Aina Mbili Kuu Za Vipima Mimba Vilivyoko!

Aina Mbili Kuu Za Vipima Mimba Vilivyoko!

Kipimo cha mimba hupima uwepo na kiwango cha kichocheo cha human chorionic gonadotropin kwa mkato hCG.

Vipimo vya ujauzito vimerahisha mambo. Hivi sasa, mama anaweza fahamu endapo ana mimba ama la akiwa nyumbani mwake. Kwa kutumia kipima mimba kinacho patikana kwenye maduka ya madawa, mwanamke ataweza kufahamu hali yake ya ujauzito. Sio lazima afike kwenye maabara ama vituo vya afya kufanyiwa kipimo. 

Kuna mambo mengi ambayo mama anapaswa kufahamu kabla ya kujitosa kwa utumiaji wa vipimo vya mimba vya kinyumbani.

Je, kipimo hiki kinafanya kazi vipi?

kipima mimba

Kipimo cha mimba hupima uwepo na kiwango cha kichocheo cha human chorionic gonadotropin kwa mkato hCG. Hii ni homoni ya mimba. Baada ya yai la mwanamke kurutubishwa na manii ya mwanamme, na kujipandikiza kwenye kuta za mji wa mtoto. Homoni ya hCG hutolewa mwilini. Huchukua muda wa takriban siku kati ya 12 hadi 14 kwa homoni hii kutolewa mwilini.

Baada ya siku 14, idadi ya kichocheo hiki huongezeka mara mbili zaidi kila baada ya siku mbili.

Aina za vipima mimba

COVID-19 effects on unborn baby

Kuna aina mbili kuu ambazo hutumika kudhibitisha iwapo mama ana mimba ama la.

  • Kipimo cha damu

Kipimo cha aina hii hufanyika hospitalini kwa sababu kina hitaji vifaa spesheli. Kipimo cha damu kinaweza onyesha ikiwa mwanamke ana mimba hata kabla ya siku 14 kutoka alipo fanya tendo la ndoa kutimia.

Kipimo hiki huchukua muda ikilinganishwa na kipimo cha kinyumbani. Kina pima kuwepo kwa kichocheo cha mimba na idadi ya kichocheo hicho mwilini.

  • Kipimo cha mkojo

Kipimo hiki ni maarufu sana. Kinajulikana kwa jina lingine kama kipimo cha kinyumbani. Kipima mimba kinatumika kuonyesha kuwepo ama kutokuwepo kwa mimba. Ni haraka na unaweza kufanyia kwa usiri wa nyumba yako.

  • Nunua kipimo hiki kwenye duka la madawa.
  • Weka mkojo wako wa kwanza siku kwenye kontena safi.
  • Kisha uweke upande wa kipima mimba hicho ulio onyeshwa ndani ya kontena hiyo.
  • Kilaze kwenye mahali laini kwa dakika zilizo dhihirishwa.
  • Baada ya wakati kutimia, angalia matokeo yake.

Je, kipimo hiki ni sahihi?

Unapo fuata maagizo yaliyo dhihirishwa na kutumia kifaa kilicho sawa, matokeo yake yatakuwa sahihi. Ikiwa una shaka kuhusu matokeo uliyo yapata, usikawie kwenda kwenye kituo cha afya kufanyiwa vipimo zaidi.

Soma Pia:Uzito Wa Mapema Katika Mimba Una Athiri Saizi Ya Mtoto Anapo Zaliwa

Written by

Risper Nyakio