Kuna masharti mengi kuhusu vitu unavyopaswa kufanya na usivyopaswa kufanya katika mimba. Masharti ya kawaida ni kama kujitenga na utumiaji wa pombe na dawa za kulevya. Mbali na masharti hayo ya kawaida, jitenge na vitu hivi katika mimba.
Jitenge na vitu hivi katika mimba
1.Kukandwa mwili

Kukandwa mwili huwa na manufaa kwa mwili na hasa katika mimba. Hata hivyo, kuna aina za kukandwa zisizo salama kwa mama katika miezi ya kwanza mitatu ya mimba. Aina ya kukandwa mwili ambapo mtu hudungwa sindano ndogo kwenye mgongo sio salama kwa mama katika miezi ya kwanza mitatu. Pia, tumbo ya mama haipaswi kukandwa katika miezi ya kwanza mitatu.
2. Paka
Mjamzito anapaswa kujitenga na kusafisha uchafu wa paka, kwani kinya cha paka huenda kikawa na maambukizi ya toxoplasmosis. Maambukizi haya humweka mama katika hatari ya kupoteza mimba ama mtoto kuzaliwa na matatizo ya ubongo ama kuona.
3. Kemikali za kusafisha
Kemikali nyingi za kusafisha huwa na onyo kwa wanawake wajawazito. Kwani bidhaa zilizotumika huwa hatari kwa afya ya mama na mtoto. Kabla ya kutumia kemikali hizi, ni muhimu kwa mama kuhakikisha kuwa hazina onyo kwa mama mjamzito. Dirisha zinapaswa kuwa wazi mama anaposafisha na kuhakikisha kuwa chumba kinapata hewa tosha.
4. Rangi
Rangi inayopakwa kwenye kuta huwa hatari kwa ukuaji wa mtoto katika trimesta ya kwanza ya mimba. Ni vigumu kudhibitisha kiwango cha hatari kwa mtoto. Hatari yoyote ile huathiri ukuaji wake, kwa hivyo ni vyema kwa mjamzito kukaa mbali na mahali penye rangi ambayo haijakauka.
5. Dawa zisizoagizwa na daktari

Kununua dawa kwa maduka ya dawa bila ushauri wa daktari ni hatari. Katika mimba, dawa ambazo mjamzito anachukuwa zinapaswa kuwa zimeagizwa na daktari ili kuhakikisha kuwa ni salama kwa afya yake na ya mtoto.
6. Kahawa
Kunywa vikombe vingi vya kahawa katika mimba kunaongeza shinikizo la damu na mpigo wa moyo. Mfumo wa kimetaboliki wa mtoto ungali unakua kwa hivyo kunywa kaffeini nyingi kunaushinikiza. Kaffeini inatokana na kahawa, soda, chokleti na baadhi ya dawa.
7. Vileo
Vileo vya aina yoyote ile katika mimba huwa na athari hasi kwa mama na fetusi. Kupitia kwa mfumo wa damu, vileo hupita kwenye placenta na kumfikia mtoto. Inaathiri ukuaji wa ubongo na viungo vingine vya mwili. Athari hasi katika mimba ni kama vile kuharibika kwa mimba, kujifungua mtoto kabla ya wakati, kuathiri ubongo wake ama mtoto kuzaliwa na matatizo ya kimaumbile.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi ya Kukabiliana na Ugonjwa wa Asubuhi Katika Mimba