Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Sababu 3 Kuu Za Matokeo Hasi Ya Kipimo Cha Mimba Hata Baada Ya kuwa Na Ishara

3 min read
Sababu 3 Kuu Za Matokeo Hasi Ya Kipimo Cha Mimba Hata Baada Ya kuwa Na IsharaSababu 3 Kuu Za Matokeo Hasi Ya Kipimo Cha Mimba Hata Baada Ya kuwa Na Ishara

Mwanamke kuwa na viwango vidogo vya homoni ya hCG, kufanya kipimo cha mimba mapema ama mimba kutungwa nje ya mji wa mtoto husababisha matokeo hasi.

Kuna sababu nyingi ambazo huenda zikamfanya mwanamke akose kupata kipindi chake cha hedhi. Mara nyingi anapokosa kupata, wazo kubwa itakuwa kuwa ana mimba. Hasa kama ana ishara zingine zinazo ambatana na mimba, kama vile kuhisi kichefuchefu, kuumwa na mgongo, maumivu kwenye chuchu. Hizi ni ishara za mapema za kuwa na mimba. Mwanamke anapaswa kufanya kipimo cha mimba kudhibitisha hali yake. Kuna wakati ambapo kipimo hakita dhihirisha matokeo dhabiti. Je, kipimo cha mimba kinaweza kudanganya?

Kuna sababu tofauti ambazo zinaweza kusababisha kipimo cha mimba kutokuwa na matokeo hasi

matiti kuuma husababishwa na nini

Kipi kinasababisha kipimo cha mimba kuwa na matokeo hasi hata baada ya isahra za ujauzito?

Kuna sababu kadha wa kadha ambazo huenda zika sababisha jambo hili. Kama vile:

  1. Kufanya kipimo mapema sana

Mimba inaonekana kwenye matokeo ya kipimo baada ya kichocheo cha human chorionic gonadotropin (hCG) kutolewa mwilini. Ikiwa kiwango cha homoni hii kingali chini, kipimo hakita dhihirisha matokeo sahihi.

Kwa kawaida, baada ya mimba kutungwa, huchukua siku kumbi na mbili hadi homoni ya mimba (hCG) kuonekana kwenye mkojo wa mwanamke. Mama anapo fanya kipimo kabla ya muda huu, nafasi kubwa ni kuwa kipimo hakita dhihirisha matokeo sahihi. Hii ndiyo sababu kwa nini mwanamke hushauriwa kungoja siku kumi na nne kufanya kipimo cha mimba baada ya kukosa hedhi.

2. Mimba iliyo tungwa nje ya mji wa mtoto (uterasi)

kipimo cha mimba kinaweza kudanganya

Hata kama nafasi ya tukio hili ni changa, bado hutendeka. Mwanamke anapo tunga mimba kwenye mirija ya falopia,  nje ya uterasi, kutungwa kwa homoni ya mimba kutachelewa. Unapo fanya kipimo chako, kitakuwa na matokeo hasi. Ikiwa ulikuwa na ishara za mimba lakini kipimo kina onyeshana matokeo hasi, ni vyema kuwasiliana na daktari wako. La sivyo, enda kwenye kituo cha afya kilicho karibu nawe ili ufanyiwe vipimo tosha.

3. Viwango vidogo vya homoni ya hCG

Mwanamke anaye fanya kipimo cha mimba cha nyumbani anashauriwa kufanya kipimo hiki punde tu anapo amka. Sababu ni gani? Mara tu unapo amka kabla ya kunywa maji ama kuchukua kiamsha kinywa chako. Huu ndiyo wakati ambapo idadi ya homoni hii mwilini huwa nyingi.

Kwa hivyo itakuwa rahisi kugundua kupitia kwa kipimo ikiwa mama ana mimba ama la. Ukiamua kufanya kipimo hiki mchana, ngoja muda mkubwa bila kuenda msalani kisha ufanye kipimo hicho.

Kipimo cha mimba kinaweza kudanganya mambo tofauti yanapo tendeka. Mwanamke kuwa na viwango vidogo vya homoni ya hCG, kufanya kipimo cha mimba mapema ama mimba kutungwa nje ya mji wa mtoto. Sababu zingine za kupata matokeo hasi ni kama vile utumiaji mbaya wa kipimo ama kutumia kifaa kilicho pitisha muda wa matumizi.

Chanzo: healthline

Soma Pia: Uzito Wa Mapema Katika Mimba Una Athiri Saizi Ya Mtoto Anapo Zaliwa

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Sababu 3 Kuu Za Matokeo Hasi Ya Kipimo Cha Mimba Hata Baada Ya kuwa Na Ishara
Share:
  • Je, Kipimo Cha Mimba Kinaweza Kudanganya?

    Je, Kipimo Cha Mimba Kinaweza Kudanganya?

  • Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

    Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

  • Kipimo Cha Mimba Kinachukua Muda Upi Kuonyesha Matokeo?

    Kipimo Cha Mimba Kinachukua Muda Upi Kuonyesha Matokeo?

  • Utaratibu Wa Kufuata Unapo Soma Kipimo Cha Mimba Cha Kinyumbani

    Utaratibu Wa Kufuata Unapo Soma Kipimo Cha Mimba Cha Kinyumbani

  • Je, Kipimo Cha Mimba Kinaweza Kudanganya?

    Je, Kipimo Cha Mimba Kinaweza Kudanganya?

  • Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

    Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

  • Kipimo Cha Mimba Kinachukua Muda Upi Kuonyesha Matokeo?

    Kipimo Cha Mimba Kinachukua Muda Upi Kuonyesha Matokeo?

  • Utaratibu Wa Kufuata Unapo Soma Kipimo Cha Mimba Cha Kinyumbani

    Utaratibu Wa Kufuata Unapo Soma Kipimo Cha Mimba Cha Kinyumbani

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it