Mbinu 3 Kuu Za Kuzuia Kutunga Mimba (Jinsi Ya Kuzuia Mimba)

Mbinu 3 Kuu Za Kuzuia Kutunga Mimba (Jinsi Ya Kuzuia Mimba)

Kutumia kondomu, kumeza tembe za kupanga uzazi ni baadhi ya mbinu za jinsi ya kuzuia mimba ambazo wanandoa wanaweza tumia.

Watu wanao jihusisha katika tendo la ndoa na wangetaka kufahamu jinsi ya kuzuia mimba, kuna hiari tofauti za kudhibiti ujauzito. Mbinu tofauti za kupanga uzazi hadi pale ambapo wana ndoa wako tayari kupata mtoto. Walakini, njia ya kipekee ya kuepuka mima ni kujitenga na tendo la ndoa.

Kulingana na ripoti iliyo tolewa na Shirika la Kupanga Uzazi huko Uingereza, lina kisi kuwa hadi asilimia 90 ya wanawake wanao jihusisha katika tendo la ndoa watapata mimba katika kipindi cha miezi 12 wasipo tumia mbinu zozote za upangaji uzazi. Kila wakati mwanamke anapo fanya tendo la ndoa, ako katika hatari ya kutunga mimba.

Jinsi Ya Kuzuia Mimba

Baadhi ya mbinu za kupanga uzazi sio lazima ushauriwe na daktari. Na kila mbinu ina athari zake hasi na chanya. Tuna kueleza kwa kina zaidi!

  • Utumiaji wa kondomu

https://www.africaparent.com/vyakula-vinavyo-sababisha-kisukari

Kondomu ndizo zinazo zuia dhidi ya maambukizi ya kingono. Utumiaji unao faa wa kondomu una linda hadi asilimi 90 dhidi ya mimba.

Je, unapaswa kuvalia kondomu kivipi?

  • Ifungue kwa makini
  • Weka ncha yake kwenye kibofu
  • Finya taratibu ili kutoa hewa kwenye ncha
  • Ivalie kwa utaratibu

Itoe muda tu baada ya kufanya mapenzi. Kisha uirushe kwenye tita la taka.

Hakikisha kuwa unachagua saizi inayo kufaa ya kondomu. Ikiwa ni ndogo sana, hautakuwa na starehe katika kitendo. Na ikiwa ni kubwa sana, huenda ikatoka katika tendo la ndoa.

  • Tembe za kupanga uzazi

kuzuia mimba baada ya ngono

Tembe za kuzuia kupata mimba huwa na vichocheo vya progesterone na estrogen. Hakikisha kuwa unachukua tembe ipasavyo na usikose kuchukua hata siku moja. Unapo kosa kufuata maagizo uliyo shauriwa, uko katika hatari ya kupata mimba. Vichocheo vinavyo tumika katika tembe hizi hukomesha kupevuka kwa yai, kwa njia hii, mwanamke hawezi tunga mimba.

  • Kutumia siku za kupevuka kwa yai (ovulation)

styles za kupata mimba

Kuzingatia mzunguko wako wa kurutubishwa wa kila mwezi unaweza kusaidia kuepuka kutunga mimba. Ikiwa hauna uhakika siku unazo kuwa na rutuba zaidi, tumia zifaa vya kupima temprecha yako ya basal, na kalenda. Jitenge na kufanya mapenzi ili kupunguza nafasi za kupata mimba.

Kumbuka kuwa kila mwanamke ni tofauti, sawa na mzunguko wake wa hedhi. Huchukua muda kuuelewa vyema.

Hizi ni baadhi ya mbinu za jinsi ya kuzuia mimba ambazo wanandoa wanaweza angazia katika juhudi zao za kupanga uzazi.

Soma Pia: Sababu Zingine Zinazo Mfanya Mwanamke Kupanga Uzazi

Written by

Risper Nyakio