Unapo amka, unapaswa kunywa nini kama kinywaji chako cha kwanza cha siku? Kumbuka kuwa, unacho kunywa ama kula asubuhi kabla ya kuanza siku yako kina dhibiti jinsi siku yako itakavyo kuwa.
Unahitaji kuwa na nishati tosha ya kuhimiza utendaji kazi wa mwili wako wa kila siku. Chai, kahawa, maji na sharubati ni mojawapo ya vinywaji maarufu sana ambazo watu huchukua wanapo anza siku zao. Wengi huenda wakasema kuwa kuna kinywaji kilicho bora kuliko kingine, lakini, tungependa ufanye uamuzi huo.
Kinywaji cha kwanza siku yako

Kunywa chai asubuhi unapo amka na kabla ya kuanza siku yako ni maarufu sana duniani kote. Hata kama kuna aina tofauti za chai duniani kote. Kuna chai ya kijani, nyeusi, nyeupe na ya oolong. Chai ina manufaa mengi ya kiafya. Kama vile kuwa na antioxidants zinazo kusaidia kustahimili mazoezi marefu, na kupigana dhidi ya saratani. Hata kama ina kafeini, inausaidia mwili wako kuwa na maji tosha. Ikiwa una lenga kupunguza uzito wa mwili, kunywa chai ya kijani.
fruit smoothie,fruit juice
Kunywa sharubati asubuhi kuna faida nyingi za kiafya kulingana na matunda na mboga zilizo tumika. Kuna sharubati ya kila kitu na kukusaidia kutimiza malengo yoyote yale ya kiafya uliyo nayo. Kunywa sharubati asubuhi kunakusaidia kutoa sumu kwenye damu, kupunguza hamu ya kula, kuwa na nishati tosha, ngozi inayo ng’aa na kupunguza uzito kwa kasi.

Tofauti na imani ya watu wengi, kahawa ina manufaa ya kiafya. Kulingana na utafiti, kahawa ina antioxidants zaidi kuliko baadhi ya matunda na mboga. Ina kusaidia kuchoma ufuta mwilini, kupigana dhidi ya aina chache za saratani na pia kupunguza uchungu mwilini. Kahawa inatumika kuboresha uwezo wako wa kukumbuka.

Kunywa maji asuuhi kabla ya kula chochote kuna manufaa mengi ya kiafya. Maji hayana virutubisho vyovyote lakini yana majukumu mengi. Yana saidia kusafisha coloni na kusaidia tumbo kutumia virutubisho kwa urahisi na pia kuhimiza uchakataji wa chakula tumboni. Pia, inasaidia kutoa sumu kwa damu yako na kuacha ngozi yako iking’aa.
Soma Pia: Ratiba ya lishe bora ya kuzingatia nchini Kenya ya mama mja mzito