Mwongozo Wa Wazazi Kuhakikisha Watoto Wako Wako Salama Facebook

Mwongozo Wa Wazazi Kuhakikisha Watoto Wako Wako Salama Facebook

Una wasiwasi kuhusu mambo ambayo watoto wako wanafanya wanapokuwa kwa mitandao ya kijamii. Tunaeleza jinsi ya kutumia kifaa cha facebook privacy checkup.

Umaarifa wa mitandao ya kijamii inaendelea kuongezeka na watu zaidi ya bilioni 2.2 wanao kuwa utumia mtandao wa Facebook mwaka wa 2020 na karibu watu bilioni 2.8 wanao kuwa kwenye mitandao kama Instagram, Whatsapp na Messenger. Kufuatia ukuaji wa kujulikana kwa mtandao huu na watoto wasio fikisha umri wa makamu na wanatumia mtandao huu kuingiliana na watu. Kulingana na utafiti wa Ofcom (Ofisi Ya Mazungumzo), angalau asilimia 71 ya watoto kati ya umri wa miaka 12 hadi 15 wana kurasa za mitandao ya kijamii ambazo zinatumika hasa kwenye Facebook. Kuingiliana na marafiki, kutangamana, kupanga matukio, kuonyeshana picha na kusoma zaidi jinsi ya kutangamana na watoto wa umri tofauti bila shaka. Ila, hatuwezi kana ukweli kuwa Facebook ina athari zake hasi. Watoto wa umri mchanga wako katika hatari ya kupata athari hizi hasi kufuatia sababu tofauti. Kama wazazi, hii ni shaka zaidi na huenda ikawa vigumu kidogo kulinda watoto wako katika wakati wote. Kwa hivyo, unawezaje kuwalinda kutokana na hatari za mitandao ya kijamii? Kutumia kifaa cha Facebook privacy checkup na kuwaongoza watoto wako jinsi ya kulinda usalama wao kwenye mtandao utasaidia kuepuka hatari zisizo tarajika.

Mwongozo wa Kuwalinda Watoto Wako Wanapokuwa Kwa Mitandao Ya Kijamii Kwa Kutumia Kifaa Cha Facebook Privacy Checkup Kuangalia Usalama

Wakati ambapo huenda likaoneka kama jambo la kutisha kuwa salamisha watoto wako kutoka kwa hatari ya dunia ya mtandao, sio vigumu unavyo fikiria. Hapa Chini Kuna mwongozo mufti wa kukuongoza ili kuhakikisha kuwa usalama wa mwanao umezingatiwa.

1. Maswala ya Umri

facebook privacy checkup

Mipaka ya umri ya kufungua kurasa kwenye mtandao wa kijamii ni miaka 13, kwa hivyo jambo la busara kufanya ni kuhakikisha kuwa watoto wako wanakaa mbali na mtandao wa kijamii wa Facebook iwapo hawatimiza miaka 13. Unaweza wakubalisha kutumia mtandao ule na kuweka thibiti za mzazi ili kuziba tovuti zisizo na ujumbe wa watoto wa umri huu. Wakati ambapo watumiaji wengi wa mtandao huwa na siku za kuzaliwa zisizo za kweli wanapo fungua kurasa zao, ni kuenda mrama na matakwa ya Facebook.

2. Tumia Kifaa Cha Facebook Privacy Checkup 

Kuongeza kwa mipangilio ya usalama wako iliyoko, mtandao wa kijamii wa Facebook umeongeza kifaa cha facebook Privacy Checkup Tool inayo kupatia njia rahisi ya kuthibiti usalama wako. Ina sehemu nne, ambazo ni:

3. Nani Anaye Weza Kuona Jumbe Zako

Na mpangilio huu, una uwezo wa kuchagua ujumbe ambao watu wanaweza kuona wakifungua kurasa lako kama vile jinsi ya kuwasiliana nawe, unako ishi na jumbe unazo weka kwenye kurasa lako. Pia mpangilio huu unakukubalisha kuona watu ulio ziba na kukuruhusu kuongeza wengine.

4. Jinsi Ya Kuhakikisha Kurasa Yako Iko Salama

 Mpangilio huu unaangazia jinsi ya kuboresha usalama wa kurasa lako kwa kukupa vidokezo vya kuwa na nywila ya nguvu zaidi na kuongeza uwezo wa kujua iwapo kuna mtu anajaribu kuihack kurasa yako.

5. Jinsi Watu Wanavyo Weza Kukuona Facebook

facebook privacy checkup

 Angalia mipangilio hii kwa makini kwa sababu zinakusaidia kuchagua watu ambao wanaweza kupata kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kisha upunguze ombi kutiririka.

Maagizo zaidi

6. Mipangilio Yako Ya Matumizi Ya Data Kwenye Facebook

Ni muhimu sana kwa sababuinakukubalisha kuchagua habari unazotaka kurasa zingine ama apps ambazo unatumia kuingia kwa mtandao wa Facebook. Apps ambazo hutumii zinaweza futwa ama kutolewa kwa kuweka hiari ii kwenye mipangilio. Fuata maagizo haya: Bonyeza Settings ? Your Data Settings on Facebook ? Apps and Websites ? kisha ubonyeze hiari ya ‘Remove’.

7. Epuka Ombi Za Wageni Kuwa Marafiki

Hakikisha kuwa watoto wako wanakubali ombo za kuwa marafiki na watu wanao wajua na uwaeleze hatari za kuwa marafiki na wageni ambao hawawajui kabisa. Unaweza rekebisha siri ama usalama wako wa Facebook kwa kufanya hivi "Bonyeza ‘Who Can send Friend Requests’ na kisha uweke chaguo ‘Friends of friends’  ili watu msiojuana wasikutumie ombi za kuwa marafiki. Pia, waonyeshe watoto wako jinsi ya kuripoti jumbe fupi zisizo sawa kwa Facebook.

8. Jua Kuhusu Applications Za Mtu Wa Tatu

Kuna applications nyingi za mtu wa tatu kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook zinazo tumika na watoto na watu wazima. Iwapo ni za michezo ama vitu vingine, mwelezee mtoto wako kuwa applications hizi si nzuri na huenda zikawa na njama mbaya. Na hawawezi pata habari za kibinafsi bila ya kibali. Hakikisha kuwa ni ujumbe mdogo sana unaweza onekana na watu wengine kuepuka kuanguka kwa mtego. Pia ni vyema watoto wako wakijua kuwa sio vyema kubonyeza jumbe zote wanazo ziona kwenye mtandao.

9. Punguza Kuonekana Kwa Kurasa Lake Na Watu

Kuna wezekana kuficha kurusa ya mtandao wa kijamii ya mtoto wako kuto onekana watu wanapo mtafuta? Ndio, inawezekana. Enda kwa "Privacy Settings kisha enda kwa ‘Do you want Search Engines Outside of FB to Link to Your Profile Section. Bonyeza ‘Edit’ na uhakikishe kuwa sanduku lililo hapo  halija tickiwa.

10. Wafunze Watoto Wako Kuhusu Kuziba

facebook privacy checkup

Kuziba ama kuzuia ni mojawapo ya vipengele vyema zaidi katika mtandao wa kijamii wa Facebook. Ni vyema kuwajulisha watoto wako kuwa wanaweza waziba watu ambao hawa heshimu ama kuwalazimisha kuwa na urafiki. Ili kuziba, fuata maagizo yafuatayo, enda kwa Settings ? Privacy ? Block ? ‘Block User ama Block Messages’ section ? Andika jina la mtu unaye taka kuziba ? Chagua kurasa lake ? Bonyeza ‘Block’.  

11. Punguza Hiari Za Kuwataja Wengine

Mwongoze mtoto wako jinsi ya kuangalia picha na jumbe ambazo anatajwa na marafiki wako. Kufanya hivi, enda kwa hiari ya "Privacy /siri" enda kwenye kurasa ya juu na ufuate maagizo. Ukikubali maagizo hayo, utakuwa unajulishwa kuhusu kutajwa, na kisha kuamua iwapo ujumbe ama picha aliyo tajwa katika inaweza onekana kwenye kurasa yake ama la.

12. Tumia Nywila Yenye Nguvu

Hakikisha kuwa watoto wako wanajua umuhimu wa kuwa na nywila za nguvu na kuto mwambia mtu mwingine kuhusu neno lao la siri hata kama ni marafiki wao. Nywila yenye nguvu ni moja iliyo andikwa kwa kuzingatia maagizo ya yaliyo peanwa ya kuwa na herufi kubwa, ndogo, na nambari. Ina shauriwa kuepuka kutumia habari zako za kibinafsi na maneno ya michezo unayo ipenda ama wanyama wa nyumbani na kadhalika.

13.Funga Kurasa Yako Iwapo Hauitumii

Kufunga kurasa lako la Facebook ama tovuti zingine ni muhimu sana. Kuna punguza nafasi zako za kujipata kwenye tovuti zisizo faa, watu wanao ihack kurusa yako kuto pata ujumbe wa kurusa ya mtoto wako.

14. Jua Kuhusu Maonevu Ya Mtandao

Kumekuwa na visa vingi sana vya kunyanyaswa kwenye mtandao hapo awali na watoto wenye umri chini ya miaka 18 wana nafasi zaidi za kuwa kwa hatari hii. Wafunze watoto wako kuhusu shughuli kama vile kudhalilishwa, kuonewa, kunyanyaswa, kupitisha jumbe za siri na jumbe za tishio. Hakikisha kuwa unaongea na watoto wako kuhusu tukio zozote kama hizo na kurepoti kwa Facebook bila kusita. Huku ukizidi kuwashauri wakae mbali na mitandao ya kijamii kwa siku kadhaa. Pia, unaweza angazia shughuli za mtoto wako ili ujue iwapo kuna tishio zozote zinafanyika na umwongeleshe kuhusu jambo hilo.

15. Tumia Vifaa Vya Mtandao Vya Kufuatilia

Pia unaweza tumia vifaa vya kufuatilia kama vile McGruff Safeguard ama SafetyWeb kufuatilia shughuli za watoto wako wanapokuwa kwenye mtandao. Vifaa vya kufuatilia tovuti mbali mbali ambazo mtoto wako amejisajilisha, na kukujulisha shughuli zozote ambazo si njema. Pia iwapo mtoto wako ana andika jumbe zisizo sawa, utaweza kujua.

Kufuata vidokezo rahisi vya siri katika mtandao wa kijamii wa Facebook kutasaidia pakubwa katika kuwaweka watoto wako salama kutoka kwa madhara na hatari za mitandao ya kijamii. Kuwa marafiki na watoto wako, kuwakubalisha kuongea na wewe kwa urahisi na kuwaonyesha jinsi ya kufuata vidokezo vya usalama tulivyo orodhesha vya mtandao wa kijamii wa Facebook na kutumia kifaa cha Kuangalia Siri Facebook (Facebook Privacy Checkup). Ni muhimu sana katika kuwalinda kutokana na hatari zozote.

Soma Pia: Are Your Kids Safe On The Internet?

Kumbukumbu: Good House Keeping, PC World, Apple Society, Input Mag, Fool

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Vinnie Wong na kuchapishwa tena na idhini kutoka kwa theAsianparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Je, una maoni zaidi jinsi ya kuhakikisha kuwa watoto wako wako salama kwenye mtandao? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi!

Written by

Risper Nyakio