Kichefu Chefu Katika Uja Uzito: Kinacho Sababisha Na Matibabu Yake

Kichefu Chefu Katika Uja Uzito: Kinacho Sababisha Na Matibabu Yake

Kuhisi kichefu chefu ni miongoni mwa ishara kuwa mama ana mimba. Inashuhudiwa katika trimesta ya kwanza na inasababishwa na mambo tofauti. Ni muhimu kwa mama kujua jinsi ya kukubaliana nayo.

Uja uzito wako ni chanzo cha furaha na pia hisia za usumbufu. Kichefu chefu cha ujauzito ni mojawapo wa ishara inayo shuhudiwa zaidi na wamama waja wazito.

Hadi asilimia 70 ya wamama waja wazito hushuhudia kichefu chefu katika wakati fulani siku za mwanzo mwanzo za safari yao ya uja uzito. Pia ni dalili ya kawaida inayo shuhudiwa wakati wa trimesta ya kwanza na wakati mwingine baada ya wakati huo.

Kichefu chefu huchangia kuhisi kusumbuka, na jambo nzuri ni kuwa haitahadharishi maisha ya mama wala ya mtoto. Kwa wakati mwingi, lina tazamiwa kama dalili kuwa una mimba. Kichefu chefu ni ya kimsingi katika ugonjwa wa asubuhi. 

 

Kuhisi kichefu chefu ni kwa maana nzuri

Kulingana na utafiti, unaposhuhudia kichefu chefu cha ujauzito katika trimesta ya kwanza, kuna uwezekano hautakuwa na uharibifu wa tumbo. Utafiti unaonyesha kuwa homoni ya uja uzito (HCG) ndiyo inayo sababisha hisia hizi za uchefu chefu. Mwili wako wa uja uzito unaanza kutoa homoni hii ya HCG punde tu baada ya kutunga mimba. Kuna uwezekano kuwa kuhisi kutapika na uchefu chefu unapokuwa na mimba yana onyesha ongezeko la homoni zinazo hitajika unapokuwa mja mzito. Wanawake wanaokuwa na hisia za hali hii kwa wingi wana idadi zaidi ya HCG kuliko wanawake wengine walizo nazo. Pia, wanawake walio waja wazito na watoto zaidi ya mmoja, wana uwezekano kupata ugonjwa wa asubuhi na kuwa na idadi zaidi ya HCG.

 

Kichefu Chefu Katika Uja Uzito: Kinacho Sababisha Na Matibabu Yake

Kinacho sababisha uchefu chefu katika uja uzito

 • HCG ni chanzo cha kwanza kinacho sababisha hali hii. Mwili wako unapo itengeneza homoni hii, utashuhudia hali ya kuto tulia.
 • Homoni ya estrogeni huongezeka siku za mwanzo za uja uzito na yaweza ongezeka kufuatia hisia za kichefu chefu.
 • Tumbo yako nyeti inaweza kuharibika zaidi mwili wako unapo zoea mabadiliko kufuatia uja uzito.
 • Fikira nyingi na uchovu husababisha mabadiliko ya mwili na kuchangia katika kutapika na kuhisi uchefu chefu.

Unapo tarajiwa kuhisi kichefu chefu cha ujauzito

 

 • Hali hii huanza katika wiki 4-8 za uja uzito. Ni dalili ya mapema ya uja uzito inayo kusudiwa kutokea wiki 4- wiki 8 baada ya kutunga mimba na inakusudiwa kupungua kutoka wiki 13- wiki 14 ya uja uzito. Ila kwa wanawake wengine waja wazito, inaweza kupitisha trimesta ya kwanza. Pia sio wanawake wote watakao shuhudia uchefu chefu wakati wote trimesta ya kwanza. Inaweza kuwa kwa wiki kadhaa peke yake na kwa wengine huenda ikaja na kuisha wakati wote katika trimesta hii yote.
 • Hali hii inajulikana kama ugonjwa wa asubuhi hata kama dalili hizi hazionekani wakati wa asubuhi peke yake. Utafiti unaonyesha kuwa ugonjwa wa asubuhi sana siku yote na sio masaa ya asubuhi peke yake.

Ukweli kuhusu ugonjwa wa asubuhi

Asilimia 50 ya wanawake waja wazito hushuhudia ugonjwa wa asubuhi. Hii ni hali ya kuhisi kichefu chefu unazo kuwa nazo trimesta ya kwanza ya uja uzito, kufuatia ongezeko la homoni mwilini mwako.

Ugonjwa wa asubuhi unaweza fuatiwa na kutapika. Madaktari wengi wanafikiria kuwa ugonjwa wa asubuhi ni dalili nzuri kwani inaonyesha kuwa kondo la nyuma ama zalio la mama linakua vizuri. Usiwe na hofu, kuna njia nyingi za kupunguza ugonjwa wa asubuhi.

 

Tiba za kinyumbani za kusaidia kuepuka na kutibu uchefu chefu katika uja uzito

 • Epuka vyakula na harufu zinazo weza kuchangia kuhisi uchefu chefu
 • Eka “crackers” za chumvi karibu na kitanda chako na ule kabla ya kulala. Jipe wakati wa chakula ulicho kula kusiagwa tumboni na uamke taratibu ukiwa tayari kutoka kitandani.
 • Kula viwango vichache vya chakula mara kwa mara badala ya kuvila vyakula vingi mara tatu kwa siku.
 • Kunywa maji machache unapo kula na uyanywe maji mengi baada na kabla ya kula.
 • Kula vyakula vilivyo kauka kama vile mchele kavu, mkate kavu, badala ya vyakula vienye unyevu nyevu.
 • Kula pipi na uweke zingine kwa kibeti chako na karibu na kitanda chako.
 • Chumba chako kiwe na hewa ya kutosha. Tembea nje ya nyumba kupata hewa safi.
 • Pumzika kwa wingi. Uskize mwili wako na ulale kwa muda kidogo.
 • Kunywa chai ya tangawizi na ndimu kupunguza hisia za uchefu chefu.
 • Ongea na daktari wako kuhusu vitamini za uja uzito unazo zinywa. Vitamini nyingi ya ‘iron’ mwilini husababisha uchefu chefu na kutumia vitamini tofauti itasaidia.
 • Uliza daktari wako kuhusu virutubisho vya vitamini ya B-6 inayo saidia kupunguza uchefu chefu na kutapika.

Hali sugu za uja uzito zilizo na uchefu chefu mwingi ni:

 • Hyperemesis Gravidarum. Hii ni hali ya kimatibabu inayo kufanya kupoteza virutubisho muhimu mwilini vinavyo hitajika katika uja uzito. Dalili zake ni uchefu chefu mwingi, kutapika, kupunguza kilo mwilini na elektrolyti za mwili kutofika kiwango kinachofaa. Hali ikiwa ndogo, inatibiwa kutumia lishe bora, kupumzika na antiacids. Hali ikiongezeka, ni muhimu kwenda hospitalini ili mama apewe maji na lishe.
 • Kupitia sindano ya kudunga. Ongea na mwuguzi wako kabla ya kutumia dawa zozote.
 • Molar Pregnancy. Inashuhudiwa panapo kuwa na ukuwaji wa tissue usio wa kawaida kwa uterasi.

 

Read Also: Is It Possible to Get Pregnant While You’re Breastfeeding?

 

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio