Fahamu Jinsi Vipimo Vya Ujauzito Hufanya Kazi

Fahamu Jinsi Vipimo Vya Ujauzito Hufanya Kazi

Vipimo vya mimba hupima kiwango cha kichocheo ama homoni ya human chorionic gonadotropin kwa mkato HCG kwenye damu ama mkojo.

Vipimo vya ujauzito ni muhimu katika kumsaidia mwanadada ama wanandoa kufahamu ikiwa wana tarajia mtoto ama la. Kuna aina tofauti ya vipimo vinavyo tumika kupima mimba. Kama vile kipimo cha asili cha kupima mimba kutumia chumvi ama kupima damu. Makala haya yana lenga kukuelimisha jinsi vipimo vya mimba vinavyo fanya kazi.

Jinsi vipimo vya mimba vinafanya kazi

jinsi ya kutumia kipimo cha mimba

Vipimo vya mimba hupima kiwango cha kichocheo ama homoni ya human chorionic gonadotropin kwa mkato HCG kwenye damu ama mkojo. Kichocheo hiki huchakatwa mwilini siku sita baada ya yai lililo rutubishwa kujipandikiza kwenye kuta za uterasi ama kuta za mji wa mimba. Idadi ya kichocheo hiki huongezeka mara mbili baada ya siku 6 na kuzidi kuongezeka kwa kiasi hicho baada ya kila siku 2 ama 3.

Aina za vipimo

kupima mimba kutumia kitunguu maji

Kuna vipimo vya aina mbili vinavyo tumika kupima mimba ili kufahamu kama mwanadada ana mimba. Hasa kipimo cha damu ama cha mkojo.

  1. Kipimo cha damu

Kipimo hiki huwa dhabiti na sahihi zaidi. Ila, haiwezekani kufanyia nyumbani. Kipimo cha aina hii kina hitaji utaalum na kinafanyika kwenye maabara ama zahanati. Kina uwezo wa kudhibitisha ikiwa mwanamke ana mimba baada ya siku 6 ama 8 za kufanya ngono isiyo salama. Tofauti na kipimo cha mkojo ambapo matokeo yake yana onekana kwa kasi, kipimo hiki huchukua muda kidogo kabla ya matokeo kubainika.

Kipimo hiki huwa na malengo mawili, na haya ni: 

  • Kupima uwepo wa kichocheo cha HCG. Kipimo cha aina hii huwa na mafanikio kinapo fanyika baada ya siku 10. Kina dhibitisha kuwepo ama kutowepo kwa kichocheo hiki kwenye mkojo.
  • Kupima wingi wa kichocheo cha HCG. Kipimo hiki hupima idadi ama wingi wa homoni hii kwenye damu. Faida nyingine ya kipimo hiki ni kusaidia kujua matatizo yoyote katika kipindi cha mimba. Kupitia kwa kipimo hiki, daktari anaweza jua ikiwa mimba ilitungwa nje ya kizazi.

2. Kipimo cha mkojo

Kipimo hiki huwa cha kasi, rahisi, cha bei nafuu na kinaweza fanyika nyumbani ama hospitalini.

Unapo fuata maagizo ya kukitumia ipasavyo, utapata matokeo ya kweli. Maagizo yake ni rahisi kufuata.

Vipimo hivi vya mimba huwa na usahihi wa asilimia 99. Ukiamua kutumia mbinu yoyote ile ya kupima mimba, kipimo cha asili cha kupima mimba ama kipimo cha damu, una nafasi asilimia 99 ya kupata matokeo sahihi.

Ukigundua kuwa una mimba, hakikisha kuwa unaenda kwa kituo cha afya ikiwa ulifanyia kipimo chako nyumbani. Daktari atakushauri jinsi utakavyo anza utunzaji kabla ya kujifungua.

Soma PiaIshara 5 Kuwa Unapaswa Kufanya Kipimo Cha Mimba

Written by

Risper Nyakio