Je, Kipimo Cha Mimba Kinaweza Kudanganya?

Je, Kipimo Cha Mimba Kinaweza Kudanganya?

Sababu zinazo fanya kipimo cha mimba kuwa na matokeo hasi.

Huenda ulichukua kipimo cha mimba ukiwa nyumbani na matokeo yake ni hasi. Lakini je, huenda ikawa kuwa matokeo haya si ya kweli? Kuna visa na hadithi nyingi za wanawake ambao husema kuwa hawakujua kuwa walikuwa na mimba hadi pale wanapofika miezi minne. Naam ni kweli na kwa wanadada ambao tumbo zao hazionekani kwa sana, jambo hili ni kawaida sana. Najua swali lako ni je, hili linawezekana vipi? Linawezekana pale ambapo kipimo cha mimba kinatoa matokeo hasi. Je, kipimo cha mimba kweli kinaweza kudanganya? Kuna sababu nyingi ambazo huenda zikafanya kipimo cha mimba kuwa na matokeo hasi ama yasiyo ya kweli.

kipimo cha mimba kinaweza kudanganya

Kipimo Cha Mimba Kinaweza Kudanganya: Sababu Ambazo Husababisha Kipimo Hasi

  1. Kufanya kipimo mapema sana

Kipimo cha mimba huonyesha matokeo ya kweli kikifanyika siku 6 baada ya kitendo cha kufanya mapenzi. Kwa wakati huu, homoni ya HCG huwa tayari imeanza kutengenezwa mwilini, ambayo ni homoni ya mimba. Baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi, nafasi za kipimo chako kuwa kweli ni asilimia 97. Ili kuhakikisha kuwa kipimo chako cha mimba ni cha kweli na matokeo yake yako sawa, hakikisha kuwa unakifanya baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi na wala sio kabla ya hapo. Kwani huenda ukapata matokeo yasiyo ya kweli. Ukipata kipimo hasi, rudi kipimo chako baada ya siku chache.

Je, Kipimo Cha Mimba Kinaweza Kudanganya?

2. Kutumia kipimo kilicho haribika

Unapaswa kuwa makini sana unapo nunua vifaa vya kupima mimba, hakikisha kuwa havija pitisha muda ambao vinapaswa kuwa dukani kwani hiyo ni sababu moja inayo fanya matokeo ya kipimo cha mimba kudanganya. Iwapo utagundua kuwa kipimo ulicho kitumia kime pitisha wakati, nunua kingine kilicho sawa kisha urudie kipimo chako.

Je, Kipimo Cha Mimba Kinaweza Kudanganya?

3. Kuchukua kipimo inavyo faa

Ikiwa ni mara yako ya kwanza kufanya kipimo cha mimba, hakikisha kuwa unafuta utaratibu ulio onyeshwa kwenye kisanduku kilicho na kifaa cha kupima mimba. Kuto fuata utaratibu huo huenda kukasababisha kuwa na matokeo yasiyo ya kweli. Pia una shauriwa kufanya kipimo chako punde tu baada ya kuamka kwani wakati huo kiwango cha HCG huwa kimekolea zaidi.

Kumbukumbu: afyatrack

Soma pia: Kipimo cha mimba kwa kutumia chumvi na mkojo

Written by

Risper Nyakio