Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Kipimo Bora Cha Kupima Mimba Kwa Upesi

3 min read
Kipimo Bora Cha Kupima Mimba Kwa UpesiKipimo Bora Cha Kupima Mimba Kwa Upesi

Yai linapopevuka kisha kurutubishwa huchukua muda wa kati ya siku tisa hadi kumi na nne ili kujipandikiza kwa ukuta wa uterasi.

Kabla ya kuelewa juu ya vipimo vya mimba, ni vyema kuelewa mambo ya msingi ya ujauzito. Yai linapopevuka kisha kurutubishwa huchukua muda wa kati ya siku tisa hadi kumi na nne ili kujipandikiza kwa ukuta wa uterasi. Hili ni muhimu kufahamu ili kujua ni wakati upi mwafaka wa kupima mimba ili kupunguza wasiwasi .Pia kupunguza gharama ya kurudia rudia vipimo. Kipimo cha haraka cha mimba  ni jambo la furaha kwa wanaotarajia na wale wana wasiwasi.

Pindi yai lililorutubishwa linapojipandikiza kwa uterasi, mwili huanza kutoa kichocheo kinachoitwa hcg(human chorionic gonadotropin). Kuwepo kwa hii homoni mwilini ndio thibitisho kamili la ujauzito.  Vipimo vya nyumbani hutazamia kupata hii homoni kwenye mkojo. Mwanzoni , hiki kichocheo huwa kwa udogo sana mwilini lakini mimba inavyozidi kukua ndivyo huongezeka mwilini.

Vipimo vya mimba

kipimo cha haraka cha mimba

Unaweza kupata vipimo vya mimba bila ya ushauri wa daktari. Kutoka kwa duka la dawa au mtandaoni. Vipimo vingi vya nyumbani huwa na stripu ambazo hugeuka rangi iwapo hCG ipo kwenye  mkojo.  Na iwapo vipimo hivyo ni vya kijidigitali huwa na matokeo ya ujauzito ama hauna ujauzito kwenye skrini

Tofauti kati ya vipimo vya nyumbani na vya hospitalini

Wengi hufikiria vipimo vya hospitalini ni vya haraka kuliko vya nyumba lakini la. Homoni inayoashiria ujauzito  yaweza kupatikana aidha kwenye mkojo ama kwenye damu. Vipimo vya nyumbani haswa huzingatia kupata hii homoni kwenye mkojo. Na  wakati wa asubuhi ambapo viwango huwa juu kabisa ndio huwa mwafaka. Vipimo vya hospitalini vya mkojo ni sawia na vya nyumbani. Vipimo  vya damu halikadhalika hufanyika tu hospitalini.

Vipimo vya damu hususan huwa vya aina mbili, moja huweza kuangazia kama kuna hCG kwenye damu na hio nyingine hutafuta kiwango cha hCG kwenye damu. Hivi vipimo si vya haraka kama vya mkojo. Manufaa ya vipimo vya damu ni:

  • Inaweza kugundua kiwango kidogo cha homoni hCG hivyo basi kutambua ujauzito ata ukiwa mchanga sana.
  • Huweza kutambua ujauzito una miezi ama siku ngapi.
  • Huonyesha afya ya mimba.

Muda wa vipimo tofauti vya mimba:

kupima mimba kutumia kitunguu maji

Kipimo cha damu huchukua muda mrefu ikilinganishwa na vipimo vya mkojo. Na pia gharama yake huwa juu kwa sababu ya ubora wake na uhakika wa matokeo. Vipimo vya mkojo huwa mara mbili. Kuna vile vya kawaida na vya kijidigitali. Stripu hizi  hufanya kazi kwa kuweka sehemu ya kupimia kwenye mkojo ama kuweka kwenye mkojo unaotiririka ili kulowa. Stripu hukupa matokeo baada ya dakika tatu hivi hivyo hupendwa na wengi na pia bei yake ni nafuu. Stripu za kijidigitali hukupa matokeo kwa chini ya dakika moja. Hivyo basi kama una wasiwasi mwingi ama unataka vipimo vya haraka stripu ya kijidigitali ndio chaguo bora zaidi. Kumaanisha, stripu za kijidigitali zinaweza kusaidia kupunguza wasiwasi. Pia ni rahisi sana kutumia.

Hukuonyesha kwenye skrini  unafaa kungojea muda  gani kabla ya matokeo kamili. Majibu yake hujionyesha  kama una ujauzito ama hauna ujauzito kwa screen. Hakuna kazi ngumu ya kusoma ishara, laini ama maumbo. Huu urahisi umeipa stripu ya kijidigatli umaarufu sana. Pia ina uwezo wa kuonyesha una ujauzito wa siku ama miezi ngapi.

Hivyo kipimo cha haraka cha mimba ni cha mkojo na kile cha kijidigitali.

Chanzo: WebMD

Soma pia: Kwa Nini Kupima Mimba Mapema Sana Hakushauriwi?

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Kipimo Bora Cha Kupima Mimba Kwa Upesi
Share:
  • Jinsi Ya Kutumia Kipimo Cha Mimba Kupima Iwapo Una Mimba

    Jinsi Ya Kutumia Kipimo Cha Mimba Kupima Iwapo Una Mimba

  • Vipimo Vya Kudhibitisha Kuwepo Kwa Mimba

    Vipimo Vya Kudhibitisha Kuwepo Kwa Mimba

  • Vipimo Asili Vya Mimba Vya Kubaini Kuwepo Kwa Mimba

    Vipimo Asili Vya Mimba Vya Kubaini Kuwepo Kwa Mimba

  • Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

    Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

  • Jinsi Ya Kutumia Kipimo Cha Mimba Kupima Iwapo Una Mimba

    Jinsi Ya Kutumia Kipimo Cha Mimba Kupima Iwapo Una Mimba

  • Vipimo Vya Kudhibitisha Kuwepo Kwa Mimba

    Vipimo Vya Kudhibitisha Kuwepo Kwa Mimba

  • Vipimo Asili Vya Mimba Vya Kubaini Kuwepo Kwa Mimba

    Vipimo Asili Vya Mimba Vya Kubaini Kuwepo Kwa Mimba

  • Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

    Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it