Njia Tofauti Za Kufanya Vipimo Vya Mimba Upesi

Njia Tofauti Za Kufanya Vipimo Vya Mimba Upesi

Shukrani kwa teknolojia, mbinu za kupima mimba zime imarika na ni rahisi kupata matokeo na kwa muda mfupi huku ukiwa nyumbani mwako.

Vipimo vya ujauzito ni muhimu sana katika kumsaidia mwanadada kufahamu kama ni mjamzito ama la. Kuna njia tofauti ambazo unaweza tumia kudhibitisha hali yako ya ujauzito. Shukrani kwa teknolojia, mbinu zime imarika na ni rahisi kupata matokeo na kwa muda mfupi. Hapo awali, mama ange ngoja kipindi kirefu kutoka siku tatu hadi wiki moja ili kubaini kama ana mimba ama la. Siku hizi kuna uwezekano wa kufanya kipimo cha mimba kwenye simu ukiwa nyumbani mwako.

Jinsi vipimo vya mimba vinavyo fanya kazi

jinsi ya kutumia kipimo cha mimba

Vipimo vya mimba hupima viwango vya kuchochea kwa homoni ya human chorionic gonadotropin (HCG) kwenye mkojo wa mwanamke ama damu. Mwili hutengeneza homoni hii baada ya yai lililo rutubishwa na mbegu ya kiume kujipandikiza kwenye kuta za uterasi.

Mchakato huu hutendeka siku sita baada ya yai kukutana na mbegu ya kiume yenye afya na kurutubishwa. Na kufanya kiwango cha HCG mwilini kuongeza mara mbili kwa kasi sana baada ya siku tatu.

Vipimo mbalimbali vya kudhibitisha mimba

Kuna aina mbili kuu ya vipimo vinavyo tumika kudhibitisha ujauzito wa mwanamke.

  1. Kipimo cha mkojo

Kufuatia ukuaji wa teknolojia unao shuhudiwa katika mwongo huu, kipimo cha aina hii kinaweza fanyiwa kwenye maabara ama hata nyumbani.

Kipimo hiki ni cha faragha, rahisi na upesi. Kuna vipima mimba ambavyo unaweza nunua kwenye maabara, zahanati ama kwenye duka za madawa. Ni rahisi kufanya na unaweza soma matokeo peke yako kwani ni rahisi kujua.

jinsi ya kufanya kipimo hiki

Weka mkojo wako wa asubuhi kabla ya kunywa kiamsha kinywa kwenye kontena safi. Unashauriwa kutumia mkojo wa asubuhi kwani una kichocheo zaidi. Fungua kipimo chako cha mimba na uweke kwenye kikopo. (zingatia ilivyo onyeshwa kwenye karatasi inayo andamana na kipimo hicho.

Weka kipimo hiko kwa njia hiyo kwa dakika mbili ama tatu ili kilowe. Usikiache kwa muda mrefu kwani huenda matokeo yaka athiriwa. Kisha usome majibu.

2. Kipimo cha damu

Kipimo hiki kinafanyiwa hospitalini kwenye maabara. Kinatumika kutambua kuwepo kwa mimba mapema zaidi, kabla ya siku kumi na nne (14). Kipimo hiki hupima kuwepo kwa homoni ya HCG na kichocheo cha homoni hii mwilini. Faida nyingine ya kipimo cha aina hii ni kuwa kinamsaidia daktari kujua iwapo kuna matatizo katika ujauzito. Kama vile ujauzito uliotungwa nje ya kizazi.

Jinsi ya kufanya kipimo cha mimba kwenye simu

kipimo cha mimba kwenye simu

Uvumbuzi uliofanyiwa mwaka ulio pita na kuvumbua Pregnancy PRO Digital Pregnancy Test & App Access. Unaweza pata app hii kwenye mtandao. Kipimo hiki cha mimba cha simu kinaweza kumwonyesha mwanamke kama ana mimba siku sita kabla ya kukosa kipindi chake cha hedhi. Na kina usahihi wa asilimia 99 katika kufahamu kuwepo kwa homoni ya mimba (HCG) kutoka siku anayo tarajia kipindi chake cha hedhi.

Kipimo hiki kinatumia bluetooth kudhibitisha majibu kwa kutumia app iliyo kwenye simu. Kwa kutumia application hiyo, unapata mwongozo wa hatua baada ya nyingine jinsi unavyo stahili kufanya kipimo hicho. Unapo subiri kupata majibu ya kipimo chako, una soma makala muhimu, kutizama video za kukutuliza na njia za kupunguza kukwazwa kifikira. Kipimo hiki kinachukua dakika 3.

Ikiwa kipimo chako ni hasi, unapata makala yanayo kusaidia kung'amua zaidi kuhusu rutuba yako ya uzazi. Na kama majibu ya kipimo chako ni chanya, unapata ujumbe kuhusu safari ya mimba.

Una shauriwa kuwasiliana na daktari ama kutembelea kituo cha hospitali baada ya kufanya kipimo cha mimba kwenye simu. Ili akuanzie utaratibu wa kujitunza kabla ya kujifungua.

Soma pia:Jinsi Ya Kutumia Kipimo Cha Mimba Kupima Iwapo Una Mimba

Written by

Risper Nyakio