Je, ulifahamu kuwa kinya cha kwanza baada ya kujifungua huwa na uchungu mwingi?
Katika miezi tisa inayo pelekea kujifungua kwako, wamama wanao tarajia huwa shupavu, wakijua kuwa baada ya safari yao ya mimba, wata stahimili uchungu na kukosa starehe kunako andamana na kuleta mtoto duniani.
Wanapo pitia uchungu wa uzazi na kujifungua, wao huhisi uhuru fulani, lakini ngoja.. kuna mengi. Lazima washinde changamoto nyingine wasio kusudia: mwendo wao wa kwanza wa tumbo. Wamama wengi wanaweza kubaliana kuwa kinya cha kwanza baada ya kujifungua huenda kikawa na uchungu mwingi kupindukia, hata zaidi ya uchungu wa uzazi na kujifungua.
Nini hiyo hasa?
Sababu sita kwa nini kinya cha kwanza baada ya kujifungua huuma

- Huenda wakawa wamevimbiwa kwa siku nyingi
Baada ya kuzaliwa, itachukua muda kwa mwili wako kupona na kurudia utendaji kazi wake wa kawaida, ukihusisha kumeng'enya chakula na kukichakata. Unywaji wa dawa na kukosa maji tosha mwilini pia huchangia katika kuvimbiwa baada ya kujifungua.
Kwa wamama walio jifungua kupitia kwa upasuaji wa C-section, kuvimbiwa kunaweza kuwa tatizo la kawaida, hasa dawa za kupunguza uchungu zinapo pungua.
- Huenda walipuuza vilainisha kinya
Umuhimu wa vilainisha kinya baada ya kujifungua hupuuzwa, lakini vinaweza saidia kupunguza mwendo wa tumbo.
- Huenda wakawa wali shuhudia kuraruka kwa uke
Wanawake wengi wanao jifungua kufuatia njia ya kawaida ya uke lazima wafanyiwe episiotomy ama kukatwa kwa sehemu kati ya uke ili kurefusha njia ya kujifungua. Kuraruka kwa vulva na perineum kunaweza tendeka bila kukusudiwa wakati wa uchungu wa uzazi.
Hata kama mama wa mara ya kwanza haku shuhudia kuraruka kwa uke, huenda bado akawa na uchungu na uvimbe sehemu hiyo.
Baada ya kuraruka ama episiotomy, madaktari hushona kidonda hicho ili kipone. Na huenda kukadumu siku kadhaa ama wiki chache. Hata kwa wamama walio jifungua kupitia upasuaji wa C-section, huenda mishoni hiyo bado ikahisi laini.
Wamama wapya wanawezaje punguza uchungu huo?

Wasiliana na daktari wako kwa matibabu yanayo faa ya kudhibiti kuto starehe kule. Krimu za kutuliza, ibuprofen na vilainisha kinya vinaweza saidia. Kushinikiza sehemu hiyo ni hatua ya kudhibiti uchungu wakati wa mwendo wa tumbo.
Unaweza tumia pedi ya uzazi na ushinikize kwa wepesi kwenye uke wako. Epuka cheese ama vyakula vya kufanya kinya kiwe kigumu kama mkate mweupe, mchele mweupe, mayai na pasta. Badala yake, kula matunda na mboga, epuka zilizo hifadhiwa pamoja na vyakula vilivyo chakatwa.
Ikiwa uchungu haupungui na kila mwendo wa tumbo, wasiliana na daktari wako ili kujua vyanzo zaidi vya kuangalia ili kumsaidia daktari wako kwenye safari yako ya uponaji, ili kufurahia miezi ya kwanza michache ya kuwa mama.
Vyanzo: The Huffington Post, Romper, What to Expect
Soma Pia: Ishara Za Uchungu Wa Uzazi