Kukosa kujipanga ni kujipanga kufeli .Wazazi wengi wanaposhika mimba, jambo la kwanza mawazoni ni kujitayarisha. Ili kujipanga, lazima mzazi aelewa jinsia ya mtoto. Ila jinsia ya mtoto huonekana baada ya muda gani?
Jinsia ya mtoto huonekana baada ya muda gani?

Mtoto anapoumbika tumboni mwa mamake, wiki za mwanzo huwa ni maumbile tu. Ni ngumu kutambua jinsia ya mtoto kwa huu wakati. Ujauzito huja na mabadiliko mengi kwa wanawake na kupitia haya mabadiliko mtu anaweza kudadisi iwapo amebeba msichana au mvulana. Ila njia za kudadisi pekee zinaweza kuwa sio sahihi.
Hivyo kuna njia ambazo huwa na usahihi kwa asilimia kubwa. Ila kwa njia zote utaweza kugundua kuwa, jinsia ya mtoto hujulikana vyema katika wiki kumi ya ujauzito.
Wakati na Kipimo Kinachofaa Kutambua Jinsia Ya Mtoto

Njia moja na kuu ya kutambua jinsia ya mtoto ni ultrasound. Hii hufanyika kati ya wiki 18 na 20 za ujauzito. Pia ni vyema kukumbuka sio kila wakati ultrasound itaonyesha jinsia ya mtoto. Hivyo unaweza kuratibisha nyingine iwapo hukupata majibu kupitia ya kwanza. Wengine huwa na kanuni kutoweka wazi jinsia ya mtoto.
Njia nyingine ya kutambua jinsia ya mtoto ni kutumia njia ya ramzi. Hii ni njia mpya ya kutambua jinsia ya mtoto kupitia ultrasound. Hii inaweza kutumika katika wiki sita ya ujauzito. Hii huamua jinsia kulingana na eneo la placenta. Hivyo ni vyema iwapo unapata ultrasound mapema kwenye ujauzito, kuulizia juu ya eneo la placenta.
Njia nyingine ya kuelewa jinsia ya mtoto ni kupitia upimaji wa maumbile. Hii huwa kwa njia mbili. Moja hujulikana kama Amniocentesis. Hufanyika baada ya wiki 16. Ila inaweza kufanyika mapema kidogo. Hiyo nyingine hujulikana kama Sura ya Villus ya Chorionic ambayo huweza kufanyika wiki kumi ya ujauzito. Hivi vipimo huwa karibu asilimia 99 sahihi kutabiri jinsia ya mtoto.
Njia nyingine ambayo ina umaarufu ni kutumia sampuli ya damu ya uzazi. Vipimo hivi vipya hujulikana kama DNA. Hutumia DNA ya fetasi inayopatikana katika damu ya mama. Hii hugharimu pesa na pia hufanyika mwishoni mwa ujauzito. Mtihani mwingine huwa ule wa mkojo. Huu unaweza kufanyika pale nyumbani bila gharama yoyote. Huu unaweza kufanyika katika wiki kumi ya ujauzito.
Mabadilko mwilini mwa mama huwa njia nyingine ambayo wengi hutumia kutabiri jinsia ya mtoto. Ila hii inaweza kuchukua muda kwani mabadiliko huchukua wakati. Lakini njia ambazo tumeratibisha zitakusaidia kuelewa jinsia ya mtoto huonekana baada ya muda gani.
Soma Pia:Mama Anaweza Kufahamu Jinsia Ya Mtoto Kwa Kufuata Dalili Hizi Kuu Za Mimba Ya Mtoto Wa Kiume