Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

Njia rahisi ya kupima mimba kwa kutumia simu yako.

Teknolojia imerahisisha vitu vingi. Kwa muda mrefu, mabinti wamelazimika kutumia njia tofauti kupima mimba. Kutoka kwa vipimo vya kinyumbani ama kutembelea zahanati kupata bidhaa za kupima kuwepo kwa mimba au la. Teknolojia iliyoko inawasaidia kufanya kipimo cha mimba kwenye simu wanapokuwa pahali popote pale.

Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu Na Jinsi Kinafanyika

Kuna njia nyingi za kupima mimba ambazo mwana dada anaweza tumia ila watu wengi hupenda kutumia njia ambayo inawakubalisha kuweka matokeo yale siri na pia kwa mazingara ambayo wamezoea. Mbinu za kupima mimba za kinyumbani zipo ambapo unaweza tumia bidhaa zilizo jioni mwako kupima mimba, kama vile kipimo cha mimba kwa kutumia chumvi. Ila, utafiti zaidi bado unaendelea kuhakikisha kuwa kipimo hiki ni dhahiri na kinaweza aminika. Kwa sasa, bado sio dhahiri iwapo unaweza kukiamini iwapo watu zaidi wanaendelea kukitumia. Kipimo cha mimba kwa kutumia simu ni rahisi na pia hakichukui muda mwingi. Pia unaweza kupima iwapo una mimba kwa mazingara uliyo yazoea bila juhudi za kwenda kwa zahanati ama hospitalini na kwa siri iwapo hungetaka wengine wajue unacho kifanya.

Kipimo Cha Mimba Kwenye Simu: Jinsi Kipimo Hiki Kinafanyika

kipimo cha mimba kwenye simu

Teknolojia hii ili vumbuliwa mwaka wa 2016 huko Umarekani. Kama kipimo chochote kile cha mimba, lazima uweke mkojo wako kwenye kijiti. Ila kwa kipimo hiki, teknolojia iliyoko kwenye kijiti kile ina tumia bluetooth kwenye app yako na kukupatia matokeo na kukujuza iwapo una mimba ama la. Kipimo hiki hakichukui muda mrefu ila ni dakika tatu tu. Huenda ukawa na mawazo mengi sana kabla kuyapata matokeo yako. Ni vyema kuhakikisha kuwa una jambo la kufanya ama usikize muziki huku ukingoja matokeo yako. Jambo hili linasaidia kuhakikisha kuwa haujikwazi kimawazo na kupunguza uwoga ambao huenda ukawa nao wa kupokea matokeo ambayo hukuya tarajia.

Mbali na kukusaidia kujua iwapo una mimba ama la, app hii inatumika kumkumbusha mama aliye na mimba muda ulio salia kabla ya kujifungua. Iwapo anapaswa kumwona daktari tarahe fulani, ni rahisi kukumbuka kwa kutumia app hii.  Utafiti zaidi unaendelea kuhakikisha kuwa matokeo unayo yapata kwa njia hii ni kamili.

Written by

Risper Nyakio