Kifo cha Professor Gilbert Ogutu

Kifo cha Professor Gilbert Ogutu

Professor mashuhuri Gilbert Ogutu Achieng’ ame kata kamba! Profesa huyu mwenye miaka 78 alikuwa mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Inasemekana kuwa kifo hiki kilisababishwa na kujinyonga. Mwili wake unasemekana kuwa ulipatikana nyumbani mwake katika kijiji cha Wambasa, Yimbo ya katikati huko Bondo. Alijinyonga kwa kutumia leso aliyoifunga kwenye dirisha ya chumba chake cha kulala. Mfanyakazi wake aliseme kuwa alipata mwili wake siku ya Jumapili saa tatu.

Mwili wa Professor Ogutu ulipatikana ukining’inia kutoka kipande cha nguo katika chumba chake cha kulala. Kulingana na mkuu wa polisi kutoka kituo cha Bondo, alijinyonga usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili. Ila hakukua na alama zozote za kuumia kwenye mwili wake.

Kifo cha Professor Gilbert Ogutu

Picha ya hayati professor Ogutu kulingana na habari za Nation

Profesa huyu na bibi wake wa pili walifika nyumbani mwao usiku wa Ijumaa kisha bibi yake akatoka kuelekea Kisumu jioni ya siku ya Jumamosi.

Mfanyakazi aliye upata mwili wa profesa alisema kuwa alikuwa ameenda kumwamsha kama ilivyo desturi yake baada ya kutengeneza maji yake ya kukoga. Ila alipigwa na butwaa na bubuwazi baada ya kuona mwili wa mkubwa wake una ning’inia bila uhai. Mfanyakazi huyu alisema kuwa mwenda zake bwana Ogutu alikuwa sawa usiku wa Jumamosi alipokuwa akienda kulala. Ila kilicho mfanya kuchukua uhai wake hakija bainika bado. Upelelezi zaidi bado unaendelea kujua hasa ni nini kilicho sababisha kifo chake profesa Ogutu.

Kifo cha Professor Gilbert Ogutu

 

Hayati professor Ogutu amekuwa akihudumia chama cha wazee cha jamii ya Waluo huko Bondo kwa zaidi ya miaka 12 kabla ya kifo chake. Alikuwa katibu wa chama hiki na kuwapa mawaidha na busara kuhusu mambo muhimu yaliyo kuwa yakitendeka. Alikuwa makini katika kuhifadhi tamaduni za kiafrika. Na alikuwa mwananchi wa kuigwa katika kijiji chake. Imani yake ilikuwa kuwa licha ya umri wako, una manufaa mengi sana ambayo unaweza fanya kuleta mabadiliko chanya katika jamii unayoishi.

Kifo cha Professor Gilbert Ogutu

Ni wakati mgumu kwa jamaa na familia ya marehemu bwana Ogutu na jamii ya Chuo Kikuu Cha Nairobi.

Mwili wake ulipelekwe kwenye chumba cha wafu cha hospitali ya Bondo.

Written by

Risper Nyakio