Jukumu La Baba Katika Familia Na Maisha Ya Watoto Wake

Jukumu La Baba Katika Familia Na Maisha Ya Watoto Wake

Jukumu la baba katika familia yake ni muhimu sana kwenye maendeleo na ukuaji wa watoto wake ya kifizikia, kiakili na kimasomo.

Wakati ambapo karibu mwanamme yeyote ana uwezo wa kupata mtoto, kuna mengi zaidi katika majukumu muhimu ya baba kwenye maisha ya mtoto wake. Jukumu la baba kwa watoto wake ni nini hasa? Tofauti ya baba mlezi na baba anaye waleta watoto duniani tu ni gani? Makala haya yana angazia jukumu la baba katika familia yake na kwenye maisha ya watoto wake.

Baba ni muhimu sana katika ukuaji wa hisia na maendeleo ya watoto wake; pia ana uwezo wa kuwalea na kuwaadhibu.

jukumu la baba katika jamii

Utafiti umedhihirisha kuwa ikiwa baba ana mapenzi, kuwaegemeza watoto wake na kuwa katika maisha ya watoto wake, kuna saidia pakubwa katika ukuaji na maendeleo ya kiakili, lugha na kijamii. Ukihusisha ukuaji wa kimasomo, kujiamini, ujasiri na imani katika ayafanyayo.

Lengo la kuwepo kwa baba ni kuboresha maarifa ya mtoto, hisia zake, fizikia, utangamano, kijamii na ukuaji wa kiroho. Lengo kuu ni kuangazia kwa makini nguvu za mtoto wako na kutumia mbinu asili za mtindo wa ulezi wa baba.

Jukumu la baba katika familia yake na kwenye maisha ya watoto wake yana husisha lakini haya dhibitiwa kwa yafuatayo:

  • Kufunza kupitia kwa michezo

Kufunza kupitia kwa michezo ndiko kunako vuta watoto kwako. Kufanya mafunzo yawe ya kufurahisha ni kuu katika mtindo wa ulezi wa baba. Tumia michezo kuwafunza rangi, nambari, shepu na miundo na alfabeti. Kucheza michezo kwa kufuata sheria kunawafunza uwezo wa hisia za kijamii na pia kukuza ukuaji wao wa kiakili na kifizikia.

  • Kuwa kocha wao

Tunakuza ukuaji na maendeleo ya watoto ya kiakili na hisia kwa kuwa kuiga tabia ama kwa kuwafunza jinsi ya kufanya jambo. Wafunze jinsi ya kufanya kitu kwa utaratibu, hatua baada ya nyingine. Kwanza fanya mwenye kisha uwafunze kwa hatua na kusifu kila jaribio lao na kusherehekea wanapo kamilisha. Kuwapa motisha na sifa ni muhimu katika utendaji wa mambo unayo wafunza. Kumbuka kuwa wewe ndiye mfano wa kuigwa wa kwanza kwenye maisha ya mtoto wako.

father

  • Mapenzi kupitia kwa kicheko

Tunawafunza watoto wetu kucheka makosa yao kwa kuwaruhusu kuona tukicheka makosa yetu. Watoto wanapo cheka na baba yao, inawafanya wahisi vizuri na kuimarisha uhusiano wenu. Kicheko ni mojawapo ya njia za kuanza ama kuendeleza matumaini kwenye familia yako. Kuweza kujicheka na kucheka na familia yako kunawafunza watoto kujua kuwa wanaweza kuja kwako wakiwa na tatizo lolote. Wana hisi starehe na uhuru kuongea nawe kuhusu makosa yao. Kwa sababu wanaona ukicheka unapofanya makosa. Kuna saidia kuboresha utangamano wako na watoto wako kwa sababu wanaelewa kuwa ni sawa kufanya makosa kwenye familia yako.

Jukumu La Baba Katika Familia Na Maisha Ya Watoto Wake

  • Kuhusika kwa nia

Kuhusika kwa nia kwenye maisha ya mtoto wako kunahitaji wakati, utulivu na kuto kata moyo. Lakini uhusiano wote unahitaji kazi ikiwa ungependa ukue. Hakuna tofauti kusoma jinsi ya kuimarisha uhusiano wako na mtoto wako. Baada ya muda na juhudi, utaona mazao yake.

Mwishowe, mzazi mzuri hapimwi na jinsia yake mbali na wakati na juhudi anazo tia katika kulea watoto.

Soma piaWazazi Wanao Wasukuma Mabinti Wao Wanawalea Kufuzu Maishani

Written by

Risper Nyakio