Wakenya wajishika tama huku yakihuzinishwa na maisha magumu yanayo karibia. Haya ni baada ya mkuu wan chi Rais Kenyatta kutangaza kafyu nchini kote. Hatua hii inatarajiwa kuthibiti visa vinavyo endelea kuongezeka vya virusi vya korona. Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kafyu nchini Kenya ambayo inaanza siku ya Ijumaa tarehe 27 mwezi wa tatu mwaka wa 2020.

Virusi vya korona vilianza mwezi wa kumi na mbili mwaka uliopita mkoa wa Wuhan nchini Uchina. Iwapo hakuna aliyekusudia kuwa maradhi haya yangesambaa hadi kwa nchi na bara zingine. Watu kutoka nchi tofauti wame athirika na virusi hivi. Kufuatia idadi kubwa ya watu walio athirika na virusi hivi, Shirika la Afya Duniani lilitangaza virusi hivi kuwa janga duniani kote.
Kisa cha kwanza kilipo tangazwa Kenya, kila mkenya alihisi kana kwamba serikali ilikuwa imefeli katika jukumu lake kwa kuruhusu ndege kutoka nchi zingine ziendelee kuingia nchini. Serikali ilianza juhudi za kuhakikisha kuwa kuna hospitali ya kuwapeleka waathiriwa wa virusi hivi na kuwa hospitali hiyo ina vitanda tosha. Imeendelea kufanya jitihada ili kila mmoja anaye ingia nchini anapimwa na kuwekwa kwenye karantini ya siku 14.

Baada ya visa vya watu walioathiriwa na virusi vya homa ya korona kufika watu 28, rais Uhuru katika hotuba yake hayo jana aliimarisha kafyu. Hakuna mtu anaye paswa kuwa nje ya nyumba yake ama akizurura kutoka saa 6.00 jioni hadi 5.00 asubuhi. Ni jambo lililo watia wengi kero huku wakilia kuwa wanapaswa kuruhusiwa kuwa nje na kufanya shughuli zao kama hapo awali kwani wasipo fanya hivi, watakosha chakula. Huku wengine wakikubaliana na hatua iliyo chukuliwa na serikali ya kuweka kafyu nchini Kenya. Watu wengine ikiwemo watu mashuhuri nchini wangetaka rais achukue hatua ya kuwa na lockdown mzima nchini kote. Ambapo watu hawaruhusi kutoka manyumbani mwao ili waji karantini kwa angalau siku 14. Watu wengine walisema kuwa rais angetaza mwendo wan je na ndani ya mji mkuu wa Nairobi.

Ilhali wamama wengi wana furahi kwani mabwana zao watakuwa wanafika nyumbani na kuwa na wakati na familia zako. Hapo awali wengi walikuwa wanaenda kuchukua vileo na kupata sababu nyingi za kuchelewa kufika nyumbani. Pia watu wanaona kua hatua hii itasaidia kukabiliana na janga la virusi vya homa ya korona. Tuna zidi kuomba mwenyezi Mungu ailinde Kenya na watu wake na kutumainia kuwa janga hili litapita.
Chanzo: Tuko Kenya, Taifa leo