Je, Wataka Kuwa Mzazi Mvumilivu? Tizama Mbinu Hizi

Je, Wataka Kuwa Mzazi Mvumilivu? Tizama Mbinu Hizi

How to become a patient parent: Deep breaths. Tally marks. Pretend someone's watching. What would mom do? How does this help? Take a break. Teach.

Mchakato wa kuwa mzazi mvumilivu ni mgumu, lakini ni muhimu na inawezekana.

mzazi mvumilivu

Jinsi ya kuwa mzazi mvumilivu: Mbinu za kubadilisha maisha

mzazi mvumilivu

Jiulize ‘kwanini’

Ni vigumu sana kuamini lakini watoto wengi ni wasumbufu. Sio kwa kuzaliwa vile ama kutoelewa vizuri ila, hivyo ndivyo walivyo, kwa sababu ya kitu fulani na tunapaswa kujiuliza kwanini.

Kuwa mtazamo

Siku ikiisha, jua kuwa unahusiana na watoto sio watu wazima. Akili za watoto wadogo bado zinakua na hazitakuwa zimekomaa hadi miaka 25. Kwa hivyo vitu zingine zitachukua muda, lakini kuna muda utakao fika ambapo mtoto ataweza kuelewa.

Jikaze kiakili na kimwili

Bob Marley hakuwa anatutania aliposema ’Binamu aliyenjaa ni aliyejawa na hasira’. Kwa hivyo kula au kunywa kitu kabla ya kushughulikia tabia za mtoto.

Kutunza mwili wako na akili kabla ya kukabiliana na mtoto itakupa mhemko mzuri. Pia itakusaidia kuwa na mtazamo shwari kuhusu nidhamu, njia itakayo saidia na pia mbinu yenye ubunifu.

Taswira

Njia hii husaidia kabla ya wakati kufadhaika kuwasili. Ukiwa peke yako pahali ambapo pametulia bila kelele. Kuwa na taswira ya jinsi utakavyo shughulikia mtoto wako, akifanya jambo ambalo litakukasirisha. Utachukulia hali hiyo vipi? Utakaa aje? Utasema nini? Mtoto wako atafanya nini? Itasaidia vipi uhusiano wako na mtoto wako? Fikiria kuhusu vitu hivi, kuwa na taswira shwara ya hali hii, hivi ndivyo unakuwa mzazi mtulivu.

mzazi mvumilivu
Jinsi ya kuwa mzazi mvumilivu inahitaji ukweli wa kibinafsi
Jipe muda

Sio njia ya sawa kushughulikia tabia ya mtoto wako. Kama umekuwa na siku mbaya, chukua muda na ufanye jambo ambalo litafanya uskie vizuri; kama kutengeneza nywele, fanya mazoezi ama chukuwa muda na kuongea na marafiki. Kuchukua muda wa kupumzika ili kusaidia afya yako ya kiakili itasaidia itasaidia kutupa mtazamo mwema na kutupa uwezo wa kuwa wazazi ambao wana utulivu.

Pata usaidizi

Ukijipata katika hali ngumu, ongelesha daktari wa mtoto. Utafiti unaonyesha tiba ya tabia za watoto inaisaidia na inachangia pakubwa wakati mtoto angali mchanga. Kwa hivyo kama unahitaji usaidizi wa wataalam, utafute ili kubadilisha maisha yako na mtoto wako.

Hesabu mpaka kumi

Mbinu hii inasaidia sana. Ukiskia unakasirika, acha alafu pole pole hesabu kutoka moja hadi kumi. Ukimaliza hautapatwa na msukumo wa kukelesha mtoto wako. Ukihesabu kwa sauti hadi kumi,watoto wako watajifunza kwamba katika wakati huo wanapaswa kukuondokea. Hivi ndivyo unaanza kuwa mzazi mtulivu.

Je, Wataka Kuwa Mzazi Mvumilivu? Tizama Mbinu Hizi

Pumua kwa uzito

Hii inasaidia sana pamoja na mbinu ya kuhesabu mpaka kumi, Pumzika kidogo, kisha urudie kupumua kwa nguvu. Ukifanya hivi unaskia hasira zikipungua.

Sema ombi

Usisahau kusema ombi kama unaamini kuwa maombi yanasaidia. Mwombe Mungu akupe uwezo wa kupenda, kusaidia na kuwa mzazi mtulivu na bila shaka maombi yako yatajibiwa.

Cheka

Wakati mwingine tunahitaji kujikumbusha hakuna mtu aliyesawa kikamili, tunapaswa kuwa tunafurahia muda huu pamoja na watoto wetu. Ni maisha inapaswa kuwa ya kufurahiwa-na ya kufurahisha. Cheka, kuwa na furaha. Haisaidii kila wakati lakini ni vyema kujikumbusha kila wakati.

Penda

Badala ya kushughulikia watoto wako wakifanya jambo mbaya kwa hasira, jifunze kuwaonyesha upendo. Mtoto wako akimwaga kitu ama avunje kitu ambacho ulikithamini sana, akuongeleshe vibaya au afanye jambo mbaya shule. Lishughulikie jambo lile kwa upendo kwani ndio mbinu shwari

Njia zingine unazopaswa kujaribu ni:

  • Kufunza
  • Jiifanye ni kama kuna mtu mwingine anaye kuangalia
  • Jiulize mama yako angefanya nini
  • Jiulize au hasira ndio njia haswa ya kutatua shida ile

Uzazi wenye furaha!

Kids Health

Also read: 5 Hilarious Things Parents Wish They Could Do To Their Children

Written by

Risper Nyakio