Mama anaposhika mimba kuvuja damu huwa jambo la wasiwasi. Ila kiasi cha kuvuja damu kinaweza kuashiria iwapo ni hali ya dharura au la. Hivyo, kuna kiasi cha kuvuja damu kilicho kawaida katika mimba?
Kiasi Cha Kuvuja Damu Kilicho Kawaida Katika Mimba

Kwa kawaida mama mjamzito hutokwa na damu kiasi kidogo mwanzoni wa ujauzito. Hii hufahamikka kama implantation bleeding. Yai linaporutubishwa kwenye mirija ya fallopian baada ya siku sita hadi siku kumi na mbili, lile yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uterasi na kujipandikiza pale.
Huku kusafiri kwa hili yai hadi kuja kwa uterasi ndio hupelekea matone ya damu kutoka ukeni. Hivi hutoka kwa uchache mno kwenye kile kipindi mtu alifaa kupata siku zake hedhi. Hii huweza kutokea ndani ya siku kumi hadi kumi na nne. Baadaye huja ikakoma.
Hii hukoma kwani lile tendo la yai kujipandikiza kwenye mfuko wa uzazi limekamilika. Pia hujulikana kama spotting. Hii huwa sawa kabisa na huwa si hatari aidha kwa mama au mtoto. Ila kuna hali zingine ambazo zinahitaji uchunguzi zaidi. Kama vile kuvuja damu iwapo mimba inatishia kutoka.
Kwa Nini Mimba Itishie Kutoka?
Kuna mazinigira hatarishi kwa mama mjamzito kama vile:
- Mama aligongwa tumboni ama mama alipata mshtuko. Dalili yake ni damu kutoka ukeni ikiambatanishwa na maumivu au yasiwe
- Bakteria infection husababisha mimba kutishia kutoka. Hili hufanyika kwenye mji wa mfumo wa uzazi. Wakati wa uzazi sio uterasi pekee inayotanuka mbali pia servksi. Kwa hivyo kama kuna maambukizi mama huweza kuvuja damu
- Maambukizi ya virusi ikawa inaashiriwa na damu kutoka ukeni
- Wale wenye uzito mkubwa wanaweza kuwa na dalili ya mimba kutishia kutoka na kuashiriwa pia na kutokwa na damu ukeni
- Kuna plasenta ambayo hupitisha virutubishi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto. Hii plasenta inafaa kuwa juu ya tumbo la uzazi. Ila kwa kina mama wengine inaweza kuwa iko chini au kwenye shingo la uzazi. Hii husababisha matone ya damu kutoka kwenye uke
- Kubadilika kwa vichocheo vya homoni husababisha matone ya damu kutoka ukeni
Sababu Nyingine Kuu Za Kuvuja Damu

Kuvuja damu kabla ya wiki 28 za ujauzito hudhaniwa kuwa ni kuvuja damu mapema katika ujauzito. Ikitokea baada ya wiki 28 huitwa utokaji wa damu wa baadaye katika ujauzito. Mkato huu wa wiki 28 umezingatia uwezekano wa kuishi ikiwa mtoto atazaliwa kabla ya tarehe iliyotarajiwa katika wiki 28.
Matumaini ya kuishi kabla ya wiki 28 ni madogo sana katika nchi nyingi zinazoendelea. Hii ni kwa kuwa kuna upungufu wa vifaa vya afya vya utunzaji maalum kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Visababishi vikuu vya kuvuja damu mapema katika ujauzito ni utoaji mimba, kutoka kwa mimba mapema kwa sababu ya kufa kwa fetasi, mimba iliyotungwa nje ya uterasi (ectopic pregnancy) na mimba isiyo kuwa ya kawaida.
Kama unatokwa na damu unashauriwa:
- kupata mapumziko
- kutofanya mapenzi
- kuepuka kazi ngumu
- kujiepusha na uvutaji sigara, kunywa pombe na madawa ya kulevya
- Kuepuka mkazo wa mawazo
Kuvuja damu wakati wa ujauzito ni ishara ya jambo linalohitaji uchunguzi zaidi. Hivyo hakuna kiasi cha kuvuja damu kilicho kawaida katika mimba ila spotting.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi