Kuchambua Zaidi Kuhusu Kifo Cha Ghafla Cha Watoto

Kuchambua Zaidi Kuhusu Kifo Cha Ghafla Cha Watoto

Kila mwaka, maelefu ya watoto chini ya umri wa mwaka mmoja huja bila kutarajia. Hali hii ya kuhuzunisha inafahamika kama kifo cha ghafla cha watoto maarufu kwa kimombo kama sudden infant death syndrom ama kifo cha kitandani (crib death) kwa sababu mara nyingi watoto hupatikana wakiwa wamekufa vitandani vyao.

Je, nambari za kifo cha ghafla cha watoto ni zipi?

Kulingana na MedlinePlus, chanzo kinacho ongoza cha vifo vya watoto wa umri kati ya mwezi mmoja hadi mwaka mmoja ni kifo cha ghafla cha watoto (SIDS). Hali hii inatendeka mtoto akiwa na mwezi mmoja hadi miezi minne.

Nini chanzo cha kifo cha aina hii?

Wataalum wa afya bado wanafanya utafiti zaidi kugundua kinacho sababisha vifo hivi. Lakini kwa sasa, Mayo Clinic imegundua sababu hatari zinazo ongeza nafasi za vifo hivi kufanyika.

Sababu mbili kuu ni:

 • Sababu za kifizikia
 • Sababu za mazingira ya kulala

Sababu za kifizikia zinazo sababisha kifo cha ghafla cha watoto

Kifo cha ghafla cha watoto

 1. Uzito mdogo wa kuzaliwa

Hii ni mojawapo ya sababu zinazo mfanya mtoto kuathiriwa na SIDS kwa sababu akili yake bado haija komaa vyema kudhibitisha majukumu ya kawaida kama vile kupumua na mpigo wa moyo.

2. Changamoto za kiakili

Ulemavu wa kiakili huongeza nafasi za mtoto kuugua ugonjwa huu. Hii ni kwa sababu pande moja ya akili ina jukumu ya kazi muhimu kama kuamka kutoka usingizini haifanyi kazi vyema.

3. Matatizo ya kupumua

Watoto ambao wamekuwa na homa kali huenda waka athiriwa na kifo cha ghafla cha watoto kwa sababu bado hawapumui vyema hata baada ya kupona kutokana na maambukizi hayo.

Sababu za mazingira ya kulala yanayo sababisha SIDS

Wakati mwingine, mazingira ya kulala huenda yaka athiri kifo cha ghafla cha mtoto. Hizi ndizo baadhi ya sababu zinazo ongeza hatari ya SIDS

 • Kulalia mahali ambapo ni laini sana

Kumlaza mtoto juu ya blanketi laini ama godoro kunaweza sababisha kufungika kwa mfumo wake wa kupumua.

 • Kulala na watu wengine

Hatari ya ugonjwa huu huongezeka mtoto anapo lala kwa kitanda kimoja na wazazi, ndugu zake ama wanajamii wengine.

 • Kuwekelea vidoli kwenye kitanda chake

Vidoli vinaweza sababisha SIDS kwa sababu kuna nafasi kuwa huenda vikamlalia mtoto usoni na kuepuka kupumua vyema.

 • Kumlaza mtoto kwa tumbo ama upande

safe sleeping tips for babies

Kumlaza mtoto kwa upande ama kwa tumbo kunaweza sababisha matatizo ya kupumua.

 • Joto

Mtoto anapo pata joto jingi kwa kasi anapokuwa amelala, kuna nafasi kuwa hawatakuwa na starehe na atapata matatizo ya kupumua.

Jinsi ya kuepuka kifo cha ghafla cha watoto

Wakati ambapo hakuna chanzo kinacho julikana cha tatizo hili, kuna uwezekano wa kutoa sababu zinazo ongeza nafasi za jambo hili kutendeka.

 • Hakikisha kuwa mtoto wako hakosi ratiba yake ya chanjo
 • Safisha kitanda cha mtoto na utoe vidoli vyote na mito na blanketi zisizo tumika
 • Mlishe maziwa ya mama peke yake kwa miezi ya kwanza sita ya maisha yake
 • Mnunulie mtoto kitanda chake

Wakati ambapo mtoto ako salama kulala kwenye kitanda chako, mlaze kwenye kitanda chake. Kwa njia hii, unapunguza uwezekano wa mtu mzima kupinduka na kumlalia.

 • Hakikisha kuwa mtoto hana joto jingi

Ikiwa hali ya anga haina joto jingi, hakuna haja ya kumfunikia mtoto anapo lala. Na ikiwa lazima umfunikie mtoto wako, hakikisha kuwa hujamfunikia uso.

 • Mlaze mtoto wako kwa njia inayo faa

Kifo cha ghafla cha watoto

Sisitiza kuwa mtu yeyote anaye mlaza mtoto wako, anamlaza kwa mgongo na sio kwa tumbo ama kwa pande. Lazima mtoto wako aangalie juu anapo lala.

 • Godoro lako linapaswa kuwa na  ugumu wa wastani na lisikubalishe maji kupita
 • Mnaweza lala kwa chumba kimoja na mtoto wako kwa miezi sita ya kwanza ila hakikisha kuwa analala kwenye kitanda chake
 • Unapo mfunikia mtoto, hakikisha kuwa blanketi haipiti mabega yake
 • Hakikisha kuwa hakuna mtu anavuta sigara karibu na mtoto wako
 • Weka temprecha za chumba cha mtoto wako zikiwa za kawaida; isiye joto sana ama baridi sana

Kifo cha ghafla cha watoto hakina vyanzo vinavyo julikana, lakini vidokezo hivi vitakusaidia kuhakikisha kuwa mtoto wako ako salama.

Vyanzo: MedlinePlus

Mayo Clinic

NHS

Soma pia:Sababu Zinazo Mfanya Mtoto Wako Kucheka Akiwa Amelala

 

Written by

Risper Nyakio