatizo ama anaye kitumia asipo fuata maagizo, matokeo huenda yaka haribika. Usipo ona laini yoyote, matokeo yame haribika, huenda ikawa haukutumbukiza strip ile kwa muda unao faa. Itumbukize tena kwa angalau sekunde 5 kisha ungoje dakika 7 kabla ya kusoma matokeo.

Matokeo chanya ya mimba ni ashirio kuwa mkojo wako una kiwango tosha cha kichocheo cha human chorionic gonadotropin (hCG). Baada ya kupata matokeo chanya, ni vyema kuwasiliana na daktari ama kutembelea kituo cha afya karibu nawe. Ufanyiwe vipimo kisha uanze kliniki mapema iwezekanavyo. Kuanza kliniki mapema kuna ongeza nafasi za kujifungua mtoto mwenye afya na kuwa na safari nzuri ya mimba.

Hivi ndivyo jinsi ya kutumia pregnancy strip. Kumbuka kufuata maagizo yanavyo paswa ili upate matokeo sawa.

Soma pia:Je, Kupima Mimba Ni Bei Ghali Ama Rahisi?

Written by

Risper Nyakio