Vidokezo Vya Kuwa Mzazi Bora

Vidokezo Vya Kuwa Mzazi Bora

Mpe mwanao nafasi ya kufanya uamuzi wa kitu anacho kitaka, kwa njia hii ata soma jinsi ya kufikiria kuhusu anacho kitaka na kufanya uamuzi mzuri.

Ushauri wa kuwa mzazi bora umekuwepo kwa muda mrefu na kila mara kuna mabadiliko. Kumbuka kuwa kila mzazi ni wa kipekee na uhusiano wake na watoto wake haufanani na wa mzazi mwingine. Lakini ni vyema kuboresha utangamano wako na watoto wako kila mara. Tuna kudokezea jinsi ya kuwa mzazi bora!

Vidokezo vya kuwa mzazi bora

kuwa mzazi bora, baba

1.Kuwa na utangamano

Tenga angalau dakika 30 kila siku za kuwa na mtoto wako na kama una wawili, kila mtoto apate muda peke yake nawe. Unaweza uita baada ya jina la kila mtoto, kwa mfano, wakati wa Maria ama wakati wa Ali. Wape uhuru pia waamue wanacho taka kufanya katika muda huo, kisha wakati unao fuata uta chagua. Katika kipindi hiki, hakikisha kuwa unamsikiza mtoto wako kwa makini bila kufanya kazi zingine zozote. Weka simu yako mbali na uzime runinga.

2. Dhibiti hisia zako

Kuna baadhi ya wazazi wanao walipukia watoto wao, kuwa somea na kuwa kelelesha wanapo kosea. Wanapo feli shuleni, wasipo maliza kazi ulizo wapatia na kadhalika. Hakikisha kuwa una dhibiti hisia zako na kumwongelesha mwanao kwa njia ya utulivu. Kufanya hivi kuta wasaidia kuwa na imani kwako na kuja kwako wanapo kuwa na matatizo yoyote.

3. Usim nyamazishe anapo ongea

Mtoto wako anapokuja kwako na imani na kuanza kukwambia kuhusu vitu anavyo chukia na mambo yaliyo mtendekea shuleni, usim nyamazishe. Kuna kitu kilicho mfanya aseme alicho sema. Kama mzazi, unapaswa kumsikiliza kwa makini, kisha umpe mawaidha, mwongeleshe kwa upole. Umpe nafasi akuelezee yote anayo hisi, kwa kufanya hizi, mtakuwa na utangamano mzuri.

4. Msaidie kudhibiti hisia zake

Vidokezo Vya Kuwa Mzazi Bora

Mojawapo ya majukumu yako kama mzazi ni kumfundisha mtoto wako jinsi ya kudhibiti hisia zake. Watoto ni watu kama watu wazima na kuna nyakati ambazo watakuwa na hisia nyingi za kulia. Mtoto anapo lia, mwache alie, sio lazima kumtuliza kila mara, mhakikishie kuwa ni sawa kulia na kutoa uchungu wote ulio ndani. Pia epuka kutumia usemi kama 'wewe ni mvulana haupaswi kulia', mtoto ni mtoto haijalishi jinsia yake na ni vyema wanapo onyesha hisia zao kuliko kuzifungia ndani. Mtoto wako anapaswa kuhisi kuwa ako salama kukimbia kwako, kukukumbatia na kulia anapo hisi hasira ama kuumizwa.

5. Kuwa na wakati wa kucheka

Watoto wanapenda watu wacheshi hasa kama watu hawa ni watu wanao wa fahamu na kuwapenda kama wazazi wao. Hakikisha kuwa unapata wakati wa kumchekesha mwanao ama kutizima kipindi cha ucheshi pamoja.

6. Mfunze mwanao kufanya uamuzi

Kosa ambalo wazazi wengi hufanya ni kuamini kuwa watoto wanapaswa kufanya na kufuata kila kitu wanacho waambia na kuchagua kitu unacho taka. Kufanya hivi kunamfanya mtoto ashindwe kujifanyia uamuzi katika mambo muhimu maishani anapo kua. Mpe mwanao nafasi ya kufanya uamuzi wa kitu anacho kitaka, kwa njia hii ata soma jinsi ya kufikiria kuhusu anacho kitaka na kufanya uamuzi mzuri.

Soma Pia:Sababu Zinazo Mfanya Mtoto Wako Kucheka Akiwa Amelala

Written by

Risper Nyakio