Vipimo vya mimba nyumbani vimekuwa maarufu sana hivi karibuni. Ila hiki kipimo cha mimba kutumia dawa ya meno kimekuwapo toka zamani. Kina uhalali kweli ama ni hadithi tu?
Kipimo Cha Mimba Kutumia Dawa Ya Meno

Kila wakati siku zako za hedhi zimechelewa wazo la kwanza huwa kupima ujauzito. Ila njia zinazoaminika zaidi ni kutumia kits za nyumbani ama kuwmona daktari. Unaweza kupata hizi kits kwenye duka la dawa ama kwa maduka kubwa. Vipimo hivi hupima kiwango cha homoni human chorionic gonadotropin(hcg) kwenye mkojo wa mwanamke. Pia daktari anaweza kufanya kipimo cha damu kwenye maabara na hiki huwa na majibu sahihi kabisa.
Kwa Nini Dawa Ya Meno Inaweza Kuwa Si Kipimo Bora Cha Mimba
Kipimo cha mimba kwa kutumiwa dawa ya meno huhusisha kuweka mkojo kwenye dawa ya meno iliyo nyeupe. Baada ya kuchanganya mtu huangalia kama kuna povu ama kubadilisha rangi. Hii inafaa kuashiria kuwa una ujauzito. Ilihali hii njia sio asilimia 100% sahihi ya kutambua ujauzito.
Nadharia nyuma ya njia hii ni kuwa kuna viungo kwenye dawa ya meno huchanganyika na homoni hcg kwenye mkojo. Huo mchanganyiko unafaa kusababisha dawa ya meno kubadilisha rangi ama kutoa povu. Ila haya majibu yanaweza kutokea kwa sababu ya ukali wa mkojo. Mkojo huwa na ukali na una pH ya 6.0 hadi 7.5. Aina tofauti za dawa za meno huwa na kiwango tofauti cha ukali.
Majibu ya ujauzito yanaweza kutokana na kuingiliana kwa kiwango cha pH kwenye mkojo na dawa ya meno iliyohusika. Kwa hivyo dawa ya meno si kipimo cha asilimia 100%. Kits ama vipimo vya nyumbani au vya hospitalini hutambua homoni hcg kwenye mkojo. Dawa ya meno haina uwezo wa kugundua hii homoni kwenye mkojo.
Vipimo Vingine Vya Nyumbani

Weka kijiko kimoja cha sukari kwenye bakuli. Ongeza mkojo kwenye lile bakuli. Ikiwa sukari itaganda kama cubes una mimba na iwapo sukari itachanganyika (dissolve) hauna ujauzito. Hormone hcg kwenye mkojo hufanya sukari kuganda kana kwamba cubes.
Hki hufanya kazi kama kipimo cha sukari. Mkojo na chumvi inafaa kuchanganywa kwa viwango vinavyotoshana. Iwapo chumvi itafanya kuganda una ujauzito na iwapo hakuna mabadiliko hauna ujauzito.
- Kipimo cha kutumia sabuni
Chukua Kipande kidogo cha sabuni. Mwagilia mkojo. Iwapo itafanya povu inamaanisha kuwa una ujauzito. Na iwapo hakuna hauna ujauzito.
- Kipimo cha kutumia baking soda
Tumia vijiko viwili vya baking soda. Ongeza kipimo kidogo cha mkojo. Tizama mchanganyiko. Iwapo itafanya povu kama vile unapofungua soda una ujauzito na kama hakuna hauna ujauzito
Jinsi Ya Kuongeza Uhakika Wa Vipimo Vya Mimba Nyumbani
- Tumia mkojo wako wa kwanza wa asubuhi kwani huwa na kiwango kikubwa cha homoni hcg
- Hakikisha kuwa unaweka mkojo wako kwenye kikombe au chombo safi
- Hakikisha kuwa umekusanya mkojo wa kutosha kufanya kipimo. Mkojo kidogo unaweza kuwa sio tosha kufanya kipimo
- Ngoja kwa dakika kumi kwa mchanganyiko au reaction kufanyika
- Pia unaweza kurudia kipimo au kutumia njia nyingine kuondoa shaka
Iwapo unataka kipimo cha mimba kisicho cha gharama ni vyema kuzingatia vipimo vya nyumbani. Mojawapo ni kipimo cha mimba kutumia dawa ya meno.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Dalili 5 Zinazo Ashiria Hatari Katika Mimba Changa