Vidokezo 4 Vya Kutunza Rasta Zako

Vidokezo 4 Vya Kutunza Rasta Zako

Ikiwa una shangaa jinsi ya kutunza rasta zako, makala haya yana kuelimisha kuhusu umuhimu wa moisturizer kwa rasta zako. Soma zaidi!

Vidokezo vya kutunza rasta

Sote tuna kubaliana kuwa rasta humfanya mtu aliye nazo kuonekana mwenye kusisimua na kupendeza. Hizi ni nywele zinazo shikanishwa namna sawa na kamba kwa kusukwa. Rasta zinaweza kuwa fupi, ndefu, za wastani ama zilizo na rangi tofauti. Jinsi ya kutunza rasta ni muhimu sana ili kuhakikisha zina pendeza na kukua ipasavyo.

Mtindo huu wa nywele uliibuka kutoka tamaduni tofauti na imani na una maana nyingi katika tamaduni tofauti. Hata kama rasta zina onekana kuwa rahisi kutunza, mtindo huu wa nywele unahitajia umakini mwingi, utunzi na wakati. Hapa kuna baadhi ya vidokezo kuhusu njia bora za kuweka kwa mkakati unapo tunza rasta zako:

Hakikisha zina viowevu vya kutosha

jinsi ya kutunza rasta zako

Kuna imani maarufu isiyo ya kweli kuwa rasta hazi hitaji viowevu. Ukweli ni kuwa, rasta zina hitaji viowevu vingi. Bidhaa za nywele ambazo unaweza tumia kuhakikisha kuwa nywele zako zina viowevu tosha ni kama vile beeswax, coconut oil, jojoba oil na maji.

Wakati wa usiku, funika nywele zako kwa kutumia skafu cha hariri ama bonnet ili kuepuka maji kwenye nywele kupotea. Epuka kutumia skafu za pamba ama vitambaa wakati wa kulala ambavyo vitakausha maji ya nywele yako. Ikiwa unaweza, tumia vitambaa vya hariri kitandani chako ili kuzilinda nywele zako zaidi.

Safisha rasta zako mara kwa mara

Wiki chache baada ya kutengenezwa rasta zako, zisafishe mara kwa mara. Kuepuka kichwa na nywele zenye harufu, tengeneza utaratibu wa siku ya kuziosha ili kuhudumia mahitaji ya usafi ya nywele zako. Epuka kutumia bidhaa zinazo wacha nywele yako kama imekauka.

Fanya masi za ngozi ya fuzu la kichwa

jinsi ya kutunza rasta zako

Masi ya ngozi ya fuzu la kichwa ni njia bota ya kuhimiza ukuaji wa nywele na kukupa urefu wa nywele unao tamani.

Jinsi ya kutunza rasta: Tengeneza mara kwa uhaba (re twist)

Hakuna haja ya kuitengeneza tena nywele yako mara kwa mara kwa sababu kufanya hivi husababisha nywele zako kukatika na kuharibika. Badala yake, unaweza badili mtindo wa kuishika mara kwa mara. Pia, hakikisha kuwa una paka moisturizer kwa nywele na ngozi ya fuzu la ngozi kabla ya kuzitengeneza tena ili kupunguza uharibifu.

Soma Pia:Bidhaa Asili Za Kutumia Kwenye Nywele Ya Mtoto Wako

Written by

Risper Nyakio