Shule Hii Inawafunza Wasichana Jinsi Ya Kuwa Mabibi Wazuri

Shule Hii Inawafunza Wasichana Jinsi Ya Kuwa Mabibi Wazuri

Kuna umuhimu wa kuwafunza mabinti kuwa mabibi wazuri kwa waume wao? Makala haya yana dokeza zaidi....

Sawa na kulivyo na shule za masomo rasmi, kuna shule ya mabibi Nigeria. Katika shule ya mabibi, wanawake wana funzwa jinsi ya kuwaelewa wanaume na jinsi ya kukaa katika ndoa zao. Katika mtindo wa kawaida wa shule, kuna mafunzo tofauti na wakufunzi ambao jukumu lao ni kufunza wanawake hawa jinsi ya kuwa mabibi wazuri.

Mwalimu mkuu katika shule ya mabibi, Adebola Jaiyeojo ana dokeza zaidi kuhusu shule hii ni ya nini, na kwa nini ilianzishwa.

"Shule ya mabibi imekuwepo kwa miaka 5 iliyo pita," alisema. "Na tumefanya toleo 21. Matatizo tunayo yashuhudia hasa kanisani, hata kama wana kristiano, visa vya kutengana kanisani haviaminiki. Matatizo yaliyoko huku nje haya aminiki. Ni kwa sababu wewe ni mwana kristiano hauta shuhudia matatizo? Lakini kwa kuelewa inavyo faa. Mwanamke ako katika ndoa hiyo kwa sababu ya matatizo. Na matatizo yata dhibitisha cheo chako kama mke. Na kwa hivyo matatizo sio sababu kwa nini unapaswa kutoka kwa ndoa yako. Kabiliana nayo. Mwanajeshi mzuri hakimbii kutoka vitani."

"Ni shule inayo jengwa kwa msingi wa kuelewana kwa sababu Proverbs 24 mstari wa 3 unasema una jenga kwa maarifa na inachukua kuelewana kutengeneza ulicho kijenga. Kwa hivyo utapata kuwa mafunzo ni kuhusu kuelewana: kumuelewa bwanako; kujielewa. Na kuelewa huku kuko katika viwango."

"Watu wengi huingia katika ndoa kwa sababu zisizo faa na tunaongea kuhusu hatua ya kuingia katika ndoa. Na kuangalia ndoa kutoka kwa mtazamo wa Mungu. Yeye ndiye aliye unda ndoa."

Wanafunzi wanaendelea vipi?

jinsi ya kuwa mabibi wazuri

Shule ya mabibi ime hitimisha wanawake wengi ambao ndoa zao zilikuwa katika hatari ya kuvunjika ama kuisha kabisa. Na wana sifa tu kwa athari za shule hii kwa ndoa zao. Walakini, kuna wanao shuku kama vile Omolara Sobiyi aliye enda kuwa mwelekezaji katika shule hii.

"Shule ya mabibi- nilijiuliza tunacho soma? Hii ni kuhusu nini? Kwa nini hatuna shule ya mabwana? Je, ni wanawake tu walio na jukumu la kufanya ndoa yao ifuzu wakati wote? Sobiyi aliuliza. Lakini hadithi ingebadilika alipo shuhudia shule hii ni kuhusu nini.

Aliendelea kwa kusema kuwa. "Kama singe jiunga na shule hii, ningepewa talaka ama kuwa katika ndoa yenye taabu nyingi. Ama kuishi tu bila furaha. Na ingekuwa kwa sababu ya kukosa maarifa, sio kwa sababu bwanangu ni mbaya. Kuna njia ya kufanya mambo. Kuna njia ndoa inafaa kufanya kazi. Na haya ndiyo niliyo gundua katika shule hii. Imefanikisha ndoa yangu; nimeolewa na nina furaha. Nina wakati wa uchungu? Naam. Hata baada ya shule. Lakini matatizo yanapo ibuka, sasa nina maarifa ya mambo ya kufanya. Talaka sio suluhu kwa sababu matatizo yanaweza tatuliwa.

Wanawake wengine walieleza jinsi walivyo pata kuelewa, kuhifadhi ndoa zilizo kuwa za vunjika. Wengine waligundua kuwa hawakuwa wana fanya ya kutosha kwa mabwana zao.

Je, unapaswa kujiunga na shule ya mabibi?

Shule Hii Inawafunza Wasichana Jinsi Ya Kuwa Mabibi Wazuri

Omolara Sobiyi bila shaka anafikiria kuwa unapaswa kujiunga na shule hii. "Shule ya mabibi ni mahali unapokuja kufunguliwa macho," alisema. Usipo jumuika na wengine katika shule hii, huwezi elewa kila kitu. Tuna masomo na mada tunapo funzwa jinsi ya kumuelewa bwanako, kuelewa mtu wako, kuelewa mahali pa kufanya mapenzi katika ndoa. Kitu kingine kilicho nisisimua ni kuelewa mipaka katika ndoa. Sikufahamu hilo."

"Tumekuwa na mabibi walio vunjwa moyo kuto funga ndoa kabisa. Kwa wakati walipo maliza, walifahamu shida zao zilikuwa zipi, na jinsi ya kuwa mabibi wazuri. Walijua jinsi ya kuweka mipaka yao. Na pia, walijielewa. Walielewa mahala pa ngono, ni nini hasa na umuhimu wake katika ndoa."

Soma pia:Mambo ya kuvutia ambayo wanandoa wanaweza jaribu kitandani

Written by

Risper Nyakio