Ishara Tatu Zinazokuonyesha Kuwa Ni Wakati Wa Kuacha Kufanya Kazi Katika Ujauzito

Ishara Tatu Zinazokuonyesha Kuwa Ni Wakati Wa Kuacha Kufanya Kazi Katika Ujauzito

Did you know that work after eight months of pregnancy is as harmful as smoking? There's actually a study to back this up.

Hii ni mojawapo ya kesi zinazo kuwa binafsi na tofauti kwa kila mtu. Wanawake wengine huchagua kufanya kazi hadi dakika ya mwisho ili wazitumie siku za ruhusa zao wanapo jifungua. Wengine wanachagua "siku ya mwisho" kabla ili waweze kupata likizo kidogo kabla ya siku yao ya kujifungua, ama wanafanya mpango ili waweze kufanya kazi kutoka nyumbani katika siku za mwisho kabla ya kujifungua. Hamna jibu mufti kwa swali hili, "je ni ishara zipi za kuwacha kufanya kazi katika uja uzito?" Ila kuna maagizo ya kiafya itakayo kusaidia kupanga mapumziko yako ya kujifungua. Hakikisha kuwa unajadiliana sababu zinazo husiana na kazi na uja uzito wako na daktari wako.

Wanawake wengi huenda wakawa na uwezo wa kifizikia wa kufanya kazi yao ya kawaida hadi wiki 32-34 za uja uzito. Karibu na wakati huu, fikira za wanawake wengi huondoka kwa kazi na zinakuwa kwa kuwa mama. Jambo hili huenda lika athiri uamuzi wako wa kuwacha kufanya kazi. Iwapo una biashara yako, uwezekano mkubwa ni kuwa utangoja hadi mwisho wa uja uzito wako ili uwache kufanya kazi. Sio jambo mbaya, ila unapo ona mojawapo ama ishara zifuatazo zote, wacha kufanya kazi na umtembelee daktari wako.

Ishara za kuwacha kufanya kazi katika uja uzito

ishara za kuwachana na kazi unapokuwa mja mzito

Miongoni mwa kazi zingine huenda zika ongeza hataru yako ya kujifungua mtoto kabla ya wakati. Kama vile, kazi zinazo husisha kuinua vitu zito, kelele nyingi, kusimama kwa masaa marefu. Ongea na daktari wako kuhusu kupata ruhusa ya kimatibabu ili kupata mjukumu tofauti. Wanawake walioshuhudia kupata mtoto kabla ya wakati kutimia huenda wakaamua kumaliza kazi yao mapema.

Bila kujali kazi unayo ifanya, kuna dalili za onyo za kawaida kuwa ni wakati wa kufikiria tena kuhusu mipango yako ya kuendelea kufanya kazi. Je, shida za kukosa usingizi zina athiri utendaji wako wa kazi? Ama una shaka kuhusu matayarisho ya mtoto ambayo lazima ikamilike nyumbani? Huenda ikawa ni wakati ufikirie kuhusu kuwacha kazi.

1. Unaupoteza mkondo katikati ya siku.

Kukosa usingizi kuna athiri utendaji kazi wako wa mchana. Na kukufanya uwe mzembe, mwenye hasira na kusahau vitu. Pia unajipata ukiwa na mawazo mengi kuhusu matayarisho yaliyo sahaulika yanayo kungoja nyumbani.

2. Kusimama na kukaa hakuna starehe.

Kuumwa na mgongo, miguu iliyo fura na miguu na shida ya kupumua ni ishara kuwa unahitaji wakati zaidi. Hasa, kama kazi yako inahitaji uwe umesimama kwa muda mrefu.

3. Una ishara za kujifungua mapema.

Uchungu mwingi wa mgongo, kuumwa na tumbo, kutokwa na damu ina ashiria kuwa unastahili matibabu ya dharura. Kuna uwezekano kuwa mwuguzi wako ataku shauri upumzike.

Iwapo unahisi hivi siku za mwanzo wa uja uzito wako, ongea na daktari wako kwa sababu una uwezo wa kufanya kazi wakati huu bila shida zozote. Ila, iwapo haya yana tendeka katika mwisho wa uja uzito wako, wacha kufanya kazi na uhakikishe una pumzika nyumbani. Kwani akili zilizo na afya za mama zitamsaidia mtoto akue kwa kasi ndani yake.

Kama tulivyo sema, kila ishara ni ya kibinafsi na unapaswa kuongea na daktari wako.

Ishara Tatu Zinazokuonyesha Kuwa Ni Wakati Wa Kuacha Kufanya Kazi Katika UjauzitoHali za kiafya zinazo kuhitaji uwache kufanya kazi mapema

Kuna hali ambapo madaktari hushauri uwache kufanya kazi kwa ujumla. Hali zingine zina hitaji ulazwe hospitalini utakapoweza kuangaliwa. Zingine zinakuruhusu kukaa nyumbani. Kila hali inafaa kuangaliwa kwa kibinafsi na kujadiliwa na daktari wako:

Hii ni mifano ya hali ya uja uzito na matibabu ambapo madaktari huenda wakashauri upunguze ama uwache kufanya kazi:

  • Hali ambapo kondo la nyuma hushikana na kuta za uterasi katika eneo ambalo inafunika kiingilio cha uterasi
  • Ambapo kondo la nyuma humea ndani  ya kuta za uterasi.
  • Utando hupasuka kabla ya maumivu ya kujifungua
  • Upanuzi wa sehemu ya kizazi kabla ya muda ufaao
  • shinikizo la damu
  • kuzaliwa kabla ya miezi ya ujauzito kukamilika
  • Kupunguka kwa ugiligili unaopatikana ndani ya zalio
  • Kupata maumivu ya ujauzito

kazi na uja uzito

Kama tulivyosema hapo awali,mojawapo  ya shida hizi inapaswa kuchukuliwa kibanafsi na kuongelewa pamoja na daktari wako.

Umuhimu wa kuacha kufanya kazi kabla ya kujifungua

Kwa kina mama wengi, kwenda kazi wakati wa ujauzito si kazi .Unaeza penda kutoka nje ya nyumba na kuwa na kitu ya kufanya siku mzima.

Baadaye utapatwa na fikira ya kuchukua wiki kadhaa za mwisho za kupumzika sababu ya umuhimu wa kiafya. Lakini itakuwa inafaa baada ya muda. Tena, uamuzi wa kuacha kwenda kazini inategemea na mtu binafsi na unastahili kufikiria kwa makini unapopata mimba.

Also read: The Symptoms Of Stillbirth And How To Avoid Them

 

 

Written by

Risper Nyakio