Watu tofauti huhusisha krismasi na vitu tofauti. Kwa watoto, ni wakati wa kuonyeshana mavazi yao mapya huku wakiwatembelea jamaa na marafiki zao. Kwa watu wazima, ni wakati wa kupatana na marafiki na wanajamii na kuwa na muda wa kusisimua. Katika wakati huu wa sherehe, jumbe za krismasi za wapendwa huonekana kwa wingi katika mitandao na pia kwenye kadi zilizo andikwa. Tumetengeneza jumbe maalum ambazo unaweza kuwatumia jamaa na marafiki zako wakati huu.
Jumbe za krismasi za wapendwa

Hata kama inaweza semekana kuwa jumbe zote ni za wapendwa, tumechukua jukumu la kuzigawanyisha katika vikundi hasa ili iwe rahisi kwako.
Za wazazi
- Haijalishi mahali nilipo, haijalishi ninacho kifanya, nacheka ama naomba, ama hata kutenga muda kuwa nawe, wakati wote nitayafanya na mapenzi. Ulinifunza hayo na ulinifunza vyema. Nakudhamini. Krismasi njema, mama na baba!
- Asanti sana kwa kunipenda bila kipimo na wakati wote kuwa hapo nami. Iwapo nitafufuka duniani nyingine, ningependa kuwa mtoto wako. Krismasi njema, mama.
- Wakati wowote ninapofikiria jinsi familia inavyopaswa kuwa, akili yangu huwa na picha ya jinsi tulivyo kama familia. Wewe ni kila kitu kwangu. Asanti kwa kunipa picha ya jinsi familia inavyopaswa kuwa. Nakupenda baba. Chrismasi njema.
Ndugu

- Hatuwezi chagua familia zetu, hatuwezi jadiliana tunaowapata kuwa ndugu zetu. Tunaishi na tunaowapata. Lakini kwa kupitia maisha nawewe kando yangu, wakati mwingine kupigana na kuwa na wakati mwema pamoja, ningepatiwa chanya cha kuchagua, ningekuchagua wewe bado. Krismasi njema ndugu yangu!
- Hatuongei wakati wote, tunaweza kuwa na umbali mkubwa kati yetu, lakini najua wakati wote utaniunga mkono. Wakati wote, unaniegemeza, haijalishi ninachokipitia. Ni tumaini langu kuwa umoja wetu wa kidada hautawahi kuvunjika. Nakupenda dada yangu. Krismasi njema.
- Kila kumbukumbu ya krismasi ninayo ikumbuka, wakati wote, uko, na tabasamu lako la kupendeza. Natazamia kusherehekea krismasi zaidi pamoja kwa mapenzi, furaha na wingi. Krismasi njema, kakangu.
Marafiki wa familia

- Kuwa na furaha hata baada ya krismasi. Usipuuze kitu chochote maishani. Kuwa na furaha hata baada ya kipindi hiki cha kusherehekea na uwe na shukrani kwa kuwa na familia na marafiki wa kupendeza. Nakutakia kipindi chenye furaha.
- Umekuwa karibu sana na familia yetu, tunahisi kuwa wewe ni mmoja wetu. Wewe ni rafiki wa familia ambaye kila mtu angependa kuwa naye. Ni ombi langu kuwa krismasi hii itakuletea furaha kwako na familia yako. Krismasi njema mpendwa!
- Hatungeomba kuwa na rafiki bora wa familia. Asanti kwa furaha ya urafiki unayoileta. Ni tumaini langu kuwa kipindi hiki kitaleta furaha maishani mwako na kutimiza malengo yako. Krismasi njema!
Unaweza kutengeneza jumbe hizi kwa njia itakayo kupendeza zaidi.
Soma Pia: Kuupamba Mti Wa Krismasi: Mawazo Ya Mada Ya Kutumia Mwaka Huu