Watoto wetu wako katika kizazi tofauti na kilicho na raslimali zaidi. Hawafahamu njaa na kukosa ni nini. Kila wanapo enda kwenye duka na kusema wangependa hiki, wanakipata. Kutia juhudi sio jambo wanalo elewa kwa undani. Lakini wanapokua na kukumbana na dunia isiyo kuwa na huruma, hawajui jinsi ya kuishi. Na hakuna mzazi anayetaka watoto wake wakumbane na jambo hili. Suala kuu kuwa, jinsi ya kuwalea watoto wasiotarajia kupata vitu vyote wanavyo vitaka.
Jinsi ya kuwalea watoto

Kuna baadhi ya familia ambazo huwapatia watoto wao pesa kila wiki. Huku wazazi wengine wakiamini kuwa, watoto wao wanapaswa kufanya kazi za kinyumbani ili kupata pesa- kuwafunza dhamani ya kila shilingi.
Kulingana na wataalum wa mahusiano ya kijamii, Beth Johnson, wazazi wanao wapatia watoto pesa baada ya kufanya kazi za kinyumbani, wanawasaidia kuhisi ni haki yao. Kulingana na mtaalum huyu, watoto hawa wataanza kutarajia kulipwa baada ya kufanya kazi ndogo nyumbani. Wazazi wanapaswa kuwafunza watoto kusaidia na kazi za kinyumbani kwani wao ni timu moja kubwa.
Professa David Lancy kutoka Chuo Kikuu cha Utah, watoto huwa tayari kusaidia na kazi za kinyumbani wanapotimiza miezi 18. Katika tamaduni zingine, watoto huwa tayari wameanza kusaidia na kazi za kinyumbani bila kutarajia malipo yoyote. Kwa upande mwingine, baadhi ya wazazi huwafanyia watoto kila kitu bila kuwapa nafasi ya kusaidia. Watoto hawa huhisi kuwa kusaidia ni kazi ngumu na sio jukumu lao. Wanapo zidi kukua, hawataki kusaidia wazazi wao tena.
- Kuhusisha majukumu ya kinyumbani na pesa kunawachanganya watoto

Kufanya majukumu ya kinyumbani kunawasaidia watoto kuwajibika kifamilia. Pia ni ishara ya jinsi mwanao atakavyo fuzu katika kazi zao za usoni. Majukumu yanawasaidia watoto kufanya kazi vyema wakiwa kwa timu.
Kuwalipa watoto wako kwa kusafisha nyumba, vyombo na vyumba vyao hakuna manufaa yoyote. Hata hivyo, watoto wanaweza patiwa pesa wanapofanya kazi zaidi lakini isiwe kama malipo.
Hakuna umri mdogo sana kwa watoto kuanza kusaidia na majukumu ya kinyumbani - hasa kama wanajitolea kusaidia. Watakuwa wanauliza maswali mengi, kwa hivyo ni vyema kuwa na upole. Chukua muda kuwaelezea kivipi na maana ya kufanya mambo haya nyumbani.
Ila, usiwe wakali sana kwao, katika umri huu, wangali wanajifunza kufanya kazi. Kama ni kutengeneza kitanda, usitarajie kiwe kimetengenezwa kwa viwango vyako. Pongeza juhudi zao. Fuata vidokezo hivi viwili vya jinsi ya kuwalea watoto ili kuwalea watoto wasiodhani kuwa ni haki yao kupata kila wanacho kitaka.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Hatari Za Kuongea Mabaya Kuhusu Mchumba Wako Kwa Familia Na Marafiki Wako