Vipimo Vya Kudhibitisha Kuwepo Kwa Mimba

Vipimo Vya Kudhibitisha Kuwepo Kwa Mimba

Kipimo cha mimba cha nyumbani kwa ujumla huwa sahihi na utapata matokeo sahihi ukifuata  maagizo yaliyo orodheshwa.

Mara nyingi, unaweza fahamu ikiwa una mimba kwa kuangalia dalili za kawaida. Ikiwa una shuhudia mojawapo ya ishara hizi za ujauzito, unapaswa kuchukua kipimo cha mimba nyumbani ama hata kutembea kwa kituo cha hospitali ufanyiwe kipimo.

Kuna uwezekano wa kupata matokeo sahihi ya kipimo cha mimba siku moja baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi. Walakini, ni vyema kungoja angalau wiki moja baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi kuwa na uhakika kuhusu matokeo utakayo yapata.

Kipimo cha mimba nyumbani

kupima mimba kutumia kitunguu maji

Kipimo cha mimba nyumbani kinaweza tumika siku moja baada ya kukosa hedhi yako. Lakini kuna baadhi ya vipimo ambavyo vinaweza tumika mapema zaidi na kuonyesha matokeo sahihi.

Vipimo hivi vina gundua kuwepo kwa kichocheo cha HCG ama kwa kimombo, human chorionic gonadotrophin. Kichocheo hiki kina tolewa mwilini mwanamke anapokuwa na mimba. Kemikali inayo kuwa kwenye kijiti cha kupima mimba hugundua kuwepo kwa homoni hii na kubadili rangi.

Una shauriwa kufanya kipimo hiki mara mbili ili kupata matokeo sahihi. Huenda ikawa ulifanya kipimo hiki mapema sana na viwango vya kichocheo cha HCG kuwa kidogo sana kudhibitika. Kumbuka kufanya kipimo hiki inavyo faa kama ilivyo shauriwa kwa maagizo ili upate matokeo sahihi.

Kipimo cha mkojo hospitalini

Vipimo Vya Kudhibitisha Kuwepo Kwa Mimba

Unaweza fanyiwa kipimo cha mkojo kwenye hospitali iliyo karibu nawe ama zahanati. Vipimo hivi sio lazima kuwa ni sahihi zaidi kuliko vipimo vya kinyumbani. Walakini, daktari wako anaweza kusaidia kuondoa makosa yoyote ambayo huenda ika athiri usahihi wa kipimo chako. Kulingana na hospitali yako, huenda kipimo hiki kikawa ghali ikilinganishwa na kipimo cha mimba nyumbani.

Matokeo ya kipimo cha mkojo hospitalini kina tofautiana kulingana na kituo cha matibabu unacho tembelea. Walakini, mara nyingi, unaweza tarajia matokeo wiki moja baada ya kufanya kipimo chako.

Kipimo cha damu

Kipimo hiki kinafanyika kwenye ofisi ya daktari wako. Kipimo cha damu yako kinafanyika kwenye maabara kufahamu viwango vya hcg. Kipimo hiki huwa sahihi zaidi na kinaweza tumika kugundua ikiwa kuna matatizo yoyote kwenye mimba yako, ingali changa.

Hitimisho

Kipimo cha mimba cha nyumbani kwa ujumla huwa sahihi na utapata matokeo sahihi ukifuata  maagizo. Walakini, vipimo vya mkojo na damu ni muhimu ili kukuhakikishia usawa wa matokeo yako. Kulingana na matokeo yako, wasiliana na daktari wako na mchumba wako kuhusu hatua mtakazo chukua baada ya hapo.

Soma PiaJinsi Ya Kupima Mimba Ya Wiki Moja Bila Kutumia Vifaa Vyovyote

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio