Ili uhusiano kuwa na ufanisi, nyote mnahitajika kutia juhudi, kuzungumza na kuwa na angalau maoni sawa kwa vitu vichache. Kabla ya kuingia katika uhusiano wowote, ni vyema kuhakikisha kuwa mnaelewana katika vitu vingi. Tazama vitu vya kuangazia kabla ya kuingia katika uhusiano na mtu yeyote.
Kabla ya Kuingia Katika Uhusiano

- Mawasiliano
Mawasiliano ni muhimu katika uhusiano. Kabla ya kuingia katika uhusiano na mtu yeyote, hakikisha ni mtu mitindo ya mawasiliano yenye afya. Mtu asiyezungumza mara kwa mara hathamini uhusiano wenu. Utabaki na maswali mengi kuhusu vitu tofauti za uhusiano wenu.
2. Usawa wa maadili
Angalia tabia za mhusika, yeye ni nani? Anaamini nini? Je, yeye ni mkarimu? Ana jali na kuwatunza watu wengine, ama anajiweka mbele bila kujali iwapo watu wengine wataathirika. Je, yeye ni wa kuaminika, ama anadanganya kila awezapo. Ana imani zipi kuhusu familia, mahusiano, pesa na kutoka nje ya ndoa? Kuwa mwangalifu wa vitu vidogo vidogo. Amini tabia zake sio maneno yake.
3. Mtindo wa maisha
Kuwa katika uhusiano hakumaanishi uyabadilishe maisha yako na uwateme marafiki wako. Hakikisha kuwa unatenga wakati wako mwenyewe, marafiki, familia na mpenzi wako. Ikiwa mtu anataka uyabadilishe maisha yako na usiingiliane na watu wengine, huyu sio mpenzi halisi. Kuwepo kwa mpenzi maishani mwako kunapaswa kuzidisha furaha na utulivu wako, wala sio kuupunguza.

4. Utangamano
Nina uhakika ushawahi kumpenda mtu, ila kulikuwa na tofauti kubwa kati yenu. Unaamini ila yeye haamini kuwepo kwa Maulana. Ungependa mpate watoto ila yeye hataki watoto maishani mwake. Kosa ambalo watu wengi hufanya ni kuingia katika uhusiano na watu wenye utangamano tofauti. Nia yao ni kuwabadilisha kuwa na mtazamo sawa nao. Hilo kamwe halitawahi kufanyika. Kamwe hilo halitafanyika. Kuna watu wengi wenye mtazamo sawa na wewe.
5. Ukomavu wa Hisia
Unahitaji kuwa na mtu aliyekomaa kihisia, anayejijua na kujielewa. Anavyozungumza, anavyowasiliana na watu wengine, mipaka anayoweka na anavyofanya vitu vyake. Kwa njia hii, hutahisi kana kwamba unalea mtoto katika uhusiano.
Soma Pia: Ishara 5 za Kujua Iwapo Mwanamme Anakuthamini Katika Uhusiano