Ni Kipi Kinacho Tendeka Mtoto Anapokosa Mojawapo Ya Chanjo Zake?

Ni Kipi Kinacho Tendeka Mtoto Anapokosa Mojawapo Ya Chanjo Zake?

Kliniki za chanjo huonyesha ratiba za chanjo za kitaifa kwenye kuta zao. Mara nyingi, wazazi hupata kadi za chanjo zinazo onyesha chanjo za kuhudumiwa katika kila hatua. Kadi hizi na chati zinaifanya rahisi kwa wazazi kufuata kwa makini ratiba hasa ya chanjo. Ila baadhi ya wakati, maisha huingilia kati na chanjo hukosa kufuata ratiba. Kwa hivyo, ni kipi kinacho tendeka unapokosa chanjo?

what happens when you miss a vaccination

Kipi Kinacho tendeka unapokosa chanjo?

Bila shaka vitu hutendeka, na maisha yana mambo mengi. Wazazi husahau; watoto hugonjeka, wauguzi na madaktari hugoma; siku kuu huchukua siku za chanjo. Kuna sababu nyingi kwa nini wazazi na watoto hushindwa kufuata ratiba ya chanjo. Kwa hivyo, kipi kinacho endelea unapo kosa chanjo? Na ni nini wazazi wanaweza fanya kurekebisha ratiba ya chanjo ya mtoto wao?

Katika makala haya, tunajibu baadhi ya maswali kuhusu mambo yanayo tendeka unapo kosa chanjo. Pia tuta angazia swala la jambo la kufanya kurekebisha hali ile. Ushauri wetu unafuata ripoti kutoka kwa Shirika la Afya Duniani. Pia tuna husisha ushauri kutoka kwa wataalum bora zaidi wa afya nchini.

Unacho paswa kufanya ukikosa kupata chanjo

Unaweza:

1) Ongea na mtaalum wako wa afya

Iwapo mtoto wako amekosa chanjo, unaweza ongea na mtaalum wako wa afya. Hiyo ndiyo hatua ya kwanza ya kuchukua. Ni vyema zaidi kuongea na mwuguzi aliye somea kuhudumu chanjo.

Unapokuwa na wakati na mtaalum wa afya, mweleze yote. Mwambie siku hasa za chanjo zilizo pita iwapo kunazo. Ikiwa una kadi yako ya chanjo, mpe aone. Ina historia ya chanjo za mtoto na itasaidia kufanya uamuzi kuhusu jambo analo paswa kufanya.

Hapa kuna mambo machache ambayo unapaswa kuongea kwa wazi kuyahusu:

• Iwapo mtoto wako anaanza ratiba ya chanjo akiwa amechelewa

• Idadi ya dosi ambazo mtoto wako amepokea

• Iwapo ratiba ya chanjo ime athiriwa

2) Kuwa na mawazo huru

Ratiba ya chanjo isiyo fuata utaratibu wa tarehe huenda ikawa tatiza wataalum wa afya. Ushauri utalingana na kipindi cha muda kilicho pita kutoka chanjo ya mwisho. Iwapo muda ulio pita ni mwingi, itakuwa tatizo zaidi.

Kulingana na wataalum wa afya, baadhi ya chanjo zinaweza rudiwa iwapo umekosa. Hii ndiyo kesi hasa kwa chanjo ambazo mtoto hakupokea za Hepatitis B, diptheria, Vit A, measle, polio, tetanus na acellular pertussis. Katika visa vilivyo nadra, mtaalum ataanza ratiba ya chanjo mwanzo. Inalingana na historia ya mgonjwa. Mtaalum wa afya hufanya uamuzi kulingana na mgonjwa anaye shughulikia.

Unapokuwa ukishangaa kinacho tendeka unapokosa chanjo, kuwa na mawazo huru. Tia bidii kuhakikisha kuwa unafuata ushauri mpya na ratiba za chanjo kwa umakini.

kinacho tendeka mtoto anapokosa chanjo

3) Fuata kwa umakini ratiba ya chanjo

Baada ya ratiba ya chanjo kurekebishwa, fuata ratiba mpya. Usikose kupata chanjo zozote, ni vyema zaidi ikizingatiwa ili mtoto asikose tiba zinazo kuwa kwenye chanjo zili. Chanjo nyingi hazifanyi kazi vizuri zinapo chukuliwa mapema sana ama ukiwa umechelewa sana. Hakikisha unazingatia ratiba ipasavyo.

Hapa ni baadhi ya vitu unavyo weza kufanya kuhakikisha unazingatia ratiba ya kitaifa:

• Weka makumbusho kwenye kalenda yako ya simu ama kifaa cha elektroniki unacho kitumia

• Waulize watu walio karibu nawe wakukumbushe tarehe inapo wadaia.

• Andika chini tarehe ya chanjo kwenye kitabu chako cha makumbusho. Ulezi unahusisha kufanya mambo mengi katika wakati mmoja. Huenda ukasahau usipo andika tarehe yako.

• Weka kipande cha karatasi kilicho na tarehe hiyo kwenye mlango wa bafu yako.

4) Nini Kinacho Tendeka Unapokosa Chanjo Muhimu

Ni muhimu kujua kuwa baadhi ya chanjo huwa na siku hasa ambapo zinapaswa kuchukuliwa. Mifano maarufu ya chanjo hizi ni kama vile dhidi ya rotavirus na pneumococcal conjugate.

“Chanjo ya rotavirus inasaidia kuepuka kuharisha. Watoto wanapaswa kupokea dosi ya kwanza katika wiki ya sita ya maisha yao. Kisha dosi ya mbili katika mwezi wa tatu wa maisha yao. Baada ya mwezi wa tano na wa sita, chanjo haitafanya kazi ipasavyo," asema daktari Ifeyinwa Ihejirika, mtaalum wa afya ya uke katika hospitali ya Enugu.

Dosi hizi tatu za pneumococcal conjugate zinapaswa kuchukuliwa katika miezi ya kwanza tisa. Mtoto anapo pita umri wa miezi tisa, hawezi pokea chanjo alizokosa. Lakini iwapo mtaalum wa afya anampatia chanjo ile, huenda ikakosa kumlinda mtoto ipasavyo.

kinacho tendeka unapokosa chanjo

Usisahau kuwa maana ya ratiba ni kuboresha kinga ya watoto wadogo na walio zaliwa. Lengo ni kulinda watoto kutokana na maradhi ya kuambukizwa mapema maishani mwao wakati ambao kinga yao ingali dhaifu.

Shirika la Afya Duniani lina amini kuwa ni kawaida ndani na nje ya makundi ya chanjo. Programu zimeanzishwa kuwashughulikia watu walio na ratiba za chanjo zisizo na utaratibu. Kwa hivyo iwapo umekosa chanjo hata moja, tembelea kituo cha afya kilicho karibu zaidi nawe. Ongea na wataalum na uwaelezee tatizo lako.

Kumbukumbu: World Health Organisation 

NHS

Soma pia: Vaccines that may cause fever in your child

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio